Ushauri ninunuwe laptop yenye uwezo gani?

Raymond karega

New Member
Aug 30, 2022
3
3
Habari wakuu.
Msaada kwa anayeelewa, ninunue PC gani, na yenye uwezo gani mzuri kwa budget yangu ya laki7? Mimi si mtaamu wa aina za PC na uwezo wake nisaidieni nisije kuingizwa chaka.
natafuta laptop mpya, yenye uwezo wa kurun animation Kama blender, na 3D nyingne, pia inisaidie kwenye kuhariri program zangu za habari kwani nina professional ya mass communication. Nina laki 7 tu.

Ninaomba kuwasilisha.
 
Huwezi kupata laptop mpya kwa laki 7 yenye uwezo huo. Hata used ngumu sababu blender inataka machine ya maana yenye gpu nzuri.

Unaweza angalau tafuta machine used gen ya 8 kupanda na Gpu za Nvidia Mx series.
 
Bora umemwambia ukweli tu 😳🏄🏄
 
Huwezi kupata laptop mpya kwa laki 7 yenye uwezo huo. Hata used ngumu sababu blender inataka machine ya maana yenye gpu nzuri.

Unaweza angalau tafuta machine used gen ya 8 kupanda na Gpu za Nvidia Mx series.
Ahsante kwa ushauri,

Ahsante kwaio ni laptop ipi naweza pata kwa hii laki7 mpya I mean uwezo na tools zote
 
Ahsante kwa ushauri,

Ahsante kwaio ni laptop ipi naweza pata kwa hii laki7 mpya I mean uwezo na tools zote
In theory mkuu pentium/celeron mpya, Amd mendocino ama Alderlake N ama hata i3 unapata kwa hio bei.

Sema wauzaji wetu wengi wapo slow ku update mizigo yao, ngumu kuzikuta mtaani.

Laptop kama ideapad 1i unaipata around $250 yenye i3 1215u ambayo si mbaya kwa matumizi yako.

Kwa Hapa Tanzania ushauri wangu nunua used, tafuta hio gen ya 8 na Nvidia gpu ndogo kama Mx150, Mx250 etc itakusogezea siku.
 
Kuna laptop ya dell latitude 5289

Specs
Series Dell Latitude 5289 2-in-1 12.5" Touch Laptop PC
Screen Size12.5 Inches
Color Black
Hard Disk Size 256 GB
CPU ModelCore i7
Ram Memory Installed Size16 GB
Operating System Windows 10 Pro
Card Description Integrated
Graphics Coprocessor Integrated Graphic
 
Kwa bajeti yako ya laki 7, unaweza kupata laptop nzuri ambayo inaweza kukidhi mahitaji yako ya kufanya kazi za ubunifu kama vile kurun animation kwa kutumia Blender na kuhariri programu za habari kama vile Adobe Premiere Pro. Hapa kuna chaguo kadhaa ambazo unaweza kuzingatia:

1. Dell G5 15 SE: Laptop hii ina kioo cha inch 15.6 na inafanya kazi kwa kutumia processor ya AMD Ryzen 5 4600H, RAM ya 8GB, na uhifadhi wa SSD wa 512GB. Ina kadi ya grafiki ya AMD Radeon RX 5600M, ambayo inaweza kukidhi mahitaji yako ya kufanya kazi za ubunifu. Inagharimu takriban laki 7.

2. Acer Nitro 5: Laptop hii ina kioo cha inch 15.6 na inafanya kazi kwa kutumia processor ya Intel Core i5-10300H, RAM ya 8GB, na uhifadhi wa SSD wa 512GB. Ina kadi ya grafiki ya NVIDIA GeForce GTX 1650, ambayo pia inaweza kukidhi mahitaji yako ya kufanya kazi za ubunifu. Inagharimu takriban laki 6.5.

3. ASUS TUF Gaming A15: Laptop hii ina kioo cha inch 15.6 na inafanya kazi kwa kutumia processor ya AMD Ryzen 5 4600H, RAM ya 8GB, na uhifadhi wa SSD wa 512GB. Ina kadi ya grafiki ya NVIDIA GeForce GTX 1650, ambayo inaweza kukidhi mahitaji yako ya kufanya kazi za ubunifu. Inagharimu takriban laki 7.

Kumbuka kuwa, kwa kufanya kazi za ubunifu, ni vyema kuwa na laptop yenye kioo kikubwa, kadi ya grafiki bora, na RAM ya kutosha. Hivyo, unaweza kuzingatia mahitaji yako maalum ya kazi na kulinganisha sifa za kila laptop kabla ya kufanya uamuzi.
 
Back
Top Bottom