Ushauri Tafadhari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri Tafadhari!

Discussion in 'JF Doctor' started by Sebali, Jul 22, 2011.

 1. S

  Sebali Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenzenu nilipata ajali mwaka jana tar 24/10 ambapo nilianguka na baiskeli huko Iringa. Nilivunjika sehemu ya nyonga karibu na kiuno katika mguu wa kushoto.Nimekwisha hudhuria hospitali tofauti nilianzia hospitali ya mkoa wa mbeya, rufaa ya mbeya, CBRT, AMANA. Hivyo kutokana na mwingiliano wa shughuli zangu binafsi nilishindwa kufuatilia matibabu yangu kikamilifu mpaka mwisho. Mwezi march nilienda CBRT hapa dsm wakaniambia hawawezi kuweka chuma hiyo sehemu kwa vile nimechelewesha hivyo inabidi nifanyiwe 'hip replacement' ambapo gharama yake ni dola 5900. Hivyo mwezi huu nilienda Amana ili wanipe transfer ya muhimbili ili nione majibu yao. Hivyo waliniambia ngoja wachunguze kwanza wao, wakaniambia nikapige scan pale muhimbili nikawarudishia hapo Amana daktari akaniambia nyonga imekufa hivyo natakiwa niwekewe nyingine. Hivyo kanambia nikiwa tayari atanipa transfer muhimbili. Jamani naombeni kwa ushauri wowote au kama kuna daktari wa mifupa unayemufahamu pale muhimbili nipate ushauri wake hasa upande wa gharama? Nisaidieni mkulima mwenzenu!
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa mkasa uliokukumba, wajuzi watatoa taarifa zaidi.
   
 3. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,385
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pole sana ndugu mungu akitie nguvu ndugu yangu.
   
 4. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mie namfahamu Dr BAKI bingwa wa mifupa yupo kibaha
   
 5. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,849
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Pole sana mkuu, natumaini wataalamu watakusaidia.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,138
  Likes Received: 4,055
  Trophy Points: 280
  Ukifika Kibaha kwa Matias watu wa boda boda/taxi wanapajua, ni dr. mzuri. Be careful unaweza pata shida kubwa kama hautazingatia ushauri wa dr.
   
 7. S

  Sebali Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa mchango wenu wakuu, nitaufanyia kazi!
   
 8. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sana.
   
Loading...