ushauri tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushauri tafadhali

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by nachindundu, Aug 10, 2012.

 1. n

  nachindundu Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni kijana(wa kama miaka 23 hivi),na kama bahati nimebahatika kupata kazi sehemu flani,wananipa mshahara mkubwa tu,na niliowakuta kwenye department yangu,wengi ni wana umri karibia wa kustaafu,na hawana elimu sana (wengi wana certificate)...hapa ofisini nimepatiwa secretary ambaye ana umri kama mama yangu,,anapenda sana kazi yake na anajituma sana,na wote wanajishtukia niingiapo ofisini...wanachangamka nikiingia na misele inakua mingi
  kutokana na scenario hiyo hapo juu...je?
  1.ni vyema kumtuma mtu mzima ofisini?na je ni jambo la kawaida au ni kwangu tu?
  2.ni mambo gani natakiwa kufahamu ninapofanya kazi na watu wenye umri mkubwa kuliko mimi?
  3.je kama mkubwa anakosea nitumie njia gani kumkosoa au kumwelewesha?
  4.nitafanya nini ili kuwe na ka usawa flani ki umri maana siko comfortable pamoja nao,au labda sijazoea....,,,,na kama ingekuwa ni wewe ungefanyaje?

  ni mimi Nachindundu
   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hakuna job description katika kazi yenu? na vipi organisation chart haitaji wajibu wa kila mfanyakazi?
   
 3. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Kila mara wanapokosea hao watu wazima wafokee na kuwa rekebisha ipasavyo, ukisha fanya hivyo waache waendelee na kazi. Baadaye kwa muda wako muone huyo uliyemfokea(lazima atakuja 7bu wewe ni boss) Kwa sauti ya upole ongea nae kuhusu jambo lililokwisha kupita la kumfokea, Mwambia unasikitika sana kwa jinsi ulivyogomba muda ule, hukupenda bali wao ndio wanaokulazimisha. Msihi sana ajitume katika kazi ili kuepusha mambo kama yale yasijirudie tena. Hivi mnadhani mimi najisikia vizuri kumgombeza mtu kama wewe? Sipendi kabisa na wakati mwingi nafanya bila kujiona. Naomba tusiruhusu haya yatokee tena. Nimemaliza

  Kwa kufanya hivi, Huyo Mama/Baba atajua unamheshimu kwa umri wake ila kazi ndio inakulazimisha ufanye vile. Siku nyingi atajitahidi sana kuepusha hali ile isijirudie kwa kuchapa kazi vizuri. Kwa kufanya hivyo utakuwa umemuomba msamaha bila kushushusha heshima yako kama Boss. Kumbuka hii itafanya kazi kutegemeana na jinsi au namna utavyokuwa ukifikisha ujumbe huo. Achana na kuwapa mwanya wa kukujua namna ulivyo, maana wakikuzoea watakuwa wanakupeleka watakavyo na si utakavyo wewe. Leo kuwa rafiki sana kesho humjui mtu.

  Ukishindwa kuwaongoza utahatarisha nafasi yako na pia utatutangazia sifa mbaya vijana wote kuwa hatufai kupewa nafasi za juu za uongozi. Komaa sana. ikiwa kazi na iwe kazi tu, ikiwa urafiki na umama/ubaba iwe baada ya kazi
   
Loading...