Ushauri: Mtoto wangu wa nje ya ndoa kapewa baba mwingine

DOGofGOD

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
1,344
1,195
Amani kwenu wadau wote wa MMU

Nimemua kuleta uzi huu kwenu ili muweze kunisaidia ushauri utakao nisaidia kupata ufumbuzi wa tatizo langu nilionao.Naamini ni utamaduni wetu tuliouzoea apa MMU kupeana ushauri wenye manufaa.kwahiyo nilikuwa naomba kutumia nafasi hii kuwasihi tuendeleze utamaduni huu ili tuweze kutimiza lengo lililokusudiwa katika forum hii.

Awali ya yote ningependa kutanguliza shukrani zangu kwako wewe ulieamua kupoteza mda wako wa thamani sana ambao ungeweza kuutumia katika maswala mengine ya ujenzi wa taifa hili.Lakini umeamua upoteze mda wako ili uweze kuchangia katika uzi huu.

Kwahiyo naimani hutakubali mda wako wa thamani upotee bure na kwa kulitambua hilo naimani ushauri wako utakua bora na wenye manufaa sana kwangu unaolingana na thamani ya mda ulioupoteza.Pia natanguliza shukrani zangu kwako wewe ambae umetumia mda wako kusoma uzi huu lakini kwasababu za msingi sana zilizo nje na ndani ya uwezo wako umeamua husichangie chochote katika uzi huu.

Uamuzi wako huo ulioufanya ni wa hekima sana na unaonesha ni jinsi gani unavyojitambua.Kwasababu umeona badala ya kuchangia utumbo na vitu visivyoeleweka na kujaza seva umeamua uwapishe wadau wengine ambao unadhani wanaweza kua na michango mizuri zaidi.Nakupongeza kwa uamuzi wako wa busara na kama wadu wote wangekua na fikra pevu kama zako naamini MMU ingeendelea kuwa mahali bora sana na hata taifa hili lingepiga hatua sasa kimaendeleo.

Baada ya maelezo hayo ya utangulizi ningeomba sasa niingie kwenye mada.

Ni hivi wadau: Kuna binti mmojai(nitampa jina la X) nilikua katika mahusiano nae kwa mda flani lakini kwa bahati mbaya tuliachana miaka kama mitatu hivi iliyopita.Tuliachana kwasababu ambazo nisingependa kuzielezea humu ila kwa kifupi ni kwamba tuligombana.Lakini baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na maisha yake na hatukua na mawasiliano ya aina yeyote ile.Ila nilikua napata taarifa tu za juujuu kutoka kwa rafiki zake wa karibu.

Lakini kwasababu tulikua tumeshaachana nilikua nazipuuzia tu.Niliwai kupata taarifa kua huyu binti anaisha na mwanaume mwingine na ni mjamzito.Lakini kama kawaida nilizipuuzia.Ni kaja kusikia kua ameshajifungua na ana mtoto wa kiume.Lakini kwasababu nilikua tayari nimeshasikia kua anaishi na mwanaume mwingine na mimi na yeye tulishaachana kwahiyo sikuona kama taarifa kama hizo zinanihusu mimi kwahiyo niliendelea kuzipuuzia.Kwahiyo miaka ikasonga.

Miezi kama miwili hivi iliyopita nilikutana na rafiki yake wa karibu sana ambae kwangu mimi ni kama shemeji yangu na mimi na yeye uwa tunataniana sana.Nilipokutana nae akanambia kua X ananisalimia sana na alikua anatafuta namba yangu ili anisalimie.

Mwishoni mwa maongezi yetu na huyu shemeji yangu akaniuliza "umeshawai kumuona mtoto wa X?" mimi nikamjibua kua "sijawai kumuona".Shemeji yangu huyu akanambia "Yule mtoto ni wako ukimuona hukatai kwasababu sura yake ni wewe copyright".Huyu shemeji yangu ni mtu wa masihara sana lakini maneno yake yalinisitua kidogo kwahiyo ikanibidi nimuachie namba yangu.

Baada ya mwezi mmoja nikapokea simu kutoka kwa X.Tukasalimiana na kupiga stori mbili tatu.Na katika maongezi yetu nikamuuliza kuhusu hali ya mototo wake akanijibu ni mzima na anaendelea vizuri.Na nikamuuliza ana umri gani akanijibu kua kwasasa ana miaka mitatu.

Na pia nilimuuliza kuhusu mwanume aliekua anaishi nae akanijbu kua wameshatengana na kwasasa kila mmoja anaishi kivyake na mtoto yuko kwa bibi yake.Na pia kwa kipidi kile alinieleza kua yuko Dodoma ila atakaporudi dar atanitafuta ili tuonane tusalimiane.Mimi nikamwambia sawa.Baada ya apo tukaendelea kuwasiliana tu kwenye simu.

Wiki moja iliyopita alinitumia sms kua yuko njiani anarudi Dar.Ila tokea arudi sikupata bahati ya kuonana nae kutokana na ubize flani hivi.Ila jana nikabahatika kuonana nae tena baada ya kupoteana kwa miaka mitatu.Kusema kweli alifurahi kuniona na hata mimi nilifurahi kumuona coz alipendeza sana.Na tuliweza kuongea mambo mengi sana.

Ila mwishoni nilijaribu kumdadisi mambo ya mtoto na nilimuomba anaioneshe picha ya mtoto.Alikua na picha kadhaa kwenye simu yake.Kusema kweli nilivyoziona zile picha za yule mtoto amefanana na mimi copyright hajaacha kitu.Kwasasa ninae mototo mwingine wa kiume ana mwaka1.Nikiziangalia picha zao ni mtu na kaka yake kabisa.

Kusema kweli sikua na sababu ya kumficha na nikamueleza ukweli palepale kua huyu ni motto wangu.Mwanzoni alikataa ila baada ya kumbana sana mwishowe ilibidi anieleze tu ukweli kua tulipoachana mimi na yeye tayari alikua na ujauzito wangu wa karibia mwezi mmoja.Ila alishindwa kuniambia kwasababu tuligombana na mimi nilikua sieleweki kwa akipindi kile.Na ndomaana hakunambia chochote kuhusu ujauzito wa mtoto.

Mimi nilimueleza kua pamoja na yote hayo yaliyotokea lakini mimi namuhitaji mwanangu kwasababu ile ni damu yangu.Yeye alinijibu kua kumpata mtoto itakua ngumu sana kwasababu kwasasa mtoto anababa yake mwingine na yeye ndie alie mlea tokea alipokua mdogo.Na kama nikijaribu kumdai motto kwasasa nitamsababishia matatizo makubwa sana kwa ndugu zake na kwa baba wa mtoto alie mlea.

Kwasababu baba wa mtoto bado anajua kua yule ni mwanae na itakua ngumu sana kwasasa kumwanbia kua yule sio mwanae.Kwahiyo akaniomba tuyaache mambo kama yalivyo kwasababu italeta mgogoro mkubwa sana.Na nikajaribu kumuomba angalau tukapime ili tuweze kua na uhakika zaidi kama mtoto ni wangu au vipi lakini amekataa katakata.Anachodai anaomba tuyaache mambo kama yalivyo.

Kusema kweli mtoto namuhitaji sana.Na siwezi kukubali kuona damu yangu anapewa mtu mwingine.Kulingana na maelezo yake na picha alizonionesha ninauhakika kua yule mtoto ni wangu japo bado sijaenda kupima lakini imani niliyokua nayo ni kubwa sana.Lakini mpaka sasa sijajua nianzie wapi kwasababu mazingira ni magumu mno.Kumbuka mpaka sasa mtoto anatimiza umri wa miaka mitatu sijawai kumnunulia hata nepi.

Mama wa mtoto anadai kua alipata matatizo makubwa sana katika ujauzito wa yule mtoto mpaka kujifungua.Na mimi sikua na msaada wa aina yeyote ni ndugu zake ndo walioteseka nae.Kwahiyo nikiibuka sasahivi kudai mtoto ndugu zake hawatanielewa mimi na yeye pia hataeleweka.

Na baba wa mtoto aliemlea pia ni kikwazo.Kusema kweli sababu zake ni za msingi sana lakini mtoto ni wangu na namtaka na hata yeye anakubali kua mtoto ni wangu ila mazingira yalimbana na mpaka sasa bado yanambana.Kwahiyo kuepusha shari ananiomba tuyaache mambo kama yalivyo.

Naombeni ushauri wenu wadau nianzie wapi kumdai huyu mtoto? Nitumie njia gani ili niweze kua na uhakika wa asilimia100 kua huyu mtoto ni wangu? Nimewai kusikia kua kuna kipimo cha NDA lakini nasikia gharama yake ni kubwa sana ni kweli?

Naombeni mnieleweshe sheria inasemaje na haki yangu kama baba(endapo itathibitika) katika mazingira kama haya ikoje? Katika mazingira kama haya kuna uwezekano wa kumpata mwanangu?..Nini nifanye endapo mama wa mtoto atakataa kwenda kupima na akaamua mtoto ampe baba mwingine? Kumbukeni huyu ni mtoto ni wa nje ya ndoa sheria inaniruhusu kumdai.?

Naombeni ushauri wenu wadau niko njia panda.Nategemea msaada mkubwa sana kutoka kwenu.Naombeni kuwasilisha
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,685
2,000
Umepunguziwa mzigo. Tafuta mwingine huko ulikozoea - mchepukoni.
 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,271
2,000
"........kumuona coz alipendeza sana.Na ........"

Matunzoooo, we wataka rudi tena? huwezi mpenda mtoto na mama ukamchukia...ka wamtaka mtoto na mama umpende pia

nashauri huyo X awe mke mdogo

 

fundichupi

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
385
250
Duuuh..!? Hebu pata picha na wako wa mwaka mmoja si wako na mwenyewe anakuja dai anamchukua. How would you react au feel!? Wanasema ukilea mimba at tyms mtt aweza toka anaelements zako hata kama ww si biological father. Nachoshauri mwache X akae kwa aman, yy ndio ataamua akupe mtt wako lini au kama akae nae mazima.

Jifunze kuwa mwanamke hanuniwi ndugu hvo nxt tym ukiznguana nao hawa viumbe kp urself close had akupush yy kuwa u hv no place in heart or mind
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,817
2,000
Niliposoma huo utangulizi wako tu nikachoka ila nikajikaza nkamaliza story asee dam nzito fanya ufanyavo utafte dam yako
 

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,148
2,000
Hehehe wewe chezea kwingine sio mabinti qa dodoma. Mkuu mimi nilifanya ambush. Sasa hapa inategemea uko fiti kiasi gani sababu anaweza amua kukupelekesha kesi ukashindwa na kufilisika. Swala inabidi uprove negligence ya mama basi.
Halafu kipimo ni DNA sio NDA.
 

Chujio

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
804
225
Unataka kipi kati ya haya:
-mtoto?
-utambulike kama baba wa mtoto?
-uharibu mahusiano aliyonayo sasa?
 

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
6,128
2,000
Angekwambia ana mimba yako ungekataa, ila umeinyeshwa picha umekubali na kumtaka mtoto, ukisha pewa utamfanyaje? Ebu kama unampenda kweli anzaa na matumizi kumlea jina la baba mwengine sio neno, muonyeshe mzazi mwenzio kama unajali na still unaheshimu maamuzi yake...
 

Capt Nemo

JF-Expert Member
Feb 26, 2015
1,448
1,225
Ndugu yangu nimekusoma vizuri na I can understand your case.

Kwanza nakushauri kuwa achana na watu wanaokurupuka humu ndani badala ya kuongea vitu contructive wao wanakimbilia kulaumu na kuponda tu.Kuna huyu anayedai ulitelekeza...kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuonyesha mahali popote ulipokosea katika mchakato mzima

Maoni yangu ni kama ifuatavyoHuyu binti mwenye mwanao hana busara na ana ukatili fulani ndani yake. Yeye anajua kuwa mtoto ni wako..hata kama mligombana alikuwa anawajibika kukupa taarifa za ujauzito alokuwa nao na baada ya kujifungua ilibidi akufahamishe..kama ungekana mimba ingekuwa another case.
Kitendo chake cha kumpa mtoto baba mwingine nacho ni ukatili anaomfanyia huyo baba...na yupo tayari kuendelea kumficha wakati at the end itafahamika tu...come rain or sunshine.

Huyo mwanamke alikuwa anakucheat kwa sababu mpaka mwanamme asingiziwe mtoto ina maana alikuwa kwenye game muda ambao mimba ilitungwa...sisi wanaume hatuhitaji degree kujua kuwa mpaka mtoto awe wako lazima uwe ulibed na mwanamke at least miez tisa kabla ya mtoto kuzaliwa..so X ni kicheche na alikuwa anawachanganya..WANAOMTETEA NA KUTOTAKA AMANI YAKE IPOTEE WALIANGALIE NA HILI

Ndugu yangu damu ni nzito hivyo vyovyote mnavyofanya mtoto lazima amjue babake halisi..haimaanishi kama lazima umchukue au umuachie mama lakini you have to be recognized as the boy's biological father.J
ambo la kwanza mfahamishe mkeo halali hali halisi..kama uelewa wangu upo sahihi inaonyesha ulimuoa baada ya mtoto kuwa amezaliwa so hukucheat..tofauti na hapo una case ya kujibu lakini sio issue sana

Baada ya hapo mweleze X kuwa you are determined kutambulika kama baba wa mtoto. Akiendelea kugoma mwambie utamface baba-msingiziwa uongee naye direct. kama unasema mwanao wa ndoa ni copyright na huyo wa nje ya ndoa basi your case is simple kabla ya kufika kwenye DNA.Akigoma kweli tafuta watu wenye busara mumtafute baba-msingiziwa muongee naye kwa busara..najua once mwanamme akirealize mtoto si wake hawezi kumng'ang'ania..sanasana kama ndo wale akina flani atadai fidia ya matunzo ya mtoto aliyoincur..pay the guy and take your kid.

Kama hiyo itashindikana basi utakuwa huna option zaidi ya kufungua case mahakamani ya kudai kutambuliwa na kumchukua mtot baada ya kupima DNA ambayo itaprove mtoto ni wako

CASE YA KUMCHUKUA:
Ndugu yangu kama mambo yataenda mpaka mahakamani watakuwa wamekupa silaha ya kumchukua mtoto kilaiini!Kazi yako itakuwa kumprovia hakimu kuwa mama hafai kule kwa sababu
1. She is a cheat - alikuwa natembea na wanaume wawili (pengine na zaidi) KWA WAKATI MMOJA
2. She is a liar - amemdanganya mtu na kumpa mtoto si wake na akakuficha wewe ukweli kuhusu mwanao
3. She doesnt care about other people's feelings - feelings zako kwa kutopewa mwanao, feelings za baba-msingiziwa kwa kumficha ukweli, feelings za mtoto kwa kutomwonyesha his real father

Kama mambo yatashindikana maana mahakama zetu ndo vile..wewe tulia tulii usifanye chochote ila weka kumbukumbu za mchakato mzima..I guarantee you miaka isiyozidi 12 mbele mwanao atakuja bila kushikwa mkono...chezea umbea wa watu na uzito wa damu weye!!!!!
 

Luggy

JF-Expert Member
Aug 6, 2012
3,003
2,000
solve hii issue mapema,usikubaliane naye kwamba muacha tu mambo yalivyo,lkn angalia katika kutafuta ufumbuzi huu usimuumize,poa nakushauri shirikisha watu wazima wenye hekima zao
 
  • Thanks
Reactions: BAK

theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Hiyo case ngumu na nirahisi.
Ngumu kivipi huyo x wako unataka kumweka majaribuni coz ulivyomwacha yeye alimbambika jamaa yake ili huyo unayedai mwanao asiteseke kutokana na hasira zenu.
Rahisi kivipi kama busara zitatumika pande zote aliye lea na anayedai hiyo damu yake.
Ushauri kaa na x wako ujadili mkubaliane coz kumnyang'anya mtu mtoto ambaye alijua ni mwanaye sio kitu simple.
Au potezea tuu na ujue hasira ni hasira siku zote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom