Ushauri: Online class masomo ya sayansi katika kipindi cha corona wapewe walimu wazoefu

Tunkamanin

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
951
865
Ushauri: Online class masomo ya sayansi katika kipindi cha corona wapewe walimu wazoefu;- Muddy physics, Mgote, Mbuga, Mkandawire na makumaku

Kutokana na mchango mkubwa wa hawa manguli wa lecture za mitaani hasa maeneo ya mchikichini. Kwa wale waliosoma miaka hiyo, nadhani wanakumbuka mchango wa hawa Watanzania wenzetu katika kusambaza elimu na kurahisisha maisha ya elimu ya sayansi kwa vijana wa Kitanzania.

Katika kipindi hiki cha corona ambapo mikusanyiko isiyo ya lazima imezuiwa, natoa pendekezo kwa wizara ya elimu kuwapa mkataba hawa watu wazoefu na vigogo vya mafunzo ya elimu ya sekondari nchini kupitia e-class. waruke hewani kila siku, watoto wetu wapate kufaidika na hazina hizi ambazo zinapotea bure mtaani.

My take: Napenda kutoa heshima zangu kwa hawa watu: Mbuga, Mkandawile, Muddy, Osama na Hidden Agenda kwa kazi kubwa walioifanya mpaka nimefikia katika ngazi hii elimu inayonipa ugali wa kila siku mimi na familia yangu. Mwenyezi Mungu wabariki sana. wanafuaika wa moja kwa moja au hata ambao wameambulia nyaraka zao unaweza kuungana na uzi huu kwa kutoa ushauri wako.
 
Masomo hayo ya online yatawafikia wangapi? Kuna sehemu hata neno online ni msamiati
mbali kuwa online lakini hata kwenye TV yanaweza kuwekewa vipindi kama ilivyo sasa. Kama kuna watu 100 basi hata 40 wanaweza kufaidika. Lisilowezekana lote, haliachwi lote. waswahili walisema
 
Kwa jinsi hao jamaa wanavyopewa sifa humu toka enzi na enzi wangekuwa watu wa kujiongeza na kutumia fursa kikamilifu bila shaka wangekuwa mbali sana.

Wangeongea na wadau wa ving'amuzi wakaanzisha channel yao ya kulipia kwa mwezi kama ilivyo wasafi TV.

Naona wakenya tayari wana EDU TV!
 
Online ni changamoto nzito mno kwa nchi yetu. Hatukujipanga.

Tupo kwenye vita ya covid 19 kila silaha inayofaa itatumika.

Uchoyo na ukosefu wa maarifa unawasumbua walimu wengi nchini kwetu.

Miaka ya sasa ni rahisi kujirecord ukifundisha na kutuma kwa youtube au telegram au whatsapp groups.

Wito wangu ni kwamba walimu wengi wajitokeze kuelimisha kwa njia ya mtandao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jinsi hao jamaa wanavyopewa sifa humu toka enzi na enzi wangekuwa watu wa kujiongeza na kutumia fursa kikamilifu bila shaka wangekuwa mbali sana.

Wangeongea na wadau wa ving'amuzi wakaanzisha channel yao ya kulipia kwa mwezi kama ilivyo wasafi TV.

Naona wakenya tayari wana EDU TV!
wazo zuri nadhani watu walio karibu nao hata wadau wa sekta ya habari wanaweza kuwaendea na kufanya nao mazungumzo. Brazil wameweza sana hiyo biashara. kuna youtube channel nyingi sana zinazoelimisha, yaani wao shule kwanza. Sisi nyingi ni za umbea na udaku.
 
wazo zuri nadhani watu walio karibu nao hata wadau wa sekta ya habari wanaweza kuwaendea na kufanya nao mazungumzo. Brazil wameweza sana hiyo biashara. kuna youtube channel nyingi sana zinazoelimisha, yaani wao shule kwanza. Sisi nyingi ni za umbea na udaku.
Kufungua chanel tanzania bila kulipia tcra ni kesi, sasa unataka linanganisha na hao brazil?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni moja ya nyuzi zangu, jicho langu la moyoni liliona mbali sana. Leo elimu ya Physics ya Muddy amezikwa nayo, sijui pale Azam walifanikiwa kupata record ngapi za huyu mwamba wa elimu naomba kama wanazo watuwekee youtube tumkumbuke mwalimu wetu. Allah amlaze mahali pema peponi Muddy physics...Aamin
 
Back
Top Bottom