Juuchini
JF-Expert Member
- Dec 10, 2018
- 1,300
- 1,659
Mimi ni Daktari kitaaluma na ni mwenye kuzingatia maadili ya kazi yangu.
Tangu mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipelekwa idara ya watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Pamoja na huduma za kliniki pia idara hii pia inahusika na upimaji wa VVU kwa wale wateja wanaofika hospitalini hapa kwa ajili ya matibabu lakini hali za maambukizi hazijulikani (unknown HIV status).
Katika harakati za upimaji nikakutana na binti mmoja ambaye umri wa ni miaka kama ishirini na miwili.
Huyu tulipompima tukakuta ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Tukamfanyia ushauri nasaha na kumwanzisha tukiamini ametuelewa kumbe akachukua dawa halafu akaenda kuhifadhi ndani kwake. Ikapita tarehe ya kurudi, ikapita mwezi.
Siku mmoja nikiwa nakagua mafaili nikakuta namba zake nikampigia simu.
Nilipojitambulisha akakataa simu akatumia sms kuwa nimwache afe.
Baadae nikaendelea kutumiana nae meseji za kumshawishi atumie dawa lakini ananizungusha sana.
Jana aliniomba nimtembelee lakini
Nikashindwa kutokana na majukumu yangu
Leo pia akaniomba nimtembelee na bado nikakwama kutokana na kubanwa na majukumu.
Kilichonifanya niandike huu uzi ni kwamba amekuwa akilalamika sana kama vile tuko kwenye mahusiano.
Na anahisi mimi ninamnyanyapaa
Kisa ana maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Mimi ni mhubiri wa yale maneno kwamba "ukitumia dawa za ARV huwezi kuambukiza wengine" .
Lakini binafsi siamini kitu kama hicho.
Sasa wadau nifanye nini maana niko kwenye Ethical dillema.
Ushauri wenu jamani.
Sent using Jamii Forums mobile app