Ushauri tafadhali: Wanangu wanakoelekea siko

Ushauri tafadhali: Wanangu wanakoelekea siko

Wakuu nina vijana wangu wawili, wa kike na wa kiume. Wote wako high school sasa. Kimasomo naona kama wanaenda vizuri ila kimaadili napata shaka kidogo hadi nimeamua kuomba muongozo kwa wadau wenzangu hapa.Wako shule tofauti na huwa nawasiliana nao kwa simu, call na texts.

Sasa mimi baba yao nilikuwa nyuma kidogo na hii technology ya whatsApp, simu yangu ilikuwa haisupport hii huduma halafu pia nilikuwa sina munkari nayo kivile. Sasa majuzi hapa nimenunua simu ya kisasa kuliko niliyokuwa nayo mwanzo ni hizi smartphone.

Sasa na mimi ndo sasa nikaamua kujiunga na haya ma-whatsApp. Katika kupekenyua huku na kule si nikaingia kwenye profile zao, daah. Vilivyoko huko sikutegemea kabisa, hayo maneno sasa ya malavidavi kwenye status zao, na yanavyobadilishwa kila siku, khaa nimechoka mwili na roho na hizo picha hivyo vivazi sasa ndo mimeishiwa nguvu kabisa, hata sijawahi waona wakivivaa nyumbani na hata sijui wanavipata wapi.

Kama mzazi najitahidi sana kuongea na wanangu, hadi huwa najipa imani kuwa wananielewa ila haya mambo yao ya kwenye mitandao ndo yamenipa mashaka sasa. Sijawauliza chochote hao watoto na wala hata wife sijamshirikisha. Nimeona nije kwanza kupata ushauri wenu kwa kunijibu mambo yafuatayo.

Je na wewe kama mzazi ulishawahi ona mambo kama hayo kwa vijana wako we uliyachukuliaje.Je haya ni mambo ya kawaida tu katika ulimwengu wa sasa hivyo niyapuuze,je nifanyeje mimi kama mzazi.

NB: Team kuponda tafadhali piteni tu huko pembeni, nitawashukuruni sana.

vipi wewe wakati ukiwa na umri kama watoto wako ulikuwaje?? kimavazi,malavidavi??? unamwonaje mwanao kulinganisha na wewe ulivyokuwa teenager???
 
wapi hujaelewa mkuu? uliza nifafanue

Huyo jamaa nimemuelewa sana, yaani wewe njisi ulivyoandika mada yako na maswali uliyouliza pale mwishoni mwa mada yako na maswali unayoendelea kuyauliza hakiendeni na mada yako.

umetunga l ili kucheza na akili za watu, lakin nakushukuru umetumia vizuri fasihi kwa matukio wanayofanya wanafunzi wa vyuo na mtaani wewe umeyavaa ili yaweze kujadiliwa vizuri.
 
labda nikuulize wewe ni wa dini gan na shule wanayosoma inafata maadili ya dini? inakuwaje wanamiliki simu shuleni wanaruhusiwa?
mimi wa kwangu mdogo tu nilikuta ameangalia picha za xx kwenye simu yangu halafu akasahau kufuta sijui ndo hajui basi nikazikuta nilitembeza mkongoto ambao hata usahau na hadi leo huwa naacha simu kwa makusudi sijaona akirudia

lakini nmeongeza sana mafundisho ya dini ni lazima kusali sana...haya mashulle ya boarding sometimes hakuna kitu
 
vipi wewe wakati ukiwa na umri kama watoto wako ulikuwaje?? kimavazi,malavidavi??? unamwonaje mwanao kulinganisha na wewe ulivyokuwa teenager???

tofauti kabisa mkuu, mi ni wa 47 huko aisee
 
Wakuu nina vijana wangu wawili, wa kike na wa kiume. Wote wako high school sasa. Kimasomo naona kama wanaenda vizuri ila kimaadili napata shaka kidogo hadi nimeamua kuomba muongozo kwa wadau wenzangu hapa.Wako shule tofauti na huwa nawasiliana nao kwa simu, call na texts.

Sasa mimi baba yao nilikuwa nyuma kidogo na hii technology ya whatsApp, simu yangu ilikuwa haisupport hii huduma halafu pia nilikuwa sina munkari nayo kivile. Sasa majuzi hapa nimenunua simu ya kisasa kuliko niliyokuwa nayo mwanzo ni hizi smartphone.

Sasa na mimi ndo sasa nikaamua kujiunga na haya ma-whatsApp. Katika kupekenyua huku na kule si nikaingia kwenye profile zao, daah. Vilivyoko huko sikutegemea kabisa, hayo maneno sasa ya malavidavi kwenye status zao, na yanavyobadilishwa kila siku, khaa nimechoka mwili na roho na hizo picha hivyo vivazi sasa ndo mimeishiwa nguvu kabisa, hata sijawahi waona wakivivaa nyumbani na hata sijui wanavipata wapi.

Kama mzazi najitahidi sana kuongea na wanangu, hadi huwa najipa imani kuwa wananielewa ila haya mambo yao ya kwenye mitandao ndo yamenipa mashaka sasa. Sijawauliza chochote hao watoto na wala hata wife sijamshirikisha. Nimeona nije kwanza kupata ushauri wenu kwa kunijibu mambo yafuatayo.

Je na wewe kama mzazi ulishawahi ona mambo kama hayo kwa vijana wako we uliyachukuliaje.Je haya ni mambo ya kawaida tu katika ulimwengu wa sasa hivyo niyapuuze,je nifanyeje mimi kama mzazi.

NB: Team kuponda tafadhali piteni tu huko pembeni, nitawashukuruni sana.

Pole sana mkuu,
Umri unachangia ( Puberty & Foolish Age ). Well usipuuze kuwafatilia kwa karibu, wakunje angali wabichi otherwise utakuja washindwa...kua mkali na tabia na mavazi yao wanayovaa isije ikawachukua moja kwa moja. Wasistize kuhusu maadili ya Ukristo/Uislamu na maisha ya mu Africa. Uwe mbogo pale wanapokosa siku za ibada hii imenisaidia sana wakati nakua, leo hii mtu mzima nikikosa kwenda kanisani jumapili nahisi kuumwa cz nimeshazoea mafunzo na maadili nliofundwa. Ukali usiwe ule wa kuwacharaza viboko. BIG NO.

Uwe ni ule wa kuwafunza adabu kwa kauli, matendo na kifikra. Usiowaonee haya/aibu kuwaeleza kuhusu ujana na vishawishi vinavyowazunguka i.e zinaa, magonjwa, makundi mabaya....Last but not least usimfuge sana mtoto akishafika 18 of age mpe ka uhuru ila sio uliopitiliza.Naamini mpaka anafika 20 of age tayari anajua kizuri na kibaya na inakua vigumu kubadilika tabia. Binafsi na ukubwa huu kuna tabia ambazo hata niishi sehem gan na umri uzidi kwenda sintobadilika milele mpaka nakufa i think ni sabab ya malezi nliyolelewa na wazazi niko hvyo tu, ni kitu tayari kipo kwenye damu ngumu kubadilika.

Hata vitabu vya dini vinasema mtoto akishalelewa tabia na mwenendo flan wa maisha ni vigumu kuiacha hata atakapo kua mzee. Pia kama mfuko unaruhusu try ur best to keep them busy kipindi cha likizo.....short courses and studies to enhance their skills. Cz wakiwa too free ndio wanapata na muda wa kuwaza vitu vya kijinga.

I hope u get my point Brother. Best of Luck.
 
labda nikuulize wewe ni wa dini gan na shule wanayosoma inafata maadili ya dini? inakuwaje wanamiliki simu shuleni wanaruhusiwa?
mimi wa kwangu mdogo tu nilikuta ameangalia picha za xx kwenye simu yangu halafu akasahau kufuta sijui ndo hajui basi nikazikuta nilitembeza mkongoto ambao hata usahau na hadi leo huwa naacha simu kwa makusudi sijaona akirudia

lakini nmeongeza sana mafundisho ya dini ni lazima kusali sana...haya mashulle ya boarding sometimes hakuna kitu

ndio inafuata maadili ya dini za kikristo. Simu hawaruhusiwi kuwa nazo day time, lakini mida ya sas kumi na mbili jioni na kuelea wanakuwa nazo huko wanakolala mabwenini
 
Mimi mwenyewe nimemuuliza naona kimya! Isije kuwa kabadili mavazi!!

nikukuwa bado nawajibu wengine mkuu
ni vile vinavyokata makalio
 
Pole mzazi mwenzangu, ila nakutia moyo kuwa hayo ni mambo ya kawaida sana kwa kizazi hiki tena wakiwa na access ya mtandao ndio kabisaaaa, Ushauri; chamsingi usipaniki, vijana wanahitaji kuambiwa facts tena kwa kuwaheshimia sio kuwakalipia. wazazi wengi tunafanya makosa kuwakaripia badala ya kuwambia facts. kama wewe huwa unaongea nao basi unayofursa ya kukaa nao na kuongea nao juu ya tabia hatarishi.. wambie faida na hasara zake. alafu uwaache wenyewe wachague upande unaowafaa. kwa uzoefu wangu vijana ukikaa nao kama rafika na mkaongea mambo kwa uwazi mara zote nimeona wakifanya maamuzi ya afya kwao tena bila fimbo..ukiwakaripia wanafanya kiburi! na kwa kuwa wapo shule.. unaweza chart nao kirafiki kwa yale wanayopost pasipo kuonyesha ukari.. hapa tunasema inabidi uwe assertive .. unakaribia kwa hekima au upole! kila la kheri
 
vile vya kata Kund vile

sasa hio si kawaida tu,vi teenager vyote ndio vivazi vyao hivyo....sasa wewe kama mzazi wafundishe kuvaa suruali kiunoni,waeleze hivyo wanavyovaa sivyo,kupendeza sio lazima wavalie suruali makalioni.
 
yani hapa ndiyo naonaga ndiyo wakati mgumu sana kwa wazazi.......ila jitahidi kuongea nao ...hasa waeleze stage waliyopo......kwamba wanaweza kujenga au kubomoa maisha yao......
 
sasa hio si kawaida tu,vi teenager vyote ndio vivazi vyao hivyo....sasa wewe kama mzazi wafundishe kuvaa suruali kiunoni,waeleze hivyo wanavyovaa sivyo,kupendeza sio lazima wavalie suruali makalioni.

Kama umesoma vizuri maelezo yangu, nimesema wakiwa home wanavaa vizuri tu kwani nilishaongea nao khs suala la mavazi. Tena nisingejua kuwa wanavaaga hivyo huko, ni vile nimeingia kwenye profile zao na kuangalia picha zao wanazoweka huko PLUS maneno wanayoandika kwenye status zao
 
yani hapa ndiyo naonaga ndiyo wakati mgumu sana kwa wazazi.......ila jitahidi kuongea nao ...hasa waeleze stage waliyopo......kwamba wanaweza kujenga au kubomoa maisha yao......

umeona eeh
Asante kwa ushauri mdau
 
ndio inafuata maadili ya dini za kikristo. Simu hawaruhusiwi kuwa nazo day time, lakini mida ya sas kumi na mbili jioni na kuelea wanakuwa nazo huko wanakolala mabwenini

hiyo shule wanakosea sana.......mtu anasoma anawaza sms na missed calls atakazo kitana nazo akitoka darasani......

nadhani kuwaruhusu simu siyo sahihi kabisa.....simu walipaswa kukutana nazo wakiwa likizo tu........kama wazazi mnabidi mliseme hili katika vikao vya shule......simu si nzuri kwa wanafunzi......
 
Back
Top Bottom