Ushauri: nimeitwa kufanyakaz bila malipo

Wild fauna

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
461
Reaction score
189
Salaam wadau.
Kuna NGO imeniita nikajitolee. Sasa imeniambia wao hawatanipa chochote zaidi ya chakula na malazi,usafiri nitajitegemea. Sasa wadau mnanishauri vipi hapo?
Kwa sasa nipo mjini sina ishu.
 
Unakosea sana unaposema hawatakulipa chochote na hapo hapo unasema watakupa chakula na malazi. Sasa kama hauna ishu, unaona malazi na chakula ni haba? Fanya kazi kijana, upata uzoefu, ujenge CV yako ili kazi za ukweli zifuate. Ni rahisi sana kupata kazi ukiwa kazini kuliko ukiwa nyumbani.

Ukikaa mtaani miaka 3 bila kazi ndio utajua?

Salaam wadau.
Kuna NGO imeniita nikajitolee. Sasa imeniambia wao hawatanipa chochote zaidi ya chakula na malazi,usafiri nitajitegemea. Sasa wadau mnanishauri vipi hapo?
Kwa sasa nipo mjini sina ishu.
 
Sasa itabidi tena utoe pesa zako ili kujilipia nauli kwenda kazini kila siku? Sio itakuwa ni ngumu sana ukizingatia hutakuwa na chanzo cha mapato kingine? Hapo ulipo huna malazi wala chakula?
 
Salaam wadau.
Kuna NGO imeniita nikajitolee. Sasa imeniambia wao hawatanipa chochote zaidi ya chakula na malazi,usafiri nitajitegemea. Sasa wadau mnanishauri vipi hapo?
Kwa sasa nipo mjini sina ishu.


Kamata hii fursa haraka sana, itakusaidia kujenga uzoefu. Hakikisha unachapa kazi mpaka jamaa watambue umuhimu wako. Ningekuwa mimi ndio wewe, hata vyoo ningewasafishia, ukiacha hayo majukumu mengine watakayonipangia. Wakisha admire uwepo wako (kama baada ya mwezi hivi) waambie wakupatie nauli pia ya kwenda hapo kazini kwakuwa huna chanzo kingine cha mapato. Kama kweli unajituma kisawa sawa hata mshahara utalipwa. Mwaka 2006 niliwahi kupewa fursa ya namna hiyo, baada ya kujitolea kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, nililipwa siyo mshahara tu, hadi overtime.
 
Salaam wadau. Kuna NGO imeniita nikajitolee . Sasa imeniambia wao hawatanipa chochote zaidi ya chakula na malazi ,usafiri nitajitegemea. Sasa wadau mnanishauri vipi hapo? Kwa sasa nipo mjini sina ishu
.

...ndugu yangu Wild fauna "KAZI NI KAZI ILI MKONO UENDE KINYWANI"

... Kwavile umeahidiwa cha kuweka kinywani na sehemu ya kujiegesha "NENDA UKACHAPE KAZI"
usafiri ni miguu yako.
 
Mkuu. Kama vipi tafuta baskeli uwe unaenda nayo..ingawa kama wewe ni tozi au yung babylone utaniona nakucharazia
 
Nawashukuru wadau kwa ushauri wenu! DEODAT,KBM nimewasoma sana.
Ngoja nijitutumue nitengeneze cv wadau,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…