Ushauri: Sijapata mtoto kwenye ndoa nahitaji wa kuzaa naye nje. Naumia kwa msongo wa mawazo (Depression)

Hata me wanakuwa na msongo, ila kwa umri wake sijui kwa nini anakuwa namna hii. 31 bado kijana kabisa.
Nilipata scholarship ya kwenda kusoma Australia mwaka jana ila nikaacha ili nipate mtoto kwanza ila mambo hayajaenda sawa.
 
Mkuu usikate tamaa mbona wengi wanapitia changamoto kama zako lakini Mungu huwakumbuka.

Mimi baada ya kuoa nilikaa miezi 8 hivi hola japo kila mwezi wife ana bleed na tunatiana mwanzo mwisho, ikabidi niende hapo rabinisia hospital nikapewa dawa za kuimalisha sperm lakini wapi ikagoma, nikahama hospital nikaenda kairuki Kwa doctor mmoja maarufu kama Piere akamuandikia dawa ( nakumbuka ilikuwa kama lectrozole kama sijakosea) wife vidonge 5 nikalipia 10K, huwezi amani wife alimeza na mwezi huo huo akanasa.
Mbaya zaidi tukaona tusitumie majira Bali tutumie kalenda kutokana na changamoto tumeopitia yaani mtoto Ile kafika miezi 6 akanasa nyingine, hapa hata hamu Sina tena ya kutaka watoto.
Hongera mkuu i wish namimi nije kuwa na ushuhuda huu
 
Kuna kapo naifahamu, mwaka wa 12 huu bila bila. Mwamba yuko around 45 na bidada around 39 hivi.

Tuliza akili, kula vizuri, fanya mazoezi, piga misumari ya kwenda...nendeni mkaangalie afya zenu za uzazi, huenda kuna issue ndogo tu.
Asante kwa ushauri mkuu
 
Natumai wote mu wazima wa afya .

Mimi ni kijana wa miaka 31 kwasasa na toka niko na miaka 25 nilikua na hamu sana ya kupata mtoto na kuwa na familia kiujumla. Kama unavyojua maisha ya ujana kuna ujinga na makosa mengi tunafanya, nikiri kwamba nilifanikiwa kuwapa mimba mabinti wawili katika mahusiano ya nyuma katika vipindi tofauti, ila wote walizitoa kitendo ambacho kiliniuma sana sababu ikiwa ni mapema kwao kuwa mama maana pia bado walikua wanasoma na walikua kwa wazazi wao hivyo waliogopa kuzalia nyumbani.

Mwaka juzi mwez wa 4 nilifanikiwa kufunga ndoa na mimi na mke wangu hatuja fanikiwa kupata mtoto.

Mke wangu huwa hormone zake hazija balance na inaweza kupita ata miezi mi 3 hajaona period. Tumeenda hospitali na kutumia madawa ya kienyeji ila bado haijakaa sawa.

Nampenda mke wangu sana na nina msapoti sana ila nimefika maali nakata tamaa maana pia umri wanguunasonga na ninaumia sana kutokua na wakuniita baba.

NAHITAJI WA KUZAA NAE KWA MASHARTI MADOGO TU.

Sijawai kuwaza kutoka nje ya ndoa yangu kwani mimi sio mtu wa wanawake sana na muda mwingi nipo kimya na kwa umri wangu sasa sio mtu wakufikiria pisi bali kujenga familia.

Nahitaji mdada wa kuzaa nae tu ata mtoto mmoja tu na mimi niitwe baba maana kuna wakat nawaza napambana sana kutafta pesa ila namtaftia nani kama sina mtoto.

Niko tayari kumuudumia yeye na mtoto na tutapanga malezi ya uyo mtoto kwa kadri ya makubaliano yetu. Kipato changu sio kikubwa sana ila kinatosheleza mahitaji ya msingi na kufanya maendeleo.

Kwetu tumezaliwa wa tatu, wanaume wawili na msichana mmoja na ndugu zangu wote wamebaatika uzao wa mapacha. Natamani sana namimi nishike wangu

Kwasasa nina miradi niliyo wekeza na nahitaji kuwa na warithi (watoto) maana maisha haya hatujui wakati gani unadondoka.

Kimuonekano mimi ni mrefu, maji ya kunde na kitaaluma mimi ni IT. Aina ya mdada ambaye ningependa kuzaa nae awe tu ni mature, mwenye malengo, msikivu na anayependa kujishughulisha. Asizidi miaka 30

Kama upo tayari please nitumie message kupitia telegram kwa kubonyeza link apo chini or njoo inbox apa apa jf.



Nina mengi ya kuandika kwa hali ninayopitia ila naomba niishie apa kwa leo.
View attachment 2233943
UkISkiA kukurupuka ndo huku sasa.
 
pole sana Mkuu ila kua makini,zaa na mtu anayejielewa usije baadae ukaja kuomba ushauri maana huyo bidada anaweza kutaka ndoa
Ok mkuu. Ndoa haiwezekani na ndo maana nimesema kuwa tayar nipo kwenye ndoa ila haja yangu kubwa ni mtoto na kwa mtu anayejitambua sio issue maana nikukubaliana kila kitu kuhusu uyo mtoto hata kabla hajazaliwa .
 
Kuhusu mkeo, kuwa mvumilivu, ikiwezekana awe anaenda hata kwenye maombezi; kuhusu mtu wa kuzaa naye, unaweza kuanzisha uhusiano wa mbali na singo maza, ukapachika mbegu zako huku maisha yakisogea.
 
Usikate tamaa, sikushauri kutika nje ya ndoa utakaribisha matatizo kwenye ndoa yako. Mimi nilikuwa nq tatizo kama la mke wako nimekaa miaka saba kwenye ndoa nikipata mtoto. Kwa sasa nina watoto wawili wa kiume,

Muombe Mungu yeye ndiye mtoa watoto. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Omba toba hata kwa ajili ya damu yako iliyomwagika kwa njia ya utoaji mimba.
Usikate tamaa hao watoto unaowatafuta ni wapita njia kwenye ndoa yenu siku ya mwisho utabaki wewe na mkeo. Jali mahusiano yako na mkeo. Kumbuka hata wewe ulikuwa mtoto kwa baba yako na sasa haupo umewaacha wazazi wako na sasa wako peke yao.
Zinaa kwenye ndoa ni mbaya usijaribu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Asante kwa ushauri. Hongera pia kwa kupata mtoto baada ya miaka saba . Kama hutojali pia naomba unishauri ulitumia dawa gani na ilikuaje ulikua hupati mtoto mwanzo ukapata mwaka wa saba? Najua pia kuna kujifunza kupitia experiences za watu wengine
 
Mkuu usikate tamaa mbona wengi wanapitia changamoto kama zako lakini Mungu huwakumbuka.

Mimi baada ya kuoa nilikaa miezi 8 hivi hola japo kila mwezi wife ana bleed na tunatiana mwanzo mwisho, ikabidi niende hapo rabinisia hospital nikapewa dawa za kuimalisha sperm lakini wapi ikagoma, nikahama hospital nikaenda kairuki Kwa doctor mmoja maarufu kama Piere akamuandikia dawa ( nakumbuka ilikuwa kama lectrozole kama sijakosea) wife vidonge 5 nikalipia 10K, huwezi amani wife alimeza na mwezi huo huo akanasa.
Mbaya zaidi tukaona tusitumie majira Bali tutumie kalenda kutokana na changamoto tumeopitia yaani mtoto Ile kafika miezi 6 akanasa nyingine, hapa hata hamu Sina tena ya kutaka watoto.
Kilanga chote cha watoto kimeisha
 
Wewe sio mtu wa wanawake sana hapo juu ukasema uliwapa mimba wasichana wawili, we injinia wewe

Wengine hatujawahi hata kusingiziwa nje
Mkuu naona adapt tu na utubu sana maisha haya mafupi ila kama huwezi oa wa pili na usiseme huruhusiwi ok
Hao wawili ilikua vipindi viwili tofauti na miaka tofauti . Vitu hutokea, watu hubadilika na kujifunza. Naamini wengi wetu tumekuwa na mahusiano uko nyuma ila haimaanishi kuwa tulikuwa watu wa wanawake wengi
 
MUNGU akajibu haja ya moyo wako ila kabla y akutoka nje jaribuni miti shamba na kwenda sehemu mbali mbali kwa specialists, hawa watoto wanaoitwa wa nje sometimes wanaweza kuja kukupa stress tu, sina nia wala maana mbaya kusema watoto wa nje.
Asante
 
Mkuu uko mkoa gan? Kuna familia huku nilipo nao walikuwa na tatizo kama lako lakin Hadi mda huu wanalea mimba. Walitumia miti Shamba na mambo yakawa safi,

Miti Shamba zinasaidia
 
Miaka miwili bado midogo sana kwa ndoa yenu na wala usiwaze kuzaa nje kwa sasa.
Mwenyezi Mungu yupo na wenye subira.

Kama mmeshafanya vipimo na pia mmetumia dawa basi nakushauri mueleze mkeo pia asiwe na mawazo sana ya kuwa na mtoto kwa muda wote na wewe pia wazo hilo ondoa kichwani mwako nyie jipeeni haki ya ndoa yenu kama inavyotakiwa na huku mkiwa na amani kabisa kwenye mioyo yenu.

Hakika haitaweza kupita mwaka bila kuona majibu.

Kwenye haya mambo ya uzazi mkiweka panic huwa inakuwa tofauti sana matokeo mnayoyawaza, kama mmeshahangaikia inatosha tulieni kwa mwaka mzima huku mkijua ratiba ya mzunguko wa mkeo ukoje.


Panic mode kama uliyonayo wewe ni mbaya sana usifanye jambo kwa muhemko tulia miaka 31 bado si mingi sana kwa baadhi ya watu tunaowafahamu wamepitia ndoa zao miaka 12-16 ndio wanakuja kupata watoto.

Na mara nyingi watu wanaochelewa kupata watoto huwa Mungu anawapa baraka unakuta uzao mmoja au miwili ni mapacha hivyo unajikuta unawatoto wengi katika kipindi ambacho haukutarajia.

Usizalishe nje kwa sasa mpe moyo na mfarije na mtoe shaka mkeo na mkabidhini Mungu kilio chenu.
Asante kwa ushauri
 
That's the prob. Ilibidi atingishe kwanza kabla ya ndoa, je yaliyomo yamo.!

Probably hana msongo kwa sababu hajabahatika mtoto, ila ana msongo sababu yupo ndani ya 'ndoa' halafu bado bila bila.
Nimeandika kwa ufupi tu ila kiukweli kuna mambo mengi sana yananifanya niwe na aya mawazo. Sijawai pata nafasi ya ku share na mtu yeyote ndo maana nikaleta humu nione . Huwa sipendi sana kueleza mambo ya familia yangu kwa watu na nikaona at least jamii forum naweza anza napo
 
Yo negro dont give up early. Kama shida ni hormonal.imbalance, most times inaeza kua treated just kupitia lifestyle changes. Hasahasa mlo. Ushauri wa bure, angalia weight ya mwrnza wako, then aanze kufanya diet ambayo haitamuumiza. Kuna jamaa anaitwa Boaz Mkumbo, check him out hua ana hyo maelekezo mpaka vitabu. Akiifuata fresh im telling u in six months unaeza kuta mmepata ujauzito.
Usikate tamaa. Hujui yeye dem wako anateseka kias gan, ukijaribu kuzaa nje ndo utakua unamuumiza zaidi
Asabte kwa ushauri ila kama hutojali naomba mawasiliano ya uyo boaz
 
Back
Top Bottom