Ushauri: Nimezaa mtoto wa nje mmoja, napata wakati mgumu kuoa mwanamke mwingine atakayempenda mtoto wangu

Afande Kirusi

Senior Member
Mar 15, 2018
110
125
Kifupi na katoto kamoja nilikapata enzi za kujaribu jaribu, mamake yuko vizuri kiuchumi anaishi nae kwakuwa bado kadogo, ila kuna muda nitamchukua niishi nae

Sasa imefika muda wa kuoa serious ila bado napata wakati mgumu nioe mwanamke wa aina gani atakayempenda mtoto wangu

Kuna kipindi nawaza nioe mwanamke mwenye mtoto ili kuwe na NEUTRALIZATION, kifupi naogopa sana maswahibu wa mama za kambo hasa kwa mtoto wa kike

Wakuu naomba mnipe ushauri nifanyaje ili maisha ya ndoa yaende vizuri hapo badae, kwasababu sitavumilia kabisa nione mke anamtesa mtoto na mimi nimuangalie tu

Ndio maana naombeni ushauri
 
Tafuta demu mwingine 'ujaribu' tena, waongeze angalau uwe na watoto wa 4 wa nje, hapo utakuwa haunashida tena ya kuoa uzae....unaoa asiyezaa unabaki kula bata tu.
 
Mkuu kama alikubebea mimba amekuzalia muoe tu dada wa watu,labda kama kuna sababu nyingine ila kama vigezo kati ya tano anakidhi Vitatu oa tu mtoto atapata malezi bora zaidi kuliko hilo wazo lako
 
Pole mkuu, muoe unaempenda kwa dhati na yeye anaekupenda, mama wa kambo ni jina tu.

Mm Nina mtoto naishi nae wa Mume wangu, tunapendana balaa, ile natoka honeymoon nakutana na watoto watatu wa kwanza wa mume wangu wawili wa shemeji zangu walizaaga wenyewe bado wanasoma

Walizan wamenikomesha kumbe wameniongezea baraka kwenye nyumba, watoto wanapendana balaa nikazaa watoto wangu wawili basi nipo na team ya watoto wa5 wanapendana SNA, niliwakuta wana miaka 6, now wote wapo darasa LA 7 wakirudi likizo sasa wananiletea zawadi balaa, wanajimek pocket money zao wanamkumbuka mama yao, yaan hawakumbuki mama zao kabisaaa

Nikinunua zawad ni za watoto wote, nikikosa nanunua big bom5 yaan wananipenda sna.

Ni roho ya MTU tu mkuu, na hofu ya Mungu ikiwepo AMAN INATAWALA
 
Ushauri ni kwamba acha kuwa na matarajio ya ajabu. Wee ulishakosea so tulizana kama hupati atakae mpenda mtoto wako basi lea mwenyewe au muoe mama yake

Mama yake kaolewa mkuu, ndomana najaribu kusolve vitu viwili kwa mpigo.moja ndoa hili lazima, pili mbali na ndoa lazima kuwe na amani ndani ya nyumba, changamoto ni wakumpata uyo atakekuja kusimamia amani ya nyumba ili maisha yaende vizuri
 
Back
Top Bottom