Ushauri tafadhali: Wanangu wanakoelekea siko

ikibidi chukua simu zao watoto hao acha waje kuktana nazo huko mbele ya safari..mavazi kuwa mkali kama pilipili wataacha...mama akusaidie kwa huyo msichana upekuzi wa ghafula ufanyike wakat wa likizo...

kama ulikuwa unawaruhusu disco sasa marufuku..geti kali...acha afanye kwa kuibaiba lkn sio mbele ya macho yako

kuna watu wanakwambia eti ndio dunia yao, ukiwaacha tu wataharibika kabisa..

kuna rafiki yangu alimpa uhuru mwanae kuvaa hata vichupi badae kale kabint kakaanza pombe kakiwa kadogo sana sas mamake anahaha huku na kule motto wa form six full majanga..ni motto wa madisco na pombe za kumwaga yaani ni aibu
 
Mkuu kwanza hongera kwa kuwa na watoto wa umri huo na pia pole kwa changamoto za malezi. Watoto huwa wasiri mno kwa asili na mara nyingi wanatabia za aina mbili yaani mbele ya wazazi wapo tofauti na wanapokua mbali na wazazi wanonyesha tabia tofauti. Mkuu nami ni mzazi na kwa bahati nzuri nimeanza kulea wadogo zangu na sasa wanangu zipo changamoto nyingi. Nakumbuka niliamini sana malezi niliyokua nawapa na mbinu nilizokua natumia kugundua tabia zao lkn kumbe kuna ambayo yalikua nje ya uwezo wangu kuyagundua. Kipindi hiki cha maendeleo ya teknojia ndio usiseme, Unaweza ukawakataza kumiliki simu lkn bado haisaidii kwani kuna wenzao watakua na simu watatumia au wao wenyewe watakuficha kama wanamiliki simu, hapo hujazungumzia vitu kama facebook na mengineyo.

Unachotakiwa kufanya ni kukaa nao na kuwaeleza athari za mitandao na za kuweka picha zisizo na staha kwenye mitandao hii waeleze kwa kina ili waelewe unamaanisha nini. Usiache kuwa wazi machoni pao jadilini kila kitu kwa uwazi ikiwezekana wape nafac watoe mawazo yao . Zungumza nao faida za mitandao hasa inapotumiwa vizuri na hasara zake . Waelimishe pia athari za kujiingiza kwenye mapenzi ktk umri mdogo na hasa ukikazia imani yenu bila kuacha kuzungumzia magonjwa, Ktk hili la mahusiano tumia muda wa mwingi kuongea nao .

Kuhusu nguo za ajabu hapo mkuu itakua ngumu mno kuwazuia ila usiache kuwakanya isipokua tegemea watafanya tu wakiwa mbali na nyumbani. Nakumbuka kijana wangu hapa huwa kila nikimbamba ananipa kiswahili na kuniweka sawa kama kwamba mie kipofu sioni. Usiwe mkali kupita kiasi au usiover restrict kila kitu kiwe kwa kiasi naamini kwa njia ya majadiliano mtakua sawa.
 
asante sana Ablessed, nimekupata vizuri mkuu
 
Last edited by a moderator:
Sina imani na 'Mshua' huyu.

Yeye ameomba watu wawe siriasi wakati mwenyewe hayupo hivyo.

Lugha uliyoitumia ina harufu na rangi ya Kijana, Sio mtu mwenye watoto wa kuwa ngazi uliyosema,
Pili, Umeulizwa umri wa watoto unasema mtu akadirie,
Kwani ingekugharimu kiasi gani kusema?

-Stop pretending.
 
wapi hujaelewa mkuu? uliza nifafanue

maneno kama malavidavi, kusepa bana, hayo ni maneno ambayo hao unaoita wanao ndiyo wanapaswa kusema. inaonyesha wamefata nyayo zako mito
 
Last edited by a moderator:
maneno kama malavidavi, kusepa bana, hayo ni maneno ambayo hao unaoita wanao ndiyo wanapaswa kusema. inaonyesha wamefata nyayo zako mito

ahaa mkuu mie nimenogesha jukwaa tu ujue
Daah, sasa hat humu unataka tuandike kiheshima heshima looh!! ndo maana tunajificha kwenye hizi ID zetu feki
 
Mbona unaandika kama kijana wa leo huonekani kama ni mtu mzima ambaye anawatoto wakubwa Wa A level

Aisee mi nakaribia 50 usione kujimwaya mwaya hapa. Anyway ngoja nikukopie nilichomjibu pakaywatek
ahaa mkuu mie nimenogesha jukwaa tu ujue
Daah, sasa hat humu unataka tuandike kiheshima heshima looh!! ndo maana tunajificha kwenye hizi ID zetu feki
 
Last edited by a moderator:
Sina imani na 'Mshua' huyu.

Yeye ameomba watu wawe siriasi wakati mwenyewe hayupo hivyo.

Lugha uliyoitumia ina harufu na rangi ya Kijana, Sio mtu mwenye watoto wa kuwa ngazi uliyosema,
Pili, Umeulizwa umri wa watoto unasema mtu akadirie,
Kwani ingekugharimu kiasi gani kusema?

-Stop pretending.

Mkuu usinihukumu kwa lugha niliyotumia, yaani ulitaka niandike kiheshimaheshima ndo ujue mi mtu mzima nastahiri kuwa na watoto wa rika hilo??

Anyway whether it's a cooked story, still I believe there are people who will learn something out of this shit story of mine. We changia tu kwa roho nyeupe ukiamini kuna mtu atajifunza not necessarily mie, story ngapi hapa mkuu ni feki lakini bado tunachangia
 
Wakuu nina vijana wangu wawili, wa kike na wa kiume. Wote wako high school sasa. Kimasomo naona kama wanaenda vizuri ila kimaadili napata shaka kidogo hadi nimeamua kuomba muongozo kwa wadau wenzangu hapa.Wako shule tofauti na huwa nawasiliana nao kwa simu, call na texts.

Sasa mimi baba yao nilikuwa nyuma kidogo na hii technology ya whatsApp, simu yangu ilikuwa haisupport hii huduma halafu pia nilikuwa sina munkari nayo kivile. Sasa majuzi hapa nimenunua simu ya kisasa kuliko niliyokuwa nayo mwanzo ni hizi smartphone.

Sasa na mimi ndo sasa nikaamua kujiunga na haya ma-whatsApp. Katika kupekenyua huku na kule si nikaingia kwenye profile zao, daah. Vilivyoko huko sikutegemea kabisa, hayo maneno sasa ya malavidavi kwenye status zao, na yanavyobadilishwa kila siku, khaa nimechoka mwili na roho na hizo picha hivyo vivazi sasa ndo mimeishiwa nguvu kabisa, hata sijawahi waona wakivivaa nyumbani na hata sijui wanavipata wapi.

Kama mzazi najitahidi sana kuongea na wanangu, hadi huwa najipa imani kuwa wananielewa ila haya mambo yao ya kwenye mitandao ndo yamenipa mashaka sasa. Sijawauliza chochote hao watoto na wala hata wife sijamshirikisha. Nimeona nije kwanza kupata ushauri wenu kwa kunijibu mambo yafuatayo.

Je na wewe kama mzazi ulishawahi ona mambo kama hayo kwa vijana wako we uliyachukuliaje.Je haya ni mambo ya kawaida tu katika ulimwengu wa sasa hivyo niyapuuze,je nifanyeje mimi kama mzazi.

NB: Team kuponda tafadhali piteni tu huko pembeni, nitawashukuruni sana.

Pole ila naomba ku share na wewe Mimi kama mzazi huwa naongeaga ukweli na watoto wangu na wasifichi kitu kabisa na kitu kingine ni kwamba nimewaambia what I expect from them in terms Ya kuvaa kuongea na mambo Mengineyo nimeenda mbele zaidi na kuwapa masharti yangu kama mzazi mfano Kupata mimba au HATA kutoa mimba au kumpa msichana mimba na mambo mengine kama kutumia madawa Ya kulevya na MENGINEYO yaani wasitegemee kwamba eti atapata mimba Halafu Mie ntalea mjukuu au hata nikisikia ametoa mimba au eti katumia bangi au madawa Halafu Mie nianze hangaika Naye aache nimewaambia vyote nnavyotaka na nsivyotaka na adhabu zake. Kuongea na watoto ni muhimu ila naona kuna umuhimu sana wa kiset standards ntakuwa firm Kwenye adhabu
 
thanks mkuu, good experience
 
lara 1 nasubiri kusikia maoni yako aisee
just be you, mi siyo kama yule mdada anayetaka kusikia yanayomfurahisha tu
 
Last edited by a moderator:
maendeleo yao shuleni yakoje.

Kama wanajitambua umshukuru Mungu wako.
 
Kaunga leo nimekuona hapa jukwaani, i want to hear something from you. Of course from others as well
Aisee pole sana na changamoto za malezi. Hapa katikati nimepitia changamoto kibao na bado naendelea nazo. Kikubwa wewe mwenyewe kuwa karibu sana na Mungu halafu mkabidhi familia yako "mimi na nyumba yangu yutamtumikia Mungu". Pili waintroduce na wao kwenye kumtafuta Mungu sana. Tatu ukiweza zuia matumizi ya simu au wabadilishie wape nokia torch kwa ajili ya kupiga na texts tu. Lakini vyote hivyo vifanyike kwa dialogue ya hali ya juu nao ukiwaeleza faida na asala za utandawazi wa kidot com.
Ni ngumu sana lkn lazima tu keep on trying bila kuchoka.
 
thanks Kaunga, nimefarijika sana kukusikia, it's so long
pole na wewe na hizo changamoto za maisha
 
Last edited by a moderator:
maendeleo yao shuleni yakoje.

Kama wanajitambua umshukuru Mungu wako.

actually hiki ndo huwa kinanipumbaza hata nachukulia na mambo mengine ya kimaadili yanaenda sana. Manake maendeleo yao shuleni yanaridhisha, na tabia zao nyumbani au machoni mwetu ni njema, ila kumbe huko nyuma ya pazia kuna vituko vinaendelea
 
Kama wako vizuri kichwani ongea nao kirafiki ukiwakumbusha wajibu wao kwao; familia; jamii na taifa zima.

Wape mifano ya watu walioweza kimaisha.

Usisemee saaaana hadi wakaanza kujihoji kwani tumekosa sana.
 
thanks Mamndenyi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom