Ushauri: Ni wiki amenuna, nimsaidiaje?

JITU LA MIRABA MINNE

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
726
475
Natokea Mwanza mke wangu ni teacher wa shule ya msingi, ndoa 1.5 years, wiki 2 zilizopita kulitokea mgogoro wa ardhi kuna mtu aliingia eneo langu taarifa toka kwa muagalizi wa shamba langu ilikuja usiku sikufanya ajizi ilipofika asubuhi nikamueleza wife na nikamwambia nimedhamiria kuondoka asubuhi hio hio ili kuweka amani yangu ya moyo akanijibu "we nenda tu"

Basi wazee nimeondoka kwenda huko Tanga toka naondoka hadi nafika hakuna kupiga simu yupo kimya tu ila mimi nikimpigia simu mara hapokei, siku 3 kabla ya kurudi ndio akawa hapokei na nilipofia huko Morogoro nilifikia kwa mzee anaenilindia shamba, wakati nimeingia chumba cha kulala nimeingia ndani ya neti nikakutana na nyoka, mwenyeji alinishtua ghafla alipomulika taa kwani nyumba yenyewe ni ya udongo niliporuka na neti nyoka, nikawa nimempumbaza kidogo alikua mweusi ana mabaka baka hata nilipomwambia wife hakutilia maani, nikasema poa halafu yeye akipata shida anapenda umuoneshe antention lakini yeye kiburi na hata akikosa na amejua amekosa hawezi kuomba msamaha atatafuta namna yaishe kimyakimya tu.

Katika maisha yangu nimekua na kifua sana hata akinikosea vipi nagumia rohoni tu kama dume lakini yeye kinachotokea anawaambia wazazi wake.
Sasa hata nilipofika Tanga walipo wazazi wake sikwenda kuwaona nilijua watakua wananichora tu basi nikafanya yangu nikageuza kufika home ananiuliza kinafiki hawajambo huko? Kina mzee(akawataja wazee wake hawajambo )nikamwambia hawajambo"ila baadae nikamtumia ujumbe kwa nn sijaenda kuwaona wazaz wake na nimekuja na akili mpya kwa aliyonifanyia.

Basi toka nimefika amenuna huyo nikaona ujinga huu na mimi nikabadilisha style ya maisha nahudumia kwani tumezaa mtoto mmoja lakini sina mda nae nikiondoka kurudi saa 4, nataka niongeze hadi 6 (kisingizio kusoma kwani nachukua Bachelor) usiku kulala analala wazungu 4 na mimi nikasema okey
moyo umeingia nyongo, kwa kweli JF imekua kama friends wa kushauriana kwani kumfata jirani ni kuchochea moto wa umbea.

Naombeni tips namna ya kuishi na huyu mwanamke kwani simwelewi
halafu kuna kipindi nilianza harakati za kuhamia Airtel kumuacha na kuanzisha uhusiano mwingine ambapo ningemuacha bila mimi kupata maumivu binti ni mzuri nae amesoma alifumania meseji zetu akampiga beat sasa nio njiapanda niishi nae vipi kwani atanipa stroke, atanizeesha, atanipa sukari
wazee ushauri wenu utanijenga au utabomoa.

Karibuni

BACKGROUND

Yeye alinunua kiwanja 20 kwa 30 na gari Canter mimi nikanunua shamba heka 2 Dar, heka 2 Mwanza na heka 1 Morogoro ambazo zipo sehemu nzuri tu mji unavyoendelea kukua tutapiga sana pesa (amekua na kauli mfano gari langu hivi kiwanja changu hivi, halafu ni mvivu hata akifua ukirudi unakuta amenuna ukiona hali hio tu ujue kuna kazi amefanya.

Ukimwambia niloekee nguo nikija nikute umezifua basi atafua kwa hasira halafu unamkuta kavimba kanuna, kama jambo halijaenda sawa ukasema mara 2,3 likirudiwa mwanaume lazima ufoke lakini atasema unamnyanyasa ) lakini mimi shamba letu hivi nyumba yetu hivi napambana kuwekeza na kufanya jitihada japo ndani ya mda mfupi basi familia iwe bora lakini nakata tamaa)

Huu ni ufupisho.
 
Wanasema katika ndoa uvumilivu ni kitu cha muhimu

Kukasirika kasirika ni dalili za kuonesha kuwa huyu mtu bado utoto unasumbua ...inawezekana ipo ivyo pia kwa mkeo

Endelea kuvumilia
Akikua ataacha
 
Ndo nini sasa kama hataki ndoa si arudi kwao? Mambo ya kuzeeshana ya nini?

Kama anashindwa kufanya wajibu wake achana nae. Najua mpaka hapo na wewe una mapungufu yako ila ndoa kuvumiliana mama zetu walipitia makubwa.

ukiona mtu kitu kidogo awe me/ke kanunu hasemi huyo mtu ni zaidi ya shetani.

Mm napenda nikimkosea mtu afunguke anambie yaishe. Sinunaa hadi hali ya hewa ikabadirika.

Wanawake wenzangu kumnunia mme bila kuwa wazi tatizo lako ni nin basi kubari msaidizi (mchepuko)

Ushauri: jishushe ongea nae mara kwa mara akigoma, kunywa juice ya pilipili upunguze machungu, yote yakishndikana " mwambie akupishe arudi kwao. Akiendeleza ubabe kwenye mambo madogo basi mtafutie msaidizi hakuna namna.
 
Mkeo ana tabia ya gubu,usimuendekeze,anza kuweka mipango yako kisiri,mali yako iwe yako maana kama yeye kakutoa kwenye mali zake nawe fanya hivyo hivyo.

Acha kumpigia pigia simu wala sms labda kwa shida muhimu tu,ikiwezekana mara moja moja fua nguo zako au peleka kwa dobi lazima atajiuliza mabadiliko hayo.

Usimbembeleze akinuna mwache anune atachoka tu,ukimuendekeza inakua tabia ya kudumu na kujiona yeye ni kiboko yako.
 
Kuna wanawake wengine hawafai kuwa mke, mwanamke mbinafsi kama nn, Mume ataka mapz na mahaba, na kumjali na kumuheshimu hata kama ni mkali kama simba atampenda tu, mke wake, lakin sio mwanamke anatunishiana misuli na mumewe uliona wapi????
 
Ni seme kwa ufupi, wanawake wengi wana hik kijitabia cha kununa bila sababu ya msingi -wangu huwa namwmbia acha tabia za kijongoo, maana jongoo ukimgusa2 anajikunja.
 
Back
Top Bottom