Ushauri please:housegal wangu ananitisha!!!

Hawachelewi kuondoka na nyeti hao,kaa chonjo utajikuta mweupe alfajiri kesha chukua hazina yako.
 
pole mno, kuna jirani yangu hapa ilimlazimu amrudishe binti siku ya nne tangu amchukue.huyo binti alikuwa anasusa kula na anajifungia chumbani tu kuanzia siku ya pili tangu afike hapo.nyumba hiyo huwa wanatoka wote asubuhi na kurudi jioni isipokuwa week end tu so binti alikuwa anakaa peke yake mpaka wanaporudi. baada ya kugundua hayo huyo mama aliamua kumuuliza na ndipo binti aliposema bibi yake huwa anakuja lakini anashindwa kuingia ndani so bibi akamwambia aache kazi ili arudi nyumbani akaendelee kufanya kazi anazofundishwa na bibi yake. Huyo bint ana miaka 16 na ni mwenyeji wa Gairo,, na huyo mama anaishi Moro mjini
 
Ipo siku utashika ujauzito halafu mashetani yatamwambia amlete kichanga sadaka. mtoe unless na wewe una mashetan yako.
 
Kesho atakuambia mashetani yanataka atembee na mumeo, la sivyo yanakufanyia.....
 
House girl muhimu jamani anasaidia pia ulinzi wa nyumba mchana wakati watu wapo makazini. maana huku uswahilini kwetu vibaka kibao
 
Huyo ni wa kumrudisha... Kuna siku mashetani yake yatamtaka mumeo
 

dawa kuondoa mashetani how kwa Jina la YESU.basi njia nyingine uwongo tu
 
Amesema ni kwa usalama wa nyumba coz ana safiri safiri. ushauri wangu, huyo dada atakusumbua, mrudishe kwao, mlete ndg yako au ndg wa mume wako waje wakuangalizie nyumba wkt unatafuta dada mwingine ingawa ndugu nao ni pasua kichwa lol!
pole lakini kame wewe
si mjamzito mtoto wa kazi wa nini jamani! umrudishe tu kwao atakusumbua
sana huyo
 
usihangaike na mtu ambae haeleweki. Maisha yako ni ya thamani sana na huwezi kuyakabidhi kwa mtu kama huyo. likizo ikiisha utamwacha nyumbani na ndio atakuwa anawatayarishia chakula. Huoni ni sawa na kumkabidhi chizi maisha yako?.
acha kuyatania maisha yako. Huenda kashajaribu kukuloga kashindwa ndio maana anafanya vitibwi. Kama unadhamini maisha yako, tafuta mtu mwingine anayefaa na kueleweka.
 
Anamtamani mumeo huyo,kama unabisha hebu mkabidhi mumeo hilo suala,wiki moja tu kwisha habari!

Baba mwenye nyumba huenda kaonja sasa likizo yako imeweka giza, rudi kazini plz
 
wanawake nyie hata aje YESU hamtabadilika, mwanamke mwenzio ana matatizo badala ya kutafuta jinsi ya kumsaidia mnalalama mrudishe kwao, kosa lake huyo dada ni lipi kusema ukweli? angeficha ndo ingekuwa vizuri? mtu anakulilia mpaka anapiga magoti! who are you? are Angel or GOD? are you perfect for everything? wanawake pendaneni na kusaidiana wenyewe kwanza ndo msaidiwe, kwani huyo mdada alipenda kuwa hivyo mnavyomnyanyapaa? ungekuwa ni wewe uko hivyo halafu unanyanyapaliwa hivyo ungejisikiaje? kwenye hii dunia maisha ni mzunguko huwezi jua ya kesho kwako, wewe dada msaidie huyo mwanamke kama wewe, mpe nafasi na atakuwa mfanyakazi mzuri kuliko usivyotarajia, MPENDE BINADAMU MWENZIO KAMA UNAVYOJIPENDA, wapo wengi walikuwa wazima na mnawajua lakini leo hii hawatamaniki.
 
Mungu tunakuomba utengeneze njia maana hapa duniani masaibu nin mengi mno! yaani mashetani yanamkataza kuongea nawewe na kumfanya akuchukie? how is doest come? najiuliza sipati picha yaani ni balaa tupu kwakweli ila muombe Mungu sana atakusaidia pia kama nawewe una imani kama yateu basi unaweza kumpeka kanisani au msikitini akaombewa then masheteni yatamtoka tu.
 
huyo sio, kama sio mwanga bac mchawi ludisha akawange mbele huko atakualibia maisha
 
hapo hata ushauri hauhitajiki, ni kufanya maamuzi magumu tu.

may be ita kucost but for the sake of ya family mrudishe tu jamani, usingoje majanga.
 
Hongera kwa kuhimili vishindo vya maisha,
Maisha ni vita na wakati ukipita umepita;

Jipe amani ya moyo wako kwa kuwa umeshashinda
mambo mengi; usikubali kumkaribisha tena ibilisi.

 
Dada mrudishe kwao huwenda ni mchawi pia angalia asije akaanza kukulimisha usiku.
 
sasa ananambia anashida sana nikimridisha kwao jumla maisha yake ni mabaya na ametafuta kazi ili ajisaidie.analia ukimuona hadi huruma itakuingia kweli ananiweka njia panda

Hiyo unayoita angalia isije siku kukuponza bi mkubwa...hayo maji unayotaka kuoga si kina chako

Utakuja kupoteza uhai wako kwa sababu ya ulimbukeni na umeshindwa kuchukua maamuzi magumu...

Kama kweli wewe unadhani ni mtu wa huruma sana, basi leo hii ungelikuwa umetoa msaada wowote wa hali na mali kwa wagonjwa mahospitalini na yatima wasio na wazazi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…