Ushauri: Niko kwenye kipindi kigumu sana

Ushauri: Niko kwenye kipindi kigumu sana

Yani dhambi kubwa ni kutoa hiyo mimba.. Unakuwa umeuwa., cha kufanya wajulishe wazazi hali ilivyo na uwe tayari kwa lolote ila mimba usitoe. Utakuja kujutia baadae kwanini uliuwa.
 
Huyu mwanaume punga kweli maana hiwezi acha mtu unaumpenda eti kwa sababu kasoma? Akili hiyo au matope?

Huyo atakuwa kapata mtu mpya huko ajirani, mapenzi mengi ya chuoni huwa hayadum baada ya kumaliza na kupata ajira iwe kwa wanawake na hata kwa wanaume.

Kwa kweli inatia uchungu sana hasa kwa hiyo mimba maana swala la kuzaa kama hujajipanga duu! Ni bora uzae kwa kujipanga sio uzae by chance utateseka sana na mbinguni usiende pia
 
Hilo nalo neno, kuna wakati wanaboa unaamua kulipiza
NB; usilipize ni dhambi kubwa sana.
 
Pole,uamuzi usio hatarishi ni kutubu kwa Mungu wako na kutunza kiumbe na si vinginevyo usiwaogope binadamu hawata kudhuru kwa vyovyote iwavyo
 
Mambo mengi yamtokeayo mtu ameyachagua mwenyewe either kwa kujua au kutokujua...

Hapo wewe lea Mimba na mtoto...mengine yatafuata
 
Pole sana.
Mtoto ni baraka toka kwa Mungu. Kwanza mueleze jamaa kuhusu mimba labda ataweza badili mawazo/kuhudumia mtoto but swala la kuitoa usiliweke akilini hata kdogo
 
Duh! We lea mimba yako. Huenda atajirudi tu mbele ya safari. Now its too late to go back and undo what has happened...
 
naomba niulize swali nje ya point!! kwa nini wanaume wasielimishwe kusema uongo kunaua nafsi za wapenzi wao? au waambiwe wakitaka kuwaachawapenzi wao waanze kupunguza mapenz taratibu na sio kuzimisha mioyo ya wadada gafla?
nirudi kwenye mada; dada usithubutu kutoa mimba waweza kuwa umebeba Obama wa kesho. Lea mimba yako na mrudie Mungu ndie mkuu wa faraja
 
Mueleze Una mimba,kama hataki bora utoe mapema,Kulea peke yako utajutraa
 
Amekuacha kwa sababu hujasoma, ndio ukweli. Sasa muambie sawa, lakini una mimba. Ajue tu lakini usikubali kuolewa nae kwa sababu ya mimba. Baada ya kuzaa hakikisha unasoma hadi phd! Ndio revenge inayomfaa huyo jamaa.

Ni vaisi vesa ujue.....hawowi mwanamke aliyesoma.......huyo jamaa ameapa hawowi kabisa.....
 
Mueleze Una mimba,kama hataki bora utoe mapema,Kulea peke yako utajutraa
y unashiriki kuua? never do that my dear no matter what the situation will be, life will go on
 
Pole sana binti mshukuru Mungu kwa kila jambo amini unaweza na Mungu atakusaidia jitahidi kumshirikisha mzazi wako na jiandae kuwa mama Hongera sana kwani una hofu ya Mungu.
 
Ninashindwa nianzie wapi jaman naona kama labda kuna kitu mie nimemkosea mungu
Nimeongea nae amesema yuko tayari mimba itolewe
Ila nawaza dhambi niliyonayo na ninayotaka kuifanya
Polee Saanaa Kiukwel Inasikitisha Na Sijui KwaNini Anayachukulia Mambo Kirahis Rahisi Hivyo..Me Nakushaul Kma Yote Yameshindikana Kwa Huyo Jamaa, Usitoe Mimba N Kaa Chini Uongee Na Mama Yako Mzaz Muelezee Kila Kitu Usimfiche. Na Katika Swala Hil Japo Nawe Unayo Makosa Ila Si Muda Wa Kulaumiana.
 
ujauzito huo una umri gani?Labda aligundua ndo maana akakata mguu mapema.
Tulia fanya maamuzi ya busara yatakayo ufaa moyo wako kwa sasa na maisha ya baadae.
kama dhambi ushafanya ya uzinzi kwahiyo katika maamuzi yako kuogopa dhambi isiwe kigezo kikubwa.
wanaume wanao.kushauri zaa ulee ndo kutwa wapo humu wana dis kuoa wanawake wenye watoto.(angalia moyo wako)
Kila la heri.na inaonesha wewe bado ni mdogo usikate tamaa ya maisha.
 
Mimi ni binti nilikuwa kwenye uhusiano na mpenzi wangu kwa miaka minne toka yeye akiwa first year chuo flani hivi, mimi kielimu ninamalizia certificate ya lab tech mwaka huu ikiwa yeye amemaliza na ameajiriwa tayari.

Tulikuwa vizuri ki ukweli sikuwahi kucheat hata siku moja toka Niko nae tumeendelea hivyo huku kila mmoja akimuombea mwenzie mwisho wa siku tufunge pingu za maisha.Pamoja na kupitia changamoto katika mahusiano na maisha magumu wakati mwingine lakini nilikuwa mstari wa mbele kuyavumilia na kumpa moyo na kuendelea mbele,

Tatizo wiki iliyopita alinitumia meseji tuachane kwa sababu yeye mipango yake hawezi kuoa mwanamke aliyeenda shule ki ukweli niliwaza sana na mpka sasa nina mawazo ambayo sijui niamue vipi. Ilinibidi nimkubalie japo ndani ya moyo wangu naumia sana hasa vile nilivyomzoea alikuwa kama baba yangu.

Niliona nipime ili nijielewe afya yangu ki ujumla maana niliwaza sana labda huenda alikuwa na MTU wake nje mimi sijui na niliwaza jinsi magonjwa yalivyo mengi sahivi , nilipima HIV nikakuta niko safi nikapima na mkojo nikakuta nina ujauzito.

TATIZO;

Nawaza sana kuotoa mimba hii ila nawaza nitaenda kujibu nini siku nikifa.

Nawaza endapo nikikubali kukaa nao mtoto wangu nitakae mzaa kumlea peke yangu.

Nawaza jinsi ya kuwaeleza wazazi wangu juu ya hali yangu ya uhusiano na hii mimba tena.

Jamani naombeni ushauri wenu niko kwenye kipindi kigumu sana nisaidie.
Wala hicho sio kipindi kigumu.
. Niletee mimba

Nitalea hadi mtoto
 
Hongera kwa kupata ujauzito. Pole kwa kupoteza mtu muhimu kwenye malengo yako kimaisha. Umeeleza kwamba bado unampenda jiulize haya. ..
1.Angekua amepata ajali akafa ungezaa au ungemuulia na hiyo mimba ili uwe umemuonyesha jinsi mapenzi yako yalivyodhahiri?

2.Wewe kwa mtazamo wako unafikiri ndoa ni pepo au ni maamuzi ya wawili kuanzisha familia na changamoto zinakuwepo?

3.Je mama yako angekua ametoa mimba yako kwa changamoto alizowahi kupitia ingekua sahihi au ww waonaje?

4.Wewe unaishi ili nn kwa nn usijiue ww na mimba yako kama kukatisha uhai ni jambo rahisi?
 
Dah...
You gotta keep ya head up even though times is hard never give up.
Zaa mtoto Mungu wako siyo wa box atakujibu.
Philippians 4:13 neno hili likupe company through everything.
 
Back
Top Bottom