Ushauri: Sijapata mtoto kwenye ndoa nahitaji wa kuzaa naye nje. Naumia kwa msongo wa mawazo (Depression)

Huna haja yakukata tamaa Mimi na mke wangu mwaka wa tatu bado hatujabarikiwa mtoto, hutukati tamaa, tunaamini IPO siku tutabarikiwa
Mkuu samahani lakini. Je kuna hatua yoyote ambayo mmechukua had wajati huu? Umeweza vipi ku handle pressure na kejeli toka kwa wanajamii?
 
Ok mkuu. Ndoa haiwezekani na ndo maana nimesema kuwa tayar nipo kwenye ndoa ila haja yangu kubwa ni mtoto na kwa mtu anayejitambua sio issue maana nikukubaliana kila kitu kuhusu uyo mtoto hata kabla hajazaliwa .

Watu wanabadilika Mkuu,zingatia hawezi kukosa tamaa ya pesa ata kama utamlipa vizuri,hii ni bongo siyo Uk wala USA,kila laheri ukifanikiwa uje na mrejesho
 
Kijana bado una mawazo ya vijiweni. Ndoa ina changamoto zaidi ya kukosa uzao. Kuzaa nje ya ndoa subiria mpaka ufikie 45yrs. Kumbuka ukizaa nje inapata first born ambaye piga ua mama yake atafanya miundombinu ya kisheria umrithishe hizo mali na baadae mke wako atashika mimba. Hapo ndo utajua kwa nini mtu mzima anakosa usingizi usiku.
 
Ninayo dawa ya mkeo kuzaa all i need ni report ya daktari na aliwahi kutoa mimba shida hasa nini halafu ndio tujie tunampa dawa gani nipo serious
Hajawai kutoa mimba yoyote ila hali ya kutokuona period hadi miez mi 3 ni hali aliyokua nayo toka zamani . Alifanyiwa vipimo akaambiwa ana vile viuvimbe vidogo ( ovary cyst) ambocho doctor halisema hakina madhara naxwadada wengi huwa navyo. Alipewa dawa za kumeza ili ku balance hormone (bigomet) ila bado period ibapitiliza.
 
Asante kwa ushauri. Hongera pia kwa kupata mtoto baada ya miaka saba . Kama hutojali pia naomba unishauri ulitumia dawa gani na ilikuaje ulikua hupati mtoto mwanzo ukapata mwaka wa saba? Najua pia kuna kujifunza kupitia experiences za watu wengine
Niligangaika sana hospital period ilikuwa haijakaa sawa niweza kaa miezi sita sijapata hakuna hospital sikwenda. Siku mojq daktari aliniambia siwezi zaa nililia sana niliyakataa hayo maneno ndio nikaanza kuomba.

Nilimuomba Mungu kwa imani sikukata tamaa. Miaka minne mfululizo nilikuwa naamka usiku ndani ya saa moja naomba.
Nilitafuta vifungu vyote kwenye biblia vinavyohusiana na uzazi nakili hivyo.

Mambo mengi ya uzazi ni tatizo la kiroho either unalijua au hulijui. Unavyomuomba Mungu atakuonyesha nini chanzo cha kukosa uzazi maana neno lake linasema hakuna tasa wala mwenye kuharibu mimba.

Usikate tamaa kutumia dawa ilimradi tu zisiwe za kutoka madhabahu ya shetani.
Pia hata virutubisho husaidia maana matatizo mengi ya homone yapo kwenye lishe.
 
Mzeya vipi tufanye exchange...mie nipenmkeo mie nikuoe gelofrend wangu maana ananisumbua anataka mtoto wakati mie sina mpamgo wakuwa baba maishani mwangu.

Huyo mke wako naona atanifaa mie

People have never cease to amaze me!!
 
Mkuu uko mkoa gan? Kuna familia huku nilipo nao walikuwa na tatizo kama lako lakin Hadi mda huu wanalea mimba. Walitumia miti Shamba na mambo yakawa safi,

Miti Shamba zinasaidia
Nipo Arusha mkuu. Kama hutojali naomba uniambie ata aina ya iyo mitishamba inbox
 
watu wanabadilika Mkuu,zingatia hawezi kukosa tamaa ya pesa ata kama utamlipa vizuri,hii ni bongo siyo Uk wala USA,kila laheri ukifanikiwa uje na mrejesho
Hahahaha anaialika vita nyumbani kwake. Mchepuko unakuzalia ilhali unajua una mke na watoto na bado unaleta tafrani kisa tu mtoto; imagine sasa mchepuko ukuzalie na huku mkeo hana mtoto. Lazima mchepuko atataka awe nafasi ya bi mkubwa. Achilia mbali ndugu wa mume wote watakaohamia kwa mchepuko in the name ametuzalia damu yetu. Ndoa yake itakuwa imevunjika hapo automatically. Mke hatokuwa na furaha tena. Mume lazima atahamishia mahaba yake na attention yake kwa familia yake mpya; hopeful hakutokuwa na kutoana roho kati ya wanawake

Nimekumbuka kuna school mate wangu fulani; walikaa muda mrefu na mumewe bila kupata mtoto. Me akachepuka akazaa nje, mke akachepuka akabeba mimba na akasema hata ndoa ivunjike sitoi hii mimba. Ndoa ilikuja kufa automatically
 
Tunasali sana tu na kutoa sadaka
Sadaka hainunui muujiza wala usijihesabie haki kupitia sadaka. Jenga imani yako kwa kusoma neno la Mungu. Imani huja kwa kusikia neno la Mungu. Kujihesabia haki mbele za Mungu kutachelewesha muujiza wako.
Na unaweza toka nje ya ndoa na Mungu asikupe huyo mtoto. Usicheze na Mungu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Niligangaika sana hospital period ilikuwa haijakaa sawa niweza kaa miezi sita sijapata hakuna hospital sikwenda. Siku mojq daktari aliniambia siwezi zaa nililia sana niliyakataa hayo maneno ndio nikaanza kuomba
Nilimuomba Mungu kwa imani sikukata tamaa. Miaka minne mfululizo nilikuwa naamka usiku ndani ya saa moja naomba.
Nilitafuta vifungu vyote kwenye biblia vinavyohusiana na uzazi nakili hivyo.

Mambo mengi ya uzazi ni tatizo la kiroho either unalijua au hulijui. Unavyomuomba Mungu atakuonyesha nini chanzo cha kukosa uzazi maana neno lake linasema hakuna tasa wala mwenye kuharibu mimba.

Usikate tamaa kutumia dawa ilimradi tu zisiwe za kutoka madhabahu ya shetani.
Pia hata virutubisho husaidia maana matatizo mengi ya homone yapo kwenye lishe.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Asante sana. kama una mchanganuo wa lishe uliokua unatumia naomba share na mimi
 
Back
Top Bottom