Ushauri please!

Ushauri please!

minagirl

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
269
Reaction score
35
Kuna rafiki yangu ana mume ambae sio mtu wa kawaida. Naposema sio mtu wa kawaida na maanisha binaadamu wa kawaida hawezi kua na mapungufu mengi ya kimaumbile ila huyu shemeji yangu ni too much,

roho mbaya yeye, wivu uliopindukia yeye, matusi yeye tena anamtukana mke wake mbele za watu, pombe yeye, kuhusu wanawake wa nje ndo usiseme, anatembea na ma baamed, makahaba, kwaufupi skert haikatizi mbele yake na kwa fununu zilizopo ni kwamba hao makahaba anawasodomaiz,

hamhudumii mkewe eti kwa sababu mkewe anakazi basi ale asile yeye hajali.

Rafiki yangu amekonda sana na kwa ufupi hawezi tena kumvumilia kwani anahofia kupata ukimwi, wote ni waislam hivyo kunauwezekano wa kuachana. Cha ajabu mwanaume ameapa kua hawez kumuacha mke wake na kujirekebisha hataki. Nimsaidieje rafiki yangu? Maana ananitegemea sana mm katika suala la ushauri na mm nishindwa ndio maana naomba ushauri.
 
Mke aitishe baraza, talaka inaweza kutolewa baraza likiamua kua hao watu hawawezi tena kua pamoja tokana na matatizo mbali mbali. Reasons for divorce exist, ni pamoja na mwanaume kutom-hudumia mwanamke, mwanaume kua na lifestyle hatarishi kwa mwanamke, mwanaume kushawishi mke wake kushiriki anal sex etc. So yeye aitishe tu baraza ya familia na mashekh, watampa advices tosha na anaweza kuomba talaka toka kwa wakuu wa baraza.
 
MWALI, wameshakaa vikao si chini ya mara tatu na mwanaume anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini baada ya mwezi mmoja anasahau na kuanza upya, sasa iv hataki hata kikao. Kiufupi rafiki yangu yupo njia panda, alitaka kwenda kwa viongozi wa dini akaambiwa lazima awe na ushahidi sasa ushahidi utaupata wapi na ilhali hayo mambo watu wanafanya wawili?
 
MDHT we ndo msemaji wa familia?
 
Last edited by a moderator:
huyo mke hajaamua na manyanyaso kayazoeaSiku akiamua ataipata talaka
 
MWALI, wameshakaa vikao si chini ya mara tatu na mwanaume anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini baada ya mwezi mmoja anasahau na kuanza upya, sasa iv hataki hata kikao. Kiufupi rafiki yangu yupo njia panda, alitaka kwenda kwa viongozi wa dini akaambiwa lazima awe na ushahidi sasa ushahidi utaupata wapi na ilhali hayo mambo watu wanafanya wawili?
Kuna mengine hayahitaji ushahidi. Kama hampi hela za matumizi, ni makosa pia, na hahitaji ushahidi. Mwanaume ndie anatakiwa kuleta ushahidi kua anatoa hela ya matumizi. Pia kama alimshawishi vya kabaaang havihitaji ushahidi, ni kufikisha tu taarifa.
Na huyo dada alijuaje vya mabaamedi? hao hao walio mletea hiyo habari waende wakaseme Barazani walicho mwambia.
 
Lawama hizo...........mambo yanageukaga hapo baadae.Familia yake haipo?
 
MWALI, wameshakaa vikao si chini ya mara tatu na mwanaume anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini baada ya mwezi mmoja anasahau na kuanza upya, sasa iv hataki hata kikao. Kiufupi rafiki yangu yupo njia panda, alitaka kwenda kwa viongozi wa dini akaambiwa lazima awe na ushahidi sasa ushahidi utaupata wapi na ilhali hayo mambo watu wanafanya wawili?
ushahidi upi zaidi unaotakiwa wakati tayari umeshaeleza mabaya mengi ya huyo shem wako? Umesema mmekaa vikao zaidi ya vitatu, na mwanaume anaomba msamaha, sasa si mtumie hizo minutes za kikao au wajumbe waliohudhuria vikao hivyo?

Nafikiri huyo rafiki yako hajanyanyasika kiasi cha kuamua kuchukua hatua kali ....
au laaa inawezekana huyo rafiki yako ni nataka sitaki!!! Kwa hali ya kawaida, huwezi kumvumilia mtu wa namna hii.
 
Mkuu BADILI TABIA, Ameshamuweka vikao ili ampe talaka na alikua akiomba msamaha lakini kwa sasa hataki kusikia kikao.
 
asanteni kwa mawazo yenu, nimepata kitu cha kumshauri, mm ntamwambia aseme na moyo wake, ikiwa amechoka na mambo ya mume wake basi achukue hatua lakini kama anaona yanavumilika basi aendelee kuishi na mume wake kwani uamuzi upo moyoni mwake.
 
Kwa kweli asiifanye ndoa kua ni kama gereza

Mwanamke ikiwa hayo ulioyasema ni ya kweli na kwa vile ni waislamu basi anahaki ya kudai talaka na inaruhusika kupewa talaka kwa vile ni waislamu njia zipo nyingi sana na huenda ikawa ndoa yao imevunjia kitambo ila hawatambui na itakua wanazini

Ila haki ya talaka anayo wala kesi hio haihitaji shahidi na talaka anaipata ingawa inaweza kua na masharti mfano:

Kama atamua kudai talaka kwa maovu hayo aliyoyazungimza kua analewa ni mzinifu n.k basi haki ya kudai talaka anayo ila atahitajika talaka yake ainunue kwa kiasi cha pesa atakachodaiwa na mime wake

Pia km hamtimizii mahitaji km chakula na tendo la ndoa basi inabidi apewe talaka bila ya masharti kwa sababu hizo mbili cha msingi ni kuenda katika mahakama ya kadhi sehemu yoyote tanzania

Ukihitaji kujua zaidi misingi na sabau za talaka ni text sms 0777433260 nitakupa njia sipendi kumuona mwanamke wa kisilamu anateswa ktk ndoa
 
Kuna rafiki yangu ana mume ambae sio mtu wa kawaida. Naposema sio mtu wa kawaida na maanisha binaadamu wa kawaida hawezi kua na mapungufu mengi ya kimaumbile ila huyu shemeji yangu ni too much,

roho mbaya yeye, wivu uliopindukia yeye, matusi yeye tena anamtukana mke wake mbele za watu, pombe yeye, kuhusu wanawake wa nje ndo usiseme, anatembea na ma baamed, makahaba, kwaufupi skert haikatizi mbele yake na kwa fununu zilizopo ni kwamba hao makahaba anawasodomaiz,

hamhudumii mkewe eti kwa sababu mkewe anakazi basi ale asile yeye hajali.

Rafiki yangu amekonda sana na kwa ufupi hawezi tena kumvumilia kwani anahofia kupata ukimwi, wote ni waislam hivyo kunauwezekano wa kuachana. Cha ajabu mwanaume ameapa kua hawez kumuacha mke wake na kujirekebisha hataki. Nimsaidieje rafiki yangu? Maana ananitegemea sana mm katika suala la ushauri na mm nishindwa ndio maana naomba ushauri.
aachane nae mara moja kwasababu asipokuwa makini ukimwi unamsubiri, tena baada ya kuachana nae akapime ajue km anaanza kuishi kwa matumaini au la.
 
Sababu Gani Zinamruhusu Mke Kuomba Talaka?

-
SWALI:
Napenda kujua sababu ngapi zinakubalika katika sheria ya kiislam kwa mwanamke ikiwa atapenda kutengana na ndoa yake au hoja gani ina nguvu zaidi-

JIBU:-
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa-aalihiwa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muuliza swali. Hakika hili ni swali ambalo linajitokeza hasa katika karne iliyopita na hii kwa yale mashambulizi ambayo yanalimbikiziwa Uislamu kuwa haujampatia haki yoyote mwanamke. Jambo la talaka ni mojawapo.
Hakika ni kuwa mke anaweza kuomba talaka kutoka kwa mumewe katika hali zifuatazo:
Ikiwa anapata dhara kutoka kwa mumewe kama kumpiga, kutomtimizia tendo la ndoa kwa sababu yoyote ile, kughibu kwa muda bila kuwa na habari kumhusu na kadhalika. Hii inatokana na msingi wa Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa -aalihi wa sallam) aliyesema: "Haifai kudhuru wala kulipana madhara" (Ahmad, Ibn Maajah, ad-Daraqutwniy).-
Ikiwa mume hana istiqaamah katika Dini kama vile kuacha Swalah na kufanya maasi mengine mengi na makubwa.-
Ikiwa mume hamtimizii mkewe haja zake za msingi kama kumtizama kwa chakula, malazi, matibabu na kadhalika.-
Ikiwa mke hampendi tu mumewe, anaweza kuomba Khul'u (kujivua kwenye ndoa) na katika hali hii mke atabidi amrudishie mumewe mahari yake aliyompatia wakati wa harusi.
Hali hii ilitokea kwa Swahaabiyyah mke wa Thaabit bin Qays bin Shammaas:
عَنْ اِبْن عَبَّاس أَنَّ اِمْرَأَة ثَابِت بْن قَيْس بْن شَمَّاس أَتَتْ النَّبِيّ - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - فَقَالَتْ يَا رَسُول اللَّه : مَا أَعِيبُ عَلَيْهِ فِي خُلُق وَلَا دِين وَلَكِنْ أَكْرَهُ الْكُفْرَ فِي الْإِسْلَام فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:-((أَتَرُدِّينَ عَلَيْهِ حَدِيقَت&#1607😉) قَالَتْ : نَعَمْ قَالَ رَسُول اللَّه - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اِقْبَلْ الْحَدِيقَة وَطَلِّقْهَا تَطْلِيقَ&#1577😉) -البخاري والنسائي
Kutoka kwa Ibn 'Abbaas kwamba mke wa Thaabit bin Qays bin Shammaas alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, silalamiki kwa tabia yake wala dini yake lakini nachukiwa kukufuru katika Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Je utamrudishia bustani yake?)) Akajibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema [kumwambia Thaabit]: ((Pokea bustani na muache talaka moja)) -[Al-Bukhaariy na an-Nasaaiy]
Ama mwanamke kuomba talaka bila ya sababu yoyote ajue kwamba haifai-na isitoshe-hatopata kusikia harufu ya Pepo:
عَنْ ثَوْبَان مَوْلَى رَسُول اللَّه – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – عَنْ النَّبِيّ – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – أَنَّهُ قَالَ 🙁(أَيّمَا اِمْرَأَة سَأَلَتْ زَوْجهَا الطَّلَاق فِي غَيْر مَا بَأْس حَرَّمَ اللَّه عَلَيْهَا رَائِحَة الْجَنَّ&#1577😉)- الترمذي و قال حديث حسن
Kutoka kwa Thawbaan Mawlaa wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanamke yeyote anayemuomba mumewe talaka bila ya sababu yoyote, Allaah Amemharimishia harufu ya Pepo)) [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan]
Na Allaah Anajua zaidi
 
asanteni kwa mawazo yenu, nimepata kitu cha kumshauri, mm ntamwambia aseme na moyo wake, ikiwa amechoka na mambo ya mume wake basi achukue hatua lakini kama anaona yanavumilika basi aendelee kuishi na mume wake kwani uamuzi upo moyoni mwake.
hivi unaona hayo uliyotueleza yanavumilika? unataka yakimshinda kabisa umuambie aachane nae wakati huo ni muathirika tayari na ilhali kulikuwa na namna ya kuzuia hayo yasitokee? the hard way the only, mwambie asiogope kuanza maisha kivyake kwani wangapi wanaachana wanaanza maisha yao na wanafanikiwa sana tu?ningemshauri tu aachane nae na ajikite ktk kuwatiza wanae km hiyo ndoa yao ilizaa matunda hayo.
 
Ndio ktk uislamu hata m/mke anatoa talaka, talaka inaitwa 'KHUL' sharti zake ni kuilia hiyo talaka IKIWA MKE AMEMCHOKA MME, lakini ikigundulika mme ndio kasababisha (hagegedi, hatunzi watoto, hapeleki mahitaji, anapiga sana, mzinifu nk) m/mke ATAONDOKA BURE. Kama ni kweli uliyohadithia, mwambie huyo mke aende tu kwa shekhe au mahakama ya kadhi akachukue (sio akaombe) talaka yake, kwani anahaki zote za msingi kuipata hiyo talaka bure. Ktk uislamu ndoa SI ndoano, mme anaweza kuacha na mke pia anayo hiyo haki hata kama hana sababu hata moja, akiwa hana sababu ya msingi ni lazima alipie mahari yaliyotolewa, then inashauriwa mme asamehe hayo mahari.
 
Mwambie rafiki yako atakuja kufa bure mapema, better to get away with temporary wounds rather than to live with permanent hurts''
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom