Ushauri: Tatizo la kutojiamini

Aqua Man

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
336
Reaction score
1,146
Habari wana forum,

Mimi ni kijana mwanafunzi wa chuo kimoja hapa TZ, kiukweli nimekuja hapa kuwaelezea tatizo langu linalonisibu hivi sasa. Kiukweli nina shida ya kukosa kujiamini kabisa kwenye mambo tofauti tofauti kama kielimu na maisha ya kawaida, mfano kama kipindi cha examination ninakua na wasi wasi hata kwenye namba yangu ya mtihani ninayoandika nahisi kama nitakuwa naikosea.

Ushauri ndugu nifanye nini kuliepuka hili tatizo maana linanipa shida sana.

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Ulienda jandoni ukiwa na umri gani kijana?
 
mara nyingi maisha ya mtu anayoishi huchangia kuto kujiamini, mfano maisha ya kuwa isolated, muda mwingi upo alone, pengine ndo upo single kabisa (huna rafik wa other side {only if you're 18+}), mambo yako yatakuwa ya kutokujiamini mbele za watu.
aibu, kuna watu wanaonea aibu hadi watu wa jinsia yao, mtu wa hivi maisha yake anakuwa kama kunguru muoga muda wote.,
 
Kiukweli me sipendelei marafik sana, so inaweza ikawa sababu pia?

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli me sipendelei marafik sana, so inaweza ikawa sababu pia?

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
kwa hilo litakucost mkuu, unaweza ukawa unajua vitu vingi sana lakini publicly huwezi kujielezea. hiyo mbaya sana tena sana penda kukaa na watu japo kupiga story kama mwanafunzi shiriki sana discussion, presentation na public speech. usijali nani atakuonaje we changia tu.

mi nilikuwa na jamaa yangu huyo yaani yeye anaweza andaa assignment vizuri kabisa ila ukimwambia apresent alicho andika bure kabisa hadi kusoma anatetemeka.

jichanganye bila kujali status yako, sijajua umri wako ila kama school guy unachance kubwa ya kujibadilisha
 
Asante sana ndugu, still me ni mwanafunz second year. Na hayo unayoyasema yote kama unanizungumzia mm. Asante nashukuru kwa ushaur ntaufanyia kazi

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…