jem_the_great
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 289
- 158
Habarini za weekend wakuu, Natumaini wote ni wazima wa afya njema..
Ni hivi mimi nina mpenzi wangu tuna miaka minne sasa toka tuanze mahusiano yetu na kama ilivyo kawaida mkiwa kwenye mahusiano lazima muwe na mipango mingi ya maisha yenu ya kifamilia hapo badae mungu akijalia.
Kwa kuwa nampenda girlfriend wangu nikaona si vibaya kama nikienda nae nyumbani waanze kumzoea na yeye kuwafahamu ndugu zangu wengine.
Sasa baada ya kumpeleka nyumbani siku chache mbeleni nikawekewa kikao cha familia na kuambiwa kuwa mtu nilienae hanifai, ana background mbaya na hawapo tayari kijana wao niende kwenye hiyo familia.
Nilijitetea sana kumsafisha mpenzi wangu aonekane si mtu mbaya kama wanavyosema ila juhudi zangu ziligonga mwamba kabisa, na kuniambia nisiende nae tena nyumbani siku nyingine.
Naomben ushauri, je nimwambie mpenzi wangu hali halisi ilivyo? Maana toka siku hiyo akiniambia habari za yeye walivyompokea nyumban nafsi yangu inakuwa inanisuta..naombeni ushauri juu ya hili.