Compact Ltd
Member
- Apr 15, 2015
- 8
- 0
Habarini wanajamvi,
Nimeamua kuja na ID ngeni hapa, kwa unyeti wa suala lenyewe, ikizingatiwa kuwa nina miaka saba hapa JF tena ni verified user, sio kawaida hili ninalotaka kunena leo nikawa huru kwa ile ID yangu.
Habari iko hivi
Mwezi April nilikuwa nimeenda nchi jirani katika mihangaiko ya kutafuta ridhiki, nikiwa huko nikakutana na mzee mmoja wa makamo hivi maeneo ya mashambani, kiukweli mi ni mtu wa utani, tulizungumza mengi sana huku tukitaniana, na hadi narudi ndiye alikuwa rafiki yangu kwa kule.
Siku moja kabla ya kuondoka tukawa tunazungumza stori za mahusiano, hadi nikajikuta namweleza my relationship history, jinsi nilivyosalitiwa na mchumba angu katika wakati mgumu na hatua za mwisho za kufunga ndoa.Mzee akaniambia kesho yake, siku ya kuondoka atanipa "zawadi" na ana imani nitaipenda tu. Asubuhi ikafika, mzee akawa kama mtu aliyesahau vile nami muda wa kuondoka umekaribia, nikamkumbusha..
Mzee kaingia ndani katoka na "habari nyingine" na akaniambia hiyo ndio dawa ya kumfunga mwanamke akifanya mapenzi na mwanaume mwingine watanasiana, yaani uume utashindwa kutoka sehemu za siri za mwanamke hadi uwategue ndipo sehemu zao zitajiachia.
Nilifadhaika kwa kweli, kwani toka nizaliwe sijawahi kujihusisha na mambo haya ya kienyeji, pili imani yangu hainiruhusu, ila upande mwingine ukiniambia "kweli kamzizi haka kanaweza fanya mambo yote hayo?" nikajipa moyo kwani nimewahi kusikia habari hizi kwa muda, ila kwangu ilikuwa kama ngano tu.
Nikarudi Tanzania, dhamira sasa nikataka kujaribu kama kweli ile "zawadi" inafanya kazi, sijaoa, sasa nitafanyeje? Nikamwita mpenzi, nikaijaribu kwake(lakini hakujua), kwa kuwa naamini na tuna ugomvi kwa muda sasa nikimtuhumu anatoka na jamaa, na jamaa nilimuonya, nikajua kama dawa ya kweli haitachukua muda nitamnasa, kisha nikamwambia likitokea lolote anijulishe.
Haikupita hata masaa 12 nikapigiwa simu na rafiki wa mpenzi wangu akinieleza tukio lililotokea huku akinisihi niende haraka, nami nikamwomba asimweleze mtu yeyote. Nikaenda na nikawafanya waseparate, kisha nikamwambia yule jamaa kuwa lengo lilikuwa kutaka kujua ukweli, kisha nikawatakia maisha mema.
Sikutaka watu wajue tukio lile kwa hofu kuwa wanaweza kusikia wazazi wa binti ikawa tatizo kwani sina mamlaka ya kumwekea wivu mtoto wao hence sio mke wangu pia itakuwa nimemdhalilisha binti yao.
Nimeandika kutaka kuomba ushauri, kwani nafsi bado inasita sana;
1. Je ni sahihi kumfanyia mke wako dawa ya namna hii?
2. Je huu si sawa na uchawi tu?
3. Je kwa kijana kumfanyia mkeo dawa ya namna hii si kuonesha kutojiamini na wivu?
MUHIMU: Nimeandika kwa urefu ili kutoa mwanga kwa kilichotokea ili nipate michango iliyopimwa kwa mazingira husika