Zingatia sana ushauri huu uliopewa hapo juu. Hata hivyo usiharakie kumweleza mwenzako. Mi nakushauri warejee wazazi wako mara tatu kuwasihi. Ikiwa mara zote tatu watakuwa wamekataa, nakusihi sana uwasikilize kama sababu zao ni za msingi kwasababu thawabu zao zina maana kubwa sana maishani mwako. Sisi tungepata nguvu ya kukushauri kama ungetueleza kwa kina sababu za wazazi kumkataa. Kama kweli unataka ushauri toka kwa watu ni vyema ukaweka wazi mpenzi wako ana background mbaya zipi ambazo wazazi wako wanazijua kuhusu mpenzi wako???
Tuambie ili tujue tukuunge mkono ww au wazazi.
Asikudanganye mtu; Safari ya ndoa ni zaidi ya mihemko ya mapenzi ndugu yangu; ingia kwenye ndoa ndio utajua ukweli. Sisi tulio kwenye ndoa tunajua thamani ya mke mwema na mwenye kibali mbele za Mwenyezi MUNGU. Usiwadharau wazazi wako kwa maana wakati mwingine Mwenyezi MUNGU hunena kupitia vinywa vya watu wa karibu yako. Mwenyezi MUNGU anajua zaidi, naomba kuwasilisha.