Ushauri tafadhali

Ushauri tafadhali

laussane

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2009
Posts
255
Reaction score
132
Habari ya siku wapendwa,
Nisiwachoshe jamani ni hivi, nina sister wangu ni mtu mzima ana 42 yrs hivi, jana alipata mgeni ambae ana kama 26 yrs ni msichana ambae ameolewa 10 months now, mgeni alikuja kwa sister kwa kuomba msaada wa mawazo tatizo ni kwamba tangia ameolewa alikutana na mme wake faragha mara 2 tu, baada ya hapo kila siku mme anarudi saa 10 alfajili na akirudi amechoka anafikia kulala tu, anatoa huduma zingine zote isipokuwa kwenda faragha hakuna, huyu sister wangu alishawai sikia kuwa yule mme anachukuliwa na wanaume wenzake na hivo ata wakati wa ndoa yao watu walikuwa na minong'ono sana ya kuwa mmh hii ndoa itakuwa vipi, lakini huyu dada mwenye mume hafaham kabisa kuhusu hilo na fikra zake anawaza mmewe ana wanawake nje, inavoonekana hajawai ata kusikia hili kwa mtu mwingine, kampani ya mmewe ni wadada wa mjini ndio rafiki zake, tunamsaidiaje dada kama huyu maana ata huyu sister wangu wa 42 amekosa ushauri nayeye anahitaji mawazo yenu pia ili amsaidie binti katika mazingira ya amani, Brothers and Sisters tushirikiane kwa umoja wetu kama kawaida tutapata mwongozo.
 
Kwa bwana Yesu kila kitu kinawezekana, mshauri huyo dada akabidhi tatizo lake kwa Yesu
 
Ndoa hizi!! Mungu akisema wanaotaka kuachana nyosha mikono,,nadhani idadi itatisha.
::
ANXWAY
Anaemjua vizuri mumewe ni mke,,achunguze athibitishe.Kuna wazee ambao Mungu anawapa uhai kwa makusudi kama haya awashirikishe na kama ni mcha Mungu aombe msaada.
Kijamii wataalam wa ndoa wapo awashirikishe.
Vyovyote iwavyo anajua anampenda kiasi gani hivyo ndoa ipo mikononi mwake
=
 
Ndoa hizi!! Mungu akisema wanaotaka kuachana nyosha mikono,,nadhani idadi itatisha.
::
ANXWAY
Anaemjua vizuri mumewe ni mke,,achunguze athibitishe.Kuna wazee ambao Mungu anawapa uhai kwa makusudi kama haya awashirikishe na kama ni mcha Mungu aombe msaada.
Kijamii wataalam wa ndoa wapo awashirikishe.
Vyovyote iwavyo anajua anampenda kiasi gani hivyo ndoa ipo mikononi mwake
=

Ndiyo maana Mungu aliweka marufuku ya kuachana maana alijua hawa wapenda shortcut lazima watatumbukia huku tu.
Mwambie huyo dada akazane kusali, kufunga na kuomba, then atajua tu.
 
Mimi nadhani huyo dada atengenezewe mazingira flani ambayo yatamfanya hata akiambiwa jambo hilo asishtuke.
Nadhani inapaswa kuambiwa ukweli ili aweze kujikita kumuokoa mumewe katika hilo wimbi chafu linalomkumba.
 
Back
Top Bottom