Ushauri: Nisaidieni namna Bora ya kutibu tatizo linalomuandama mama yangu

Asante mkuu ntajitahidi kufanya hvyo na kuhakikishia ntaleta mrejesho hali yake ikitengamaa
 
Pole sana mkuu, kwa dalili za mama anaonesha dalili za ugonjwa wa akili.
Ana dalili kama hizi
•persecutory delusion- kuwa na imani kwamba kuna watu wanataka kumdhuru bila ya kuwa na ushahidi au maelezo ya kueleweka kwa namna gani wanataka kumdhuru.
•suicidal ideation-mawazo ya kutaka kujiua.
•disorganized speech- kuongea vitu havieleweki ambavyo haviendani na muktadha.
•kukosa usingizi.
Mkuu kwa hayo machache ni dalili za ugonjwa wa akili ambapo yawezekana akawa na either magonjwa ya psychosis(HIV associated/induced psychosis) au magonjwa ya mood disorders.
Nakushauri ufike hospital yoyote hasa ile ya rufaa kwenye kitengo cha magonjwa ya akili utapata msaada mkuu.
 
Kiukweli anaishi na dada yangu na dada ananiambia wanampa ushirikiano mzuri tu pamoja na hali waliyokua nayo lakini wanajitahidi kumuelewa na kuishi nae hivyo hvyo
Mimi ndo Niko mbali nae napanga niandae likizo nikawaone na nijumuike nao Kwa pamoja

Na pia uwa naongea nae mama na ananiambia anataka amuone mjukuu wake mana tangu mke wangu amejifungua sijapata nafasi ya kumpeleka mtoto akamuone.....

Na mimi nikiwa naongea nae kwenye simu huwezi amini unaweza ukahisi Hana tatizo kabisa ila zikipita siku kadhaa tu utasikia Kuna jambo huko ameshalifanya mpaka linakua linawaogopesha watu anaokaa nao
 
Hivyo vidonge alitakiwa apewe kwa nguvu au kwa Siri hata kwenye juisi ilimuradi muhakikishe anatumia hizo dawa huwa zinawapa usingizi wanapata muda wa kupumzika, mpaka anapona.
Daah tutajitahidi ndugu yangu ila ni changamoto akibaini Kuna vitu mmemchanganyia anakua na hofu anahisi mmepanga njama za kumuua,na hapo hata umueleweshe Kwa upole namna Gani hakuelewi kabisa
 
Hataki siku hizi kwenda mwanzon alikua anaenda mwenyewe ila tulipoanza kuona hii hali uwa tunaenda tunamfatia dawa tunamletea nyumban
Kumchukulia dawa inatakiwa iwe kwa dharura tu!

Mpelekeni hospitali mkawaeleze wataalam wa afya jinsi anavyobehave, ni tatizo dogo watalishughulikia.

Nyie kama watu wake wa karibu mna jukumu kubwa sana la kumfariji na kumfanya ajihisi ni mwenye thamani sana!!

Mwisho, nina mashaka kama hata hizo dawa anazitumia Kwa usahihi ikiwa tu kwenda clinic hataki..
 
Nadhani pia upweke ulichangia hasa kama mlikuacha akiishi peke yake kwa muda mrefu.
Jaribuni kumuweka karibu na kumuweka karibu na Mungu kutokana na imani yake.
Pia kama inawezekana hana shida zaidi ya hiyo achangamane na wamama wenzie kama ni Kanisani au Msikitini ili asiwe mpweke kama ni maombi au shughuli nyingine za kidini hasa mtaani.
Pia kama hapo anapoishi Kuna majirani wa umri wake jaribu kuwaweka karibu nae ili ajichanganye na watu itampunguzia mawazo ila tu angalia wale wenye busara na pia uwaeleze tatizo lake ila usiwaeleze ugonjwa wake haitapendeza ili wajuie wanadeal na mtu wa aina gani pia waweze kumsaidia ajisikie amani.
Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Mungu amfanyie Mama yetu wepesi ila muwe mnajitahidi hata kumpigia simu kila baada ya masaa kadhaa.Vilevile kama mtampeleka Mirembe inaweza kuwa bora zaidi na msisahau kumpelela kwenye maombi!
Mkuu tunajitahidi sana Kila tuwezalo kuhakikisha mama afya yake inatengamaa
Na juzi tu hapa nilimuomba dada anitumie picha yake what's up nimuone alivyo
Aisee niliamsha mzozo wa hatari akadai nataka kupanga njama yaaaan mkuu sijui nikwambie nn mungu amponye mama ni mateso Kwa kweli
 
Kisa cha mamdogo kuogopa ni kwamba alimuona mamdogo ni kama adui yake japo alikua akimchukua na kumpeleka kwenye maombi mara Kwa mara lakini Kuna siku alitaka kujinyonga akiwa ndani kitu ambacho kilimfanya mamdogo kuogopa kukaa nae
 
Asante mkuu nashukuru Kwa ushauri wako
 
Pole hizo ni effect za matumizi ya mda mrefu wa madawa. Waoneeni madaktari wanao msaada wa kupunguza madhara ya madaw hayo. Changamoto itakuwa kwa mgonjwa kukubali kutumia Ili apone, ukaribu na ufariji ni muhimu zaidi, pili mwambie sister asichoke asiyajali maneno yake still Hakuna thamani kubwa duniani kama kumtunza mama. Msiogope msikate tamaa pambaneni hadi sent ya mwisho hadi mda wa mwisho.Ili Nguvu ya maombi itende Kazi ni lazima anaombewa airuhusu iingie ndani mwake ndipo ufanya kazi.
Dili ni chanzo cha tatizo yaani side effects za hizo dawa kwanza atakaa SAwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…