Ndugu zangu wana JF nawaombeni ushauri wenu wa dhati kabisa. Nimenunua Fuso Tipper kutoka Japan na gari limefanya kazi wiki mbili tu na kusimama. Aina ya gari hili lina engine tofauti na magari ya zamani yaani 16 na 17D. Gari ni ya mwaka 2005 na natumaini engine yake 450m. Nimejaribu kulitengeneza bila mafanikio. Nakosa usingizi kwa ajili ya tatizo la gari hili japo sikukopa mahali. Nisaidieni ushauri.