Ushauri: Nimelogwa au ni upendo?

Makuke

New Member
Jul 19, 2015
3
18
Jamani wana JF,

Naomba mnisaidie hata ushauri tu, sijui nimelogwa au ni upendo tu maana hii experience sijawahi kabisa kuwa nayo tangu nizaliwe.

Mimi ni kijana mwenye miaka 25 nilikua na mpenzi wangu (25 yrs) tuliekuwa tunapendana sana tena sana na tumeishi kwa mwaka mmoja sasa kwa malengo ya kumuoa, japo aliolewa na akakaa kwenye ndoa kwa miaka minne kabla ya kuwa na mimi na akaachika na ameshazaa mtoto mmoja mwenye miaka minne.

Shida imekuja nilipotoka na kuhamia sehemu nyingine kikazi nae akaenda kwao, ghafla mawasiliano yalipungua ikawa ugomvi hauishi na ni kwasababu amebadilika sio kama zamani.

Nimevumilia yote hayo lakini mwisho wa siku akanidhihirishia wazi kuwa anamtu baada ya kumuweka profile picture WhatsApp na kunitamkia kabisa kuwa huyo ndo mpenzi wake wa sasa na ndio aliemnunulia smartphone na nisimsumbue hawezi kurudiana na mimi.

Sikumuacha ila tulikosana kwa wiki moja tu ndo tukkaliana kimya baada ya kumpigia simu usiku simu ikawa busy akaniambia namsumbua anataka kulala na kunikatia simu siku hiyo, najitahidi kuizoea hali lakini nashindwa kabisa.

Mpaka nimemwambia kama alipitiwa akafanya hivyo basi haina shida tuanze upya lakini kasema mwili wake hawezi kuwapa watu wawili na ameshafanya nae mapenzi zaidi ya mara mbili na kasema nifute malengo yote kichwani mwangu na hana mpango wa kuolewa wala kutolewa posa kwa sasa (ilhali nilipanga kwenda kwao kujitambulisha mwezi wa 11).

Nilimzoea sana na sababu ya kuniacha hata haieleweki, wengine anawaambia simjali kifedha, wengine anawaambia mimi sijatulia, mimi ananikumbushia SMS za zamani na ugomvi wa zamani ambao tulishausolve eti ndo umesababisha.

Nifanye nini wanaJF maana hafutiki kichwani kabisa.
 
Pole sana, naomba nikuambie tu hujataka kumuacha

Amini unaweza kuishi baada ya kibuti

Maisha kabla ya kumpata huyo yalikuwaje had umpate akutende uone kama una lana?

Kaza moyo wako act like u don care, ishi maisha yako lakini ukiwa peke yako lia unavyoweza usiyazuie jichanganye na watu

Jipende, muda utakua tabibu mzur kwako

Kubali she is no longer yours maadam hakuna jambo n yeye na huyo alonunua smartphone karma hautamuacha salama
 
The same age dah! Pole kichwa cha chini kisikutese, kama wako atarudi.

Ila pesa nayo tafuta kuna kitu hakijakaa sawa mdogo wangu.
 
Pole sana, naomba nikuambie tu hujataka kumuacha

Amini unaweza kuishi baada ya kibuti

Maisha kabla ya kumpata huyo yalikuwaje had umpate akutende uone kama una lana?

Kaza moyo wako act like u don care, ishi maisha yako lakini ukiwa peke yako lia unavyoweza usiyazuie jichanganye na watu

Jipende, muda utakua tabibu mzur kwako

Kubali she is no longer yours maadam hakuna jambo n yeye na huyo alonunua smartphone karma hautamuacha salama
Umemamaliza. Also asitafute kisasi or kufanya vitu kujarib kumuonyesha ni zaidi yake. Bali atulie aweke focus yake kwenye maisha sasa, kenye kupona moyo.

Huyo ex wake asimuwaze ila ajue tu kama always win at the end. Ukweli utajulikana tu na yatamtokea yakumtokea atakuja kwa machozi.
 
Acha kulilia papuchi si utafute mwingine maisha yaendelee
Nadhani hujamuelewa jamaa. Hakumpenda kwa sababu ya papuchi, bali ni kqa sababu ya mapenz. Hivyo ni vitu viwili tofauti.

Kama lingekuwa suala la papuchi sidhan kama angeandika huu uzi maana ni suala rahis sana. Lakin hili ni suala la emotinal connection ambayo imevunjwa ghafla. Si rahi ku recover kama unavyodhani.
 
Ushaambiwa ukiachwa achika
Wanaume mnatabia ya kuchukulia kawaida mnapopendwa siyetunayalundika huku tunatafuta plan B tukipata anayetuelewa tunasepa kimyaaaa ndio mnashtuka kama wewe kumekucha mwenzio alikuchoka alikuwa akikuambia ukajidai mbishi ni kweli hakutaki kubali yaishe
 
hamna stori mingi hapo..wewe huna hela kaka sasa smartfone umeshindwa nunua unategemea nini.
ushauri wa bure...ukishaondoka sehemu na ukamuacha mwanamke kaa ukijua wapo wanaogegeda.
 
Honestly hiyo Hali ya kuwafanya wanaume wateseke kwenye mapenzi mm sijakutana nayo na siombei initokee mara zote nimekua nikiumiza wanawake sio kuumizwa japo siku hizi siwaumizi tena nimeshakua ila nilichokuja kugundua kwenye ukuaji wangu wanaume ambao huwa hawajali sana ndio hupendwa sana tofauti na wanaume wanaopenda sana kama mtoa mada, ngoja nikuambie ninavyofikiri huyo mwanamke anakutafsiri nadhani anakuona bwege bwege japo kilichokuponza ni upendo wako kwake mwanaume kupendwa ndio raha sio unakuja kulia Lia umerogwa hapa hamna kitu kama hicho mchawi akili yako wazungu wanasema it costs to be stupid the stupider you are the more it costs, anza kumtharau tena mtharau kweli kweli tafuta totow moja kali kushinda yeye ila kuwa makini usimpende sana be a player hit them as much as you can na akikuzingua kidogo achana nae kanyaga mwingine you are so young (ila kuwa makini na hilo mdogo wangu pesa na maradhi,) ukifanya hayo nina uhakika utaenjoy na utapata mke wa maisha yako achana na
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom