Kuna binti nipo nae kwenye mahusiano kwa muda kidogo. Kipindi chote tulichokuwa kwenye mahusiano tumepita kwenye nyakati tofauti ngumu na nzuri.
Ukweli ni kwamba, mwenzangu kwa bahati mbaya amepoteza wazazi wote wa wili angali akiwa mdogo.
Hvy kwa malezi amelelewa na ndugu zake mpaka kufikia umri wa kujitegemea. Changamoto ni kwamba mwaka 2017. Dada yake mkubwa alipata tatizo la ajira...lililosababista kupata tatizo la kiharusi (strock) ya mwili mzima. Hali iliyomfanya kuhudumiwa kwa kila kitu.
Balaa ni kwamba ndugu wamemsusia huyu dada jukumu la kumlea mgoja toka 2018..jambo lililomfanya ashindww kabisa kuendelea na mambo mengine binafsi ikiwa ni pamoja na swala la yeye kupata kazi.
Upande wangu tulipanga kuoana toka mwaka 2019. Lakoni hii changamoto imekuwa kikwazo katika jambo hili muhimu...nimeshindwa kuendelea na taratibu muhimu nikihofia jambo hili kama ndugu wenyewe hawatoi ushirikiano naona kama inaweza niletea shida.
Kama ni kuvumilia na kujitoka nimejitahidi sana lakini naona kabisa jambo hili linakwenda kunishinda ndugu...zangu naombeni ushauri katika hili...[emoji120]
Natanguliza shukrani.