Ushauri tafadhali: Mpenzi wangu kakataliwa nyumbani

Ushauri tafadhali: Mpenzi wangu kakataliwa nyumbani

Mimi alikataliwa home baada ya wazazi kigundua alishazaa, nilimficha sana siku moja nikaamua kumwambia alilalama sana akanitishia kunywa sumu afe na biti nyingi tu mwishowe alielewa hivo nikawa huru.
Mwambie utakuwa huru
 
Tatizo mmeruhusu familia zenu zikawazoea sana kupita kiasi ndo mana kila kitu chako watakuamulia.
 
Daah!!..... Wanaume wengine hawana tofauti na wanawake!!..... Anaeoa ni wewe au ni familia mkuu?..... Wewe ndo unaeoa, achana na maagizo na masharti ya familia!!..... Mimi natamani sana hao wanaojiita 'familia' au 'ndugu' siku moja wamkatae mchumba wangu!
 
Daah!!..... Wanaume wengine hawana tofauti na wanawake!!..... Anaeoa ni wewe au ni familia mkuu?..... Wewe ndo unaeoa, achana na maagizo na masharti ya familia!!..... Mimi natamani sana hao wanaojiita 'familia' au 'ndugu' siku moja wamkatae mchumba wangu!
Haya mambo magum sana ndugu..haswa ww ukiwa ndo mkubwa ktk familia..usiombe yakukute
 
Ni vyema ifahamike kuwa ni kweli ww ndiye muoaji na mke ni wako na ww ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kwa maana ww ndiye utakayeishi nae. Lkn nakueleza ukweli kuwa hakuna kazi ngumu kama kuishi na mke/mume aliyekosa kibali cha familia hususani baba na mama. Itakugharimu tu na kujuta utajutia tu hasa kama walikupa sababu ambazo ni za msingi. Nakusihi tena na tena; tafadhali waendee wazazi mara tatu uwaombe wakuridhie, wala usilazimishe ridhaa yao kwa njia yoyote ile. Ikiwa mara zote tatu watakataa, hakika usimwoe huyo kwa maana atakuwa amekosa kibali muhimu sana hapa duniani. Kwasasa ushawaeleza wazazi mara moja bado mara mbili za mwisho.
Kama ni MCHA MUNGU, Amka usiku wa manane Muombe Mwenyezi MUNGU ushauri na akuongoze. Kumbuka amtegemeaye Mwenyezi MUNGU hajuti.
 
Wahenga walisema kuwa KUISHI KWINGI NI KUONA MENGI....wazazi wetu watukufu waliotangulia kuliona jua kabla yetu wamepitia mambo mengi maishani mwao....
Miaka mingi walioishi duniani kabla yetu imewakusanyia hazina kubwa ya busara na hekima.....kutokana na upendo wao kwetu wanajitahidi sana kuzitumia busara hizo na hekima na kuzielekeza kwenye maisha yetu ili tusiwe miongoni mwa watu wenye kujuta hapo baadae.....

Hakuna mzazi asiyemtakia mema mwanawe au asiyemtakia furaha maishani mwake....ndio maana kwa kipindi fulani anapokuwa anakuamsha asubuhi ya baridi kali ili wewe uende shule unaona kuwa ni kero kubwa sana kwako lakini baadae unakuja kuyaona matunda yake kwa kuwa na maisha mazuri na familia yako.....

Ndivyo ilivyo hata kwenye mapenzi wazazi wanajua nini maana ya ndoa kwa kuwa hata wao ni wanandoa na wanajua ili ndoa iweze kudumu na kuwa yenye furaha kunahitajika nini.....wanajua kuwa kukosea kuoa kunaweza kuyagharimu maisha yako kwa kiasi gani kwani ndoa ni jambo la kudumu maishani mwako...

Tatizo kubwa la vijana wanaongozwa na mihemko ya
mahaba wanapoliendea jambo la ndoa kuliko uhalisia wenyewe....wao wanadhani kuishi na mwenza kwenye ndoa ni sawa na kuishi na mbuzi au ng'ombe ambaye ataenda vile unavyotaka wewe....wakati kumbe mambo ni tofauti na vichwani mwao.....na wengi wao wameishia kujuta kwenye ndoa zao.....na hao waliobaki humo ni kama wapo kifungoni kwa maana ya mateso wanayoyapitia........

NB; Vijana muache kuongozwa na hisia kuliko uhalisia wa jambo lenyewe.....UZURI WA MWANAMKE SIO UREMBO NI TABIA.....na tabia njema ndio inayojenga ndoa na sio sura nzuri na umbo la kuvutia....
 
Mchuma janga hula na wa kwao, ushauri toka kwa ndugu zako huutaki ila unataka ushauri toja JF!!!
 
Wazazi hua wanaona mbali na akiwa amekata kutakua na sababu zamsingi ambapo hata wewe inabidi uambiwe sababu kwanini wamemkata ili na wewe uridhike je uliambiwa sababu? je sababu uliopewa is it valid reson?
na kuhusu msichana usimpoteze mda wake haitokua rahisi kuipokea lakini ni afadhali umwambie ajue
kuliko kumpotezea mda wake na sorry to say this,kwanini wazazi wako wanakuingilia kwenye maisha yako?
leo wamemkata huyu kesho watamkata mwengine,sasa hapa its not about your happiness anymore,ivi ukotayari
kuishi na mwanamke watakao kuchagulia wao hata kama humpendi?
 
Ukweli hukuweka huru". Lakini pia hata yeye akishajua hakubariki atachagua aendelee kuwa na wewe ama atafute ustaarabu mwingine,Kuficha ficha hakutamaliza tatizo ila kuliongeza kumbuka demu wako kuna wengine anawakataa akijua wewe upo na tayari hatua kazaa umemuonyesha.
Ndugu si sehemu ya mapenzi yenu lakini jua wanamsaada mkubwa kwenye maisha kwa ujumla.


Acha kumdanganya ndugu hawana msaada wowote, cha muhimu awe na kipato na aoe anayemtaka, ndugu wakija sawa na wasipokuja marafiki watakuja ambao kwangu mimi ni muhimu klk ndugu!
 
Wazazi hua wanaona mbali na akiwa amekata kutakua na sababu zamsingi ambapo hata wewe inabidi uambiwe sababu kwanini wamemkata ili na wewe uridhike je uliambiwa sababu? je sababu uliopewa is it valid reson?
na kuhusu msichana usimpoteze mda wake haitokua rahisi kuipokea lakini ni afadhali umwambie ajue
kuliko kumpotezea mda wake na sorry to say this,kwanini wazazi wako wanakuingilia kwenye maisha yako?
leo wamemkata huyu kesho watamkata mwengine,sasa hapa its not about your happiness anymore,ivi ukotayari
kuishi na mwanamke watakao kuchagulia wao hata kama humpendi?


Huwo ni upuuzi na ujinga kumpoteza mtu uliyeishi naye miaka minne kisa eti wazazi, wazazi wanawezaje kumjua mtu wako zaidi yako? Hawa wazazi acheni kuwapa nguvu wasizozistahili!
 
Umemsafisha asionekane mtu mbaya.... Hebu niambie una maana gani hapo....!?
 
Huwo ni upuuzi na ujinga kumpoteza mtu uliyeishi naye miaka minne kisa eti wazazi, wazazi wanawezaje kumjua mtu wako zaidi yako? Hawa wazazi acheni kuwapa nguvu wasizozistahili!
Wallah i can understand kama wazazi wana valid reason lakini wakwambie tuu huyu hatumtaki as if wanaishi nae wao,
hapo ndio mwanzo wakukuingilia maisha yako,uta end up kuoa mke wanaompenda wao lakini wewe humpendi na utaanza
kuzini kisa unawaridhisha wazazi.........
 
Mchumba akikataliwa na wazazi, kuwa makini sana na maamuzi yako. Mara nyingi nimeona waliong'ang'ania kuoa au kuolewa na waliokuwa wachumba wao wakiishi maisha ya taabu na majuto makubwa. Sikumbuki vizuri hiko kitabu katika Biblia Takatifu, inahoji, "Ni mzazi yupi awezaye kumpa jiwe mwanaye akimuomba mkate?" Wazazi wetu ni Mungu wa hapa duniani, ndo maana akapewa uwezo wa kukupa Mibaraka ukimpendeza na kukupa Laana ukimchukiza. Kuwa makini sana ndugu.
 
Wazazi hawampendi?..lkn wewe unampenda!..na wewe ndiyo muoaji!..kazi kwelikweli.
 
Habarini za weekend wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya njema..

Ni hivi mimi nina mpenzi wangu tuna miaka minne sasa toka tuanze mahusiano yetu na kama ilivyo kawaida mkiwa kwenye mahusiano lazima muwe na mipango mingi ya maisha yenu ya kifamilia hapo badae mungu akijalia.

Kwa kuwa nampenda girlfriend wangu nikaona si vibaya kama nikienda nae nyumbani waanze kumzoea na yeye kuwafahamu ndugu zangu wengine.

Sasa baada ya kumpeleka nyumbani siku chache mbeleni nikawekewa kikao cha familia na kuambiwa kuwa mtu nilienae hanifai, ana background mbaya na hawapo tayari kijana wao niende kwenye hiyo familia.

Nilijitetea sana kumsafisha mpenzi wangu aonekane si mtu mbaya kama wanavyosema ila juhudi zangu ziligonga mwamba kabisa, na kuniambia nisiende nae tena nyumbani siku nyingine.

Naomben ushauri, je nimwambie mpenzi wangu hali halisi ilivyo? Maana toka siku hiyo akiniambia habari za yeye walivyompokea nyumban nafsi yangu inakuwa inanisuta..naombeni ushauri juu ya hili.
Kwani unawaolea ndg zako? Kama umekaa naye miaka minne na umeridhika naye hao ndg zako ni kuwapa taarifa tu. Wewe ni mwanaume gani usiyekua na msimamo na maamuzi yako?
 
Kitu kizuri kipate baraka za wazazi......kama wamesema ana background mbaya wasikilize dehemu nyingine si za kukimbilia kisa wampenda.........

Jitahidi kukaa na wazee wakueleweshe vizuri.....
 
Kama unampenda sidhani kama familia inanafasi
 
Back
Top Bottom