Ushauri tafadhali: Tuliachana ila ananisumbua turudiane

Ushauri tafadhali: Tuliachana ila ananisumbua turudiane

teddy elias

Member
Joined
Jan 10, 2018
Posts
20
Reaction score
18
Mwenzenu naomba ushauri wenu,

Nipo katika mahusiano na mchumba wangu mwanzoni tulikua tunaishi vizuri tu baadae mabadiliko yakaanza kuwasiliana ikawa kwa tabu kidogo nilipomuuliza akasema tatizo kazini anabanwa sana hivyo simu si rafiki sana.

Nilipo endelea kulalamika juu ya mawasiliano kuwa hivyo akasema tuachane, alikurupuka kunipenda nami nikamwambia sawa hiyo ndo kauli nilikua nasubiri.

Tatizo ni kwamba juzi kanipigia simu sikupokea katuma meseji anadai amenifikiria sana yale maamuzi yalikua ya hasira tu anaumia kunitamkia vile.

Wadau amekua msumbufu sana nami nishakata tamaa kwa kauli alizonieleza.

Naomba ushauri maana amekua msumbufu sana.
 
kama mtu mwenye busara hawez kutafuta solution kupitia simu kama anajua kakosa basi lzima tu akutafute ana kwa ana akuchane live...maon yangu nayaacha hvyooo
 
tatizo ni kwamba yeye yupo mkoa mwingine kikazi yupo dar nami nipo arusha masomon
 
Alikuwa anakupima msimamo wako kaza uzi mwanaume hajaribiwi aliyekuwa naye kambwaga kaona heri arudi kwako mwambie nina mtu tayari siwezi miliki wawili aendelee tu
 
mwenzenu naomba ushauri wenu,nipo katika mahusiano na mchumba wangu mwanzoni tulikua tunaishi vizuri tu baadae mabadilikomyakaanza kuwasiliana ikawa kwa tabu kidogo nilipo muuliza akasema tatizo kazin anabanwa sana hivyo simu si rafiki sana,nilipo endelea kulalamika juu ya mawasiliano kuwa hivyo akasema tuachane alikurupuka kunipenda nami nikamwambia sawa hiyo ndo kauli nilikua nasubiri.tatizo ni kwamba juzi kanipigia sim sikupokea katuma msg anadai amenifikilia sana yale maamuzi yalikua ya hasira tu anaumia kuniatamkia vile,wadau amekua msumbufu sana nami nishakata tamaa kwa kauli alizo nieleza.naomba ushauri nimjibuje make amekua msumbufu sana
sasa mkuu hata hili unataka third Part akushauri cha kufanya? Unashindwa nini kumblock? Unashindwa nini kumwambia kuwa Nafasi hiyo ilishajaa humhitaji tena? Au umeshindwa nini kumuweka kwenye black list? Yaani Njia zote hizo unashindwa hata kutumia mojawapo kufikia uamzi wako mpaka uje humu? au huna alternative???
 
Nilichogundua wenye cases kama hizi(na mimi nilishawahi kuwa nayo na nikaileta humu kushauriwa) huwa tayari tunakuwa na majibu/maamuzi yetu

Mi naona ufanye kile moyo wako utapenda mama angu
 
Back
Top Bottom