Ushauri: Nitumie Njia Gani, Kumfunza Mtoto.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: Nitumie Njia Gani, Kumfunza Mtoto..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by S. S. Phares, May 7, 2009.

 1. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wana Jamii,

  Naombeni mawazo yenu kwenye suala hili zito linalokoroga akili yangu..

  Ni namna gani nimfundishe mtoto awe na busara kwenye matumizi ya rasimali alizonazo (nilizompatia) hasa fedha?

  Binafsi ilinichukua muda sana (into 30's) kuona umuhimu wa kutumia mali vizuri mpaka pale niliposota, kupata shida sana ndipo nilipojifunza.

  Ningependa kusikia kwa wazazi wengine out there, wao wanatumia mbinu gani..nisingependa watoto wangu wapitie nilikopita kwa sababu najiona nilikuwa na bahati kukomboka.


  Walisema: It Takes a Village to raise a child...


  Natanguliza ahsante.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Itategemea umri wa mtoto.
  Kwa mtoto mdogo sana labda wa KG - usimzoeshe pesa.Shuleni atayarishiwe chakula ( snack na kinywaji) kwa maana hata hajajua pesa na thamani yake vizuri.Hata kama una pesa nyingi vipi usipende kumpa picha hiyo maana atajenga imani kuwa pesa ipo tu tena ya kumwaga.
  Umri unapoongezeka, anza kumpa pocket money kwa kiwango fixed kufuatana na uwezo wako, umri wa mtoto na mahitaji yake halisi lakini kisiwe kiwango kikubwa sana.Pia endelea kumpa mawaidha kuhusu rasilimali hiyo na nyingine, na umuhimu wa kupenda shule ili baadae aweze naye kuja kuweza kujitafutia kipato chake.Pia mfundishe concept ya savings.Kwamba pocket money pia anaweza kusave na kujiwekea akiba.Uwe pia umemfungulia akiba yake na akifanya savings umsaidie kuweka kwenye account.Hata kama ataweza ku save elfu 1au 2 itampa fundisho na kumhamasisha.Hii ni kwa uchache sana.
   
 3. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mfundishe faida za kuweka akiba. Ikiwezekana mtafutie kitabu kinaitwa "Crazy Investment" sikumbuki author wake ila kinaelezea faida za kuweka akiba kidogo kidogo kulingana na umri halafu kinampa mazoezi ya kucalculate compound interest itakayopatikana kulingana na muda pesa zake zitakavyokaa benk. Akisome chote. Wakati mwingine mnaweza kusoma wote na kueleweshana sehemu zile muhimu
   
 4. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  carrot and stick....yap..hii itasaidia sana maana hata mie ilinisaidia at those early up to foolish ages...unapewa pesa uki-overspend within ur budget time una-suffer the consequences then atakuwa na akili ya ku-utilize fully the FAMILY RESOURCES if at oll means money
   
 5. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lingine la msingi ni kumu imarisha mtoto katika maadili. na wewe m(wa)zazi kuwa wa mfano. Ajue faida ya kuishi, kuwa na familia nzuri, kuheshimu ndoa, upendo katika ndoa, upendo wa wazazi kwa watoto, faida ya kuwekeza mapema, kujituma kufanya kazi na mambo mengine mengi ambayo yatamfanya mtoto ajitambue na pale atakapopambana na watoto wengine wasio na mwelekeo wowote wa maisha asiyumbe bali aweze kusimama na kuelezea kwa kinagaubaga kwa nini anaamini kile anacho kifanya ni cha faida kwake na sio kwamba amelost? Mfano baadhi ya watoto hujikuta wakidelay kufanya ngono si kwa sababu ya kujua umuhimu wa kudelay bali kwa sababu tu labda ya aibu ya kutongoza, labda mara ya kwanza alipotongoza alitukanwa na kukataliwa na hivyo kujenga uoga, aliambiwa kuwa ni dhambi ingawa anatamani kufanya lakini anaogopa, wazazi ni wakali hivyo anaogopa kukamatwa n.k. watoto wanamna ni rahisi kuangukia kwenye mtego pale wanapokutana na watoto wenzao wanaotukuza ngono kama ndio ujana hasa tofauti na mtoto mwenye taarifa sahihi za kwa nini asubiri kuanza ngono.
   
 6. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mtoto anahitaji kushirikiswa kwa vitendo, na wazazi au walezi tunatakiwa kuwa mfano

  ashirikishwe katika matumizi kwa kuanzia na matumizi yake binafsi, umueleimishe umuhimu wa kuwa na priority katika matumizi, na pia umuhimu wa kuwa na akiba, unaweza ukawafungulia akaunti na kuwashirikisha katika utunzaji wa akaunti hizo, na pia unaweza kuwapima uwezo wao kwa kuwapa majukumu madogomadogo ya kutunza mali ya familia, kwa mfano unaweza kwa zamu ukawapa wajibu wa kukamata pesa ya miscelenous na kuangalia kila mmoja atatoa ripoti gani mwisho wa mwezi,

  pia ni muhimu mno kuwapa nafasi kushiriki katika kuandaa bajeti na matumizi ya familia, bajeti za mwezi za kawaida, mambo ya maendeleo, nk mara nyingi unaweza kuwapa wao challenge ya nini wadhani kinafaa kifanyike kwa kiasi cha pesa kilichopo hii itwasaidia kuongeza uwezo wao wa kufikiria na kuona umuhimu wa kupanga matumizi!!
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yebo yebo, kama upo seriously please ''Copy and Paste'' huo ushauri wa WOS na Bibi kizee........I would have suggested the same!

  Na kama utafanikiwa kuwafanya waelewe na kufuata hayo.....basi mkuu hata ukizimika anytime unakuwa huna wasiwasi huko tusiko kujua!

  Thanks 100 times WOS & Bibi kizee...you said it all!
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Labda pia kama ni muumini usisahau kumfundisha kutoa zaka na sadaka. Hiyo itamfanya awe mwaminifu sana na muangalifu.
   
 9. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama ni mdogo introduce concept ya "saving" kwa kumnunulia piggy bank
   
Loading...