Mkumbushe sababu ya siku ya kwanza kukutana na sababu iliyofanya Aishi kwako.
Mimi ningekuwa wewe,ningetafuta chumba kizuri nikampangia,nikamwekea kitanda na godoro..then siku ya siku mnatoka sehemu iliyotulia mnazungumza na kumkumbusha Kwanini alikuja kukaa kwako.
Inawezekana kwa mwanamke ikawa ni ngumu kukuelewa lakini ni bora umuumize kumwambia ukweli akae akijua.
Baada ya kumkumbusha ukweli unamwambia nimeshakutafutia chumba na umelipa kwa miezi kadhaa na kitanda kipo ndani kwaajili ya kuanza maisha.wewe akuache kwenye nyumba yako kama alivyokukuta.
Atalia ,ataumia,atakulaumu,atakuona mbaya sana tena mkatili..kwakuwa hisia za kimapenzi kwake zimeshika hatamu lakini siku akija kurudi kwenye mhimili wa akili,atakushukuru sana na kukuombea(inawezekana asikwambie kuwa anakushukuru nakumuomba Mungu kwa ajili yako)lakini ukweli atakuwa na shukrani.
Maisha Haya hayatabitiki hakuna sababu ya kuachana vibaya wakati unaweza kutumia njia ya kiustaarabu na kiuungwana kuachana na mtu