Ushauri: Niko kwenye kipindi kigumu sana

kanisela

Member
Jan 2, 2016
6
1
Mimi ni binti nilikuwa kwenye uhusiano na mpenzi wangu kwa miaka minne toka yeye akiwa first year chuo flani hivi, mimi kielimu ninamalizia certificate ya lab tech mwaka huu ikiwa yeye amemaliza na ameajiriwa tayari.

Tulikuwa vizuri ki ukweli sikuwahi kucheat hata siku moja toka Niko nae tumeendelea hivyo huku kila mmoja akimuombea mwenzie mwisho wa siku tufunge pingu za maisha.Pamoja na kupitia changamoto katika mahusiano na maisha magumu wakati mwingine lakini nilikuwa mstari wa mbele kuyavumilia na kumpa moyo na kuendelea mbele,

Tatizo wiki iliyopita alinitumia meseji tuachane kwa sababu yeye mipango yake hawezi kuoa mwanamke aliyeenda shule ki ukweli niliwaza sana na mpka sasa nina mawazo ambayo sijui niamue vipi. Ilinibidi nimkubalie japo ndani ya moyo wangu naumia sana hasa vile nilivyomzoea alikuwa kama baba yangu.

Niliona nipime ili nijielewe afya yangu ki ujumla maana niliwaza sana labda huenda alikuwa na MTU wake nje mimi sijui na niliwaza jinsi magonjwa yalivyo mengi sahivi , nilipima HIV nikakuta niko safi nikapima na mkojo nikakuta nina ujauzito.

TATIZO;

Nawaza sana kuotoa mimba hii ila nawaza nitaenda kujibu nini siku nikifa.

Nawaza endapo nikikubali kukaa nao mtoto wangu nitakae mzaa kumlea peke yangu.

Nawaza jinsi ya kuwaeleza wazazi wangu juu ya hali yangu ya uhusiano na hii mimba tena.

Jamani naombeni ushauri wenu niko kwenye kipindi kigumu sana nisaidie.
 
Kwanza, ulikosea pale uliporuhusu kufunua utupu wako na kumwachia mwanaume avinjali wakati, maandiko yanasema usiyaamshe mapenzi mpaka yatakapotaka yenyewe, kwa maana kuwa pale utakapofunga ndoa.
Pili unasahau kuwa, dhambi si kupata mimba tu, ila hata unapozini unafanya dhambi.
Ninakushauri umrudie Mungu wako na kufanya toba ya dhambi.
 
Pole sn dadangu, nafkri ingekuwa vizur utafute mazingra mazur ya kuongea na huyo jamaa, umwelezee juu ya ujauzito, pia kuhusu namna unavyompenda. Inawezekana ameamua kukuacha kutokana na ushawish wa marafiki au maneno ya kijiweni, hivyo ukipata muda mzur wa kuongea naye mnaweza jikuta mnalifufua penzi lenu.
 
Hebu mpigie simu mkutane na umueleze na kama hataki mkutane mueleze kuwa una mimba yake!

Huyo jamaa ki ukweli hakupendi kabisa na kakuchoka na unachotakiwa ni kusonga mbele hata kama akiendelea kukukataa usitoe mimba bali fight vivyo hivyo uwezi jua huyo ndio mwanao wa pekee ..!

Usitoe mimba mueleze akikataa songa mbele na hata akikubali unatakiwa kujua hakupendi kwa dhati bali mimba ndio sababu!

Usitoe mimba kabisa..
 
Huyo inaonekana ana akili za kushikiwa..Kuna watu watakuwa wamemjaza ujinga..Kipindi chote hicho unasoma na mko kwenye mahusiano alikuwa anafikiri hautagraduate ama?..Umeshamwambia kama una ujauzito wake?
 
Ninashindwa nianzie wapi jaman naona kama labda kuna kitu mie nimemkosea mungu
Nimeongea nae amesema yuko tayari mimba itolewe
Ila nawaza dhambi niliyonayo na ninayotaka kuifanya
 
Huyo inaonekana ana akili za kushikiwa..Kuna watu watakuwa wamemjaza ujinga..Kipindi chote hicho unasoma na mko kwenye mahusiano alikuwa anafikiri hautagraduate ama?..Umeshamwambia kama una ujauzito wake?[/QUOT




Tayari nimeshamwambia ila amesema yuko tayar tuitoe
 
Kama hivo cha kufanya kubali kuzaa na umulee mwenyew. Ondoa imani potofu kuwa ukizaa hautaolewa tena, Diamond yuko na Zari wakati ashazaa watoto watatu, kwahyo asipokuoa yy yuko ambaye Mungu alishamuandaa kwa ajili yako.
 
Anaelea ni Mungu maana toka tunatungwa mimba yeye anatujua. Daudi katika Zaburi 51 anatubu akisema ktk moja ya mistari (Mama yangu alinichukua mimba hatiani). Ninachotaka kusema ni kuwa whatever the situation, mtoto hana hatia na Mungu ndio mlezi maana yeye anajua.

Tubu kwa Mungu kwa ajili yako na kwa ajili ya mtoto then mwambie Mungu amlee huyo mtoto maana wewe huwezi. Usijeukarogwa kuongeza dhambi ya juu ya dhambi.

Kuhusu jamaa mwambie kama haeleweki mwache.

Kuhusu wazazi; tafta namna mwelezee mama yako au shangazi hali yako ili wakusaidie kuwa karibu na wewe.

Hongera na pole. Hongera kwasababu unamwogopa Mungu hakika atakusaidia
 
Kiwango cha elimu yako hakiwezi kuwa threat kwake, afu maisha kusaidiana siku hizi iweje akatae ke mwenye elimu??? 4yrs kwa mahusiano na mimba juu afu hataki mtoto??? Atakuwa ana mtu mwingine anakutafutia sababu, ila kwa mwanaume ambaye hata damu yake haithamini bora umwache aende usimng'ang'anie!!!!
Ukiamua kulea unaweza mama usimwage damu isiyo na hatia...
 
Mimi ni binti....nilikuwa kwenye uhusiano na mpenz wangu kwa miaka minne toka yeye akiwa first year Chuo flan hivi
Mimi kielimu Ninamalizia certificate ya lab tech mwaka huu ikiwa yeye amemaliza na ameajiriwa tayari ....
Tulikuwa vizuri Tu ki ukweli sikuwahi kucheat hata siku moja toka Niko nae tumeendelea hivyo huku kila mmoja akimuombea mwenzie mwisho Wa siku tufunge pingu za maisha ...,
Pamoja na kupitia changamoto katika mahusiano na maisha magumu wakati mwingine lakini nilikuwa mstari Wa mbele kuyavumilia na kumpa moyo na kuendelea mbele,
Tatizo wiki iliyopita alinitumia meseji tuachane kwa sababu yeye mipango yake hawezi kuoa mwanamke aliyeenda shule
Ki ukweli niliwaza sana na mpka sasa Nina mawazo ambayo Sijui niamue vipi

Ilinibidi nimkubalie japo ndani ya moyo wangu naumia sana hasa vile nilivyomzoea alikuwa kama baba yangu

Nilionelea nipime ili nijielewe afya yangu ki ujumla maana niliwaza sana labda huenda alikuwa na MTU wake nje mimi Sijui na niliwaza jinsi magonjwa yalivyo mengi sahivi ,nilipima HIV nikakuta Niko safi nikapima na mkojo nikakuta Nina ujauzito
TATIZO

Nawaza sana kuotoa mimba hii ila nawaza nitaenda kujibu nini siku nikifa.,

Nawaza endapo nikikubali kukaa nao mtoto wangu nitakae mzaa kumlea peke yangu

Nawaza jinsi ya kuwaeleza wazazi wangu juu ya hali yangu ya uhusiano na hii mimba Tena

Jamani naombeni ushauri wenu Niko kwenye kipindi kigumu sana nisaidie .
Pole sana dada hii ndo Dunia,Ushauri wangu ni kwamba Usitoe mimba kwa maana utakuwa umeongeza kosa jingine kubwa zaidi,halafu haujui km Mwenyezi Mungu amempangia nini huyo mtoto,yawezekana ndo Rais wa kesho,suala la malezi lisikupe shida,kwani huyo jamaa km angekuwa amefariki ungemleaje mtoto??,Je ungelitoa mimba kisa wakulea nae kafariki???,Basi wewe zaa then lea mtoto,Halafu usiwe na wasi utakuja uolewe tu,km ipo ipo tu,never give up!!!!.
 
embuacha upuuzi wa kuwaza hata kuitoa....huyo achana naye lea mimba uzae...yuko inferior au labdauliianza kumuonesha mabavu una elimu asikukubabaishe ila sio hivo kwa mujibu wako...hivo hajiamini...ukitoa mimba hutazaa tenea mpaka unakufa we lea zaa
 
Jaribu kumueleza kuwa una ujauzito japo najua kama kishaamua kushika 50 zake ujauzito si kitu, duh pole sana
 
Tunza mimba yko, ukijaaliwa kupta mtot hakika hutajuta.. wanafariji na yey (mtoto )atakupa mapenz ya kweli.. na kuhusu utaipta.. kama ipo ipo tu...!
 
Ninashindwa nianzie wapi jaman naona kama labda kuna kitu mie nimemkosea mungu
Nimeongea nae amesema yuko tayari mimba itolewe
Ila nawaza dhambi niliyonayo na ninayotaka kuifanya
Usitoe mimba acha usenge wewe. Mtoto ataishi hivyo hivyo kama wewe utakavyoishi
 
Back
Top Bottom