Ushauri: Nimezaa mtoto wa nje mmoja, napata wakati mgumu kuoa mwanamke mwingine atakayempenda mtoto wangu

Pole mkuu, muoe unaempenda kwa dhati na yeye anaekupenda, mama wa kambo ni jina tu.

Mm Nina mtoto naishi nae wa Mume wangu, tunapendana balaa, ile natoka honeymoon nakutana na watoto watatu wa kwanza wa mume wangu wawili wa shemeji zangu walizaaga wenyewe bado wanasoma

Walizan wamenikomesha kumbe wameniongezea baraka kwenye nyumba, watoto wanapendana balaa nikazaa watoto wangu wawili basi nipo na team ya watoto wa5 wanapendana SNA, niliwakuta wana miaka 6, now wote wapo darasa LA 7 wakirudi likizo sasa wananiletea zawadi balaa, wanajimek pocket money zao wanamkumbuka mama yao, yaan hawakumbuki mama zao kabisaaa

Nikinunua zawad ni za watoto wote, nikikosa nanunua big bom5 yaan wananipenda sna.

Ni roho ya MTU tu mkuu, na hofu ya Mungu ikiwepo AMAN INATAWALA


Asante kwa ushauri mzuri, ubarikiwe, wanawake wenye moyo kama wako ndo changamoto, kipindi cha uchumba hawana tatizo, mziki akiingia ndani mambo yanabadilika
 
Mama yake kaolewa mkuu, ndomana najaribu kusolve vitu viwili kwa mpigo.moja ndoa hili lazima, pili mbali na ndoa lazima kuwe na amani ndani ya nyumba, changamoto ni wakumpata uyo atakekuja kusimamia amani ya nyumba ili maisha yaende vizuri

Ah majamaa walishamchukua bby mama....dah sasa hapo tafuta single mother uoe
 
Tatizo ni ww mwenyewe...kwa nn usimuachie mama yake amlee tu hadi awe mkubwa ila ukita kuhudumia utamuhudumia akiwa huko huko kwa mama yake na kwako atakuja kusalimia tu.
 
Kama hamna tatizo muache aishi na mama ake utahuhumia kama kawa... Likizo atakuja kukutembelea
Maana mama wa kambo hawa mmmmmmmmmmmh
 
mama wa kambo shida sana huyo mwana akisemeshwa kidogo kwa ukali babae lazima aje juu...
 
Kifupi nakatoto kamoja nilikapata enzi za kujalibu jalibu, mamake yuko vizuri kiuchumi anaishi nae kwakua bado kadogo, ila kunamda ntamchukua niishi nae

Sasa imefika muda wa kuoa serious ila bado napata wakati mgumu nioe mwanamke wa aina gani atakaempenda mtoto wangu

kunakipindi nawaza nioe mwanamke mwenye mtoto ili kuwe na NEUTRALIZATION, kifupi naogopa sana maswahibu wa mama za kambo hasa kwa mtoto wa kike

wakuu naomba mnipe ushauri nifanyaje ili maisha ya ndoa yaende vizuri hapo badae, kwasababu sitavumilia kabisa nione mke anamtesa mtoto namimi nimuangalie tu

Ndio maana naombeni ushauri
Majibu unayo mwache akae na mama yake
 
Km bibi yake mzima na haoni tabu kumhudumia ,basi mpeleke huko...ni wanaume wachache hujali maslahi ya watoto wao kabla ya yakwao,wengi wanaume ni selfish huwa wanajiolea tu..so big up
 
muache mtoto akae kwa mama yake, ndio anakuwa huru zaidi kwani amemzoea, sasa wewe anakuona mara moja kwa mwaka halafu tena ukamuweke na mtu hamjui si kumtafutia depression mtoto?. Kama mama hajakwambia umchukue muache mtoto.
Ushauri mzuri,Mimi pia nlikua nawaza hivyo mtoto abaki Kwa mamake atakua safe zaidi kuliko kuanza kutafuta mke Kwa
vigezo tu ampende mwanao,hiyo ni utashi wa uyo mwanamke utaempata,anaeza mpenda au asimpende.
 
Back
Top Bottom