USHAURI: Nina million 20 nifanye biashara gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Nina million 20 nifanye biashara gani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by The only, Jun 8, 2012.

 1. The only

  The only JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 1,423
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  yenye uhakika na itanipa daily cashflow kwan nikiichezea narisk maisha ya mke na watoto 2,ni mkopo wa mshara kukatwa nusu
   
 2. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  mkuu, hongera kwa kubahatika, pili naomba ungejieleza upo wapi? una shughuli gani? una uzoefu gani? ulishawahi kufanya biashara yoyote? binafsi ulishawahi kuwa na mawazo gani ya biashara? unapenda nini? umeoa/ kuolewa? Upo tayari kufanya biashara ya ubia??? ....... amini kuwa BIASHARA YA KUFANYA INATEGEMEA MTU NA MTU NA MAZINGIRA ALIYONAYO, SI KILA ANACHOKIFANYA MWINGINE NA WEWE UTAWEZA AMA SI KILA ANACHOSHINDWA MWINGINE NA WEWE KITAKUSHINDA.

  Swali la kizushi: unaweza kutueleza umekopa wapi hizo milioni 20 kwa mkopo wa mshahara na sisi tukakope??? Unarejesha kwa muda gani?? kwa riba gani???
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwenye Red hapo umenifurahisha sana,

  Ok Mimi nitakuwa tofauti kidogo na wewe kuhusu mleta Maada, Kuna watu wengi sana wanasema ukitaka kuficha dokoment zako mhimu kama pesa basi weka kwenye kurasa za kitabu, utarudi utazikuta,

  Hii thread ni kama ya 20 hivi kuzingumzia mtu kuwa na mtaji na kuhitaji mchango wa mawazo, mkuu hizo thread ziko nyingi sana na michango inafanana so ni vizuri ukasoma hiyo michango kabla ya kupost thred, na hii thread ya haitapata michango mingi kwa sababu ni marudio ya thread nyingi sana kama hizi,

  Mwisho, mkuu unawezaje kukopa kabla hujajua unaenda kufanyia nini? wewe ulikopa ili ukafanyie nini? make ni mzaha wa hali ya juu kwamba uliomba mkopo ila hukujua unaenda kufanyia nini,

  TUJARIBU KUWA SIRIAZI WAKUU, MAKE HILI JUKWAA LINATEMBELEWA NA WAKENYA NA WAGANDA NA WANATUONA TUSIVYO SIRIAZI KABISA NA HAPA NDO WANAPO ANZA KUPANGA MIKAKATI YA KUTUPIGA BAO KWENYE EAC


   
 4. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nakupongeza kwa kupata mkopo; bali kama ambavyo KOMANDOO alivyosema zimeshapita thread nyingi za namna hii na zipo hapa hapa kwenye jukwaa la biashara, nakumbuka kuna moja ya mtaji wa milioni 10 alianzisha MBU kama sikosei, ilikuwa na michango mingi sana. Mimi nina wazo lakini sina mtaji na sina sifa ya kupata mkopo kama wewe, hivyo naomba mchango wako wa Tsh 4970/= tu, kwani natafuta watu 1000 kutoka kwenye jamii watakaonichangia kiasi hicho kila mmoja ili niaze mradi wangu. Unaweza kutembelea thread yangu hapa ndani ya jukwaa hili - https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/273049-niwezeshe-kutimiza-ndoto-yangu.html
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nunua gari mkuu
   
 6. galagaja mtoto

  galagaja mtoto Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  plz fuatilia masomo ya ujasiriamali yanayopatikana humu jamvini kutoka kwa galagaja mtoto, kupitia category hii ya business na hata kule kwenye nafasi za kazi.
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....Dah! Nasisimka sana ninapojikuta mchana kama huu ninapiga miayo, jiko na mama vimenuna na hakijaeleweka halafu kuna mtu ana shilingi Milioni 20 lakini hajui azifanyie nini ili kuzizalisha. Tell me comrade, Why ddnt you ask Us before taking the Loan? Dd You take the Loans with no plans at all on what to do with the money?? Then why dd you take it at all if you dd not have any plans at all and you depended on JF to give you One??.....YAAAWN!!:yawn::yawn:
   
 8. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  teh tehe tehe teh........Nimecheka sana..
   
 9. lolyz

  lolyz JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Make decisions and act on them. Make mistakes, fall and try again. Even if you fall a thousand times, at least you won't have to wonder what could have been. At least you will know in your heart that you gave your dreams your best shot
   
 10. chash

  chash JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ok ok.

  Hauna biashara nyingine inayo endelea vizuri uii expand? Kama jibu ni No. Wewe upo kazini, kwa hiyo huwezi kuwepo kwenye biashara muda mwingi. Therefore avoid, duka haina yeyote, muuzaji atakufilisi. taxi, bajaj dereva atajifaidi mwenyewe. Mkeo au mmeo kuiendesha biashara hiyo ya duka au taxi, bajaji dala dala nk. Ok, lakini uwe tayari kumsamehe kama atakuwa hana experience ya biashra. Ndugu je? 90 % chances you will fail.

  Pia zingatia asilimia 95 biashara mpya u feli ndani ya miaka 5. Inahitaji passion, ufanye kitu unacho kipenda saaaana moyoni wako. Hivyo unakuwa mwepesi kuvumilia matatizo yeyote hata kufanya kazi mda mrefu bila kuchoka. Mvumilivu ula mbivu. Bado hamna? Kiwanja. You will not regret. Baadaye unaweza kukiuza at a profit au ukajenga. So far bado tu?

  Usikubali kuweka partnership na mtu atafaidi yeye. Usitume mtu kwamba nenda kanunue mbao au ndizi tuje tuuze, chances are it will not work. Trust ipo chini sana siku hizi.

  My final advice.

  Kilimo: Tafuta shamba yenye maji ufanye kilimo cha umwagiliaji. Kilimo cha kutegemea mvua ni very risky. Ekari mbili za kilimo cha umwagiliaji ni sehemu kubwa mno. Panda kabeji, nyanya, kitunguu, carrots nk Tafuta hybrid seeds upate mavuno makubwa. Fuga kuku wa kisasa wa kienyeji ambao gharama za kufuga zipo chini kuliko za grade. Zinataga mayai kila siku au baada ya wiki nane zitakuwa na zaidi ya kilo moja na tayari kuuzwa nyama. Nenda pole pole usiwe mwepesi wa kuamua. Think before you leap. Slow and sure wins the race.

  Hata hivyo yote yakishindikana na hela iishe usipate presha ndivyo maisha yalivyo, sahau yaliopita na ujipange upya.

  Oh na usisahau, kama ni mtu wa imani fungu la Mungu peleka kanisani au msikitini. Kumbuka pia wazazi kiasi, waombe waibariki kazi ya mikono yako.
   
 11. chash

  chash JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Oh nimesah. Kuongeza elimu pia ni wazo nzuri. Kwenye kazi zako unaweza kuongeza kozi zipi ili uongezee cheo au mshahara?
   
 12. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  nimesoma mwanzo hadi threat ilipo, ninachokiona na kumuomba Mungu ni "Mwenyezi Mungu atusaidie sana Watz katika kuwa wabunifu, wajasiri/watu wa kuthubutu? watu wenye alternative thinking katika areas zote za maisha! siasa, uchumi, mpira, michezo,ujasiliamali nk.
  kabla ya threat hii nimepitia moja ambayo mwanzishaji anaulizia jinsi ya kuazisha biashara/uchuuzi wa m-pesa na watu wamemwaga mawazo yao.
  Kimsingi ukipia hii na hivo zingine utaona jinsi Watz tu watu wakutofikiri sana/kwa kina bali twapenda vitu vyepesivyepesi na upeo wetu ni narrow sana.
  Mawazo yanayotolewa hapa zaidi ni jinsi gani ya kufanya uchuuzi na si jinsi ya kufanya udhalishaji wa kuongeza dhamani na hata kuweza kutoka nje ya mipaka ya nchi kama wenzetu wakenya wanavyofanya. Tz ama watz tulivyo hakuna hata benki moja ya tz ipo Burundi, rwanda ama kenya lakini wao waja nakutukuta bado tunaulizana tufanye nini?
  May God help us!!!
   
 13. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli inasikitisha pale ambapo waTZ wengi bado tunaendelea kujiuliza tufanye nini na huku wageni wanakuja katika ardhi yetu na kuziona fursa na wanachukua hatua. Mara nyingi huwa sipati jibu sahihi kwa mtu anapouliza nini cha kufanya?, inamaana katika mazingira yanayomzunguka hakuna mahitaji? mbona TZ bado mahitaji ni mengi katika jamii?, kuanzia asubuhi mpaka jioni unakutana na shida mbalimbali; hizo ndio fursa za biashara, unapoenda kupanda daladala na unakuta watu wanagombanaia daladala hilo ni tatizo na unaweza kuligeuza kuwa fursa ya biashara kwako, unachotakiwa ni kufikiri jinsi ya kuondoa tatizo hilo na mengine mengi tu katika mazingira tunayoishi.
   
 14. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nenda suma JKT pale Mwenge upate trecta jipya farm tract 60-70 inauzwa shillingi milioni 18,000,000/= unalipa nusu yani 9,000,000/= unapewa trecta kiasi kilichobaki unapewa miaka 2 [miwili] kulipa. Utabakiwa na milioni 11.

  Then unakwenda kukodi heka 100 kwa kila heka ni shilingi 15000/= hadi 20,000/= jumla 2,000,000/= uwezo wa trecta kulima kwa siku ni ekari 20 utatumia siku 5 kumaliza shamba lako baada ya hapo uta anza kulima mashamba ya watu kwa gharama ya sh 30000/= kwa heka kwa muda wa siku 30 hadi 45 mfululizo gharama za kulima shamba zote zinarudishwa na trecta lenyewe heka 100 unaweza kupata gunia 700 za mahindi hadi 900
   
 15. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama uko seriuos, mimi na marafiki zangu wachaga watano tuna biashara amabyo inalipa vizuri, ila huwa tunakutana pale Hongera Bar (DSM) kila siku ya Ijumaa kuanzia saa tisa mchan kupanga mikakati mipya, hivyo karibu sana Ijumaa hii ukifika ulizia Kaunta 'meza ya kama tulivyo' watakuonyesha. Iam serious.
   
 16. J

  JBAM Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ila ahakikishe analima mahali ambapo pana uhakika wa maji ya kumwagilia. karne hii sio ya kulima kwa kuangalia angani (kusubiri mvua) atafilisika na kutafuta presha bure. pia afuate ushauri wa kitaalam juu ya namna ya kufanya hicho kilimo chake ili kuongeza tija kwa eneo badala ya kuwa na eneo kuuuubwa na mapato kidogo huku gharama za uzalishaji zikiwa kubwa pia na hivyo kupunguza profit. God advice bwana whilshere
   
 17. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu KIMBITO NYAMA, nawapa pongezi kwa ushirika wenu; naomba nifikishie ujumbe wangu kwenye meza yenu ya "KAMA TULIVYO" hapo hongera bar, ujumbe wenyewe - https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/273049-niwezeshe-kutimiza-ndoto-yangu-2.html; kumbuka mjumbe hauwawi.....!!!, nashukuru kwa kufikisha ujumbe wangu...!!!
   
 18. babalao

  babalao Forum Spammer

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakushauri uanzishe biashara mchanganyiko ya M PESA, Kuuza luku, vocha za mitandao yote, TRA, DAWASA. Nunua mashine ya Max Malipo kwa deposit ya shs. 500,000 tu itakuwezesha kufanya biashara zote hizo. Cha muhimu tafuta sehemmu ambayo watu wengi wanapita ndipo ufungue biashara yako hiyo.
   
 19. The only

  The only JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 1,423
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Aisee watu makini hivi bado mnaishi hata nyakati hizi umenichana ukweli bila chenga sikutanii i will work on it
   
 20. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....Kabila lina ulazima? maana umetaja hapo marafiki zako watano 'Wachaga'! kama jamaa ni Msukuma ama Msambaa asije??:thinking:
   
Loading...