Ushauri, Nataka kusoma Computer Science (Online Course)

Ushauri, Nataka kusoma Computer Science (Online Course)

Tetramelyz

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
4,372
Reaction score
12,479
Hii course inatolewa Havard University kupitia mtandaoni (online) na wanafundisha vitopics hivi;

-Abstraction,
-Algorithms,
-Data structures,
-Encapsulation,
-Resource Management,
-Security,
-Software Engineering, na
-Web Development.

Kwa mnaofahamu, kozi hii ina changamoto gani na nijiandae vipi? Nimewiwa kutoka moyoni kuisoma kwakuwa ni bure na inatolewa na chuo bora duniani, kwakuwa nataka kuongeza maarifa.

Nimeiona hapa Introduction to Computer Science

Karibuni waungwana kwa ushauri n.k.

NB:Moderator naomba huu uzi usipelekwe jukwaa la elimu.
 
Hats Mie natamani Sana kusoma hyo kitu. Chamsingi in kuwa an Nia YA DHATI TU.
 
Algorithm na Data encapsulation zipo kwenye C and C++ Programming language, Data structures sikushauri Sana kwa sababu ni ngumu kuisoma online
 
Hapo kwanza lazima uwe na ABC ya mathematics kingine ujitoe sana katika mazoezi ya programming
 
Algorithm na Data encapsulation zipo kwenye C and C++ Programming language, Data structures sikushauri Sana kwa sababu ni ngumu kuisoma online
Kwani kwenye hivyo vipengele vya kusoma ninaweza kusoma baadhi na vingine nikaacha??
 
Hesabu lazima uwe na mwanga kidogo mfano ukiambiwa usolve quadratic equation lazima uwe unaijua
 
Hesabu lazima uwe na mwanga kidogo mfano ukiambiwa usolve quadratic equation lazima uwe unaijua
Hilo halina tabu, hata integrals na differential equations nazifahamu sana
 
Elimu popote ila tenga muda na uwezo wako inawezekana, jamaa yangu alimaliza course za online na alienda kukamalizia miezi miwili huko kwa wakoloni.
 
Naomba maelezo zaidi kama hutojali. Sijakuelewa hapo kwenye accredation
Nenda kaulize TCU kama hicho chuo wanakitambua hasa kwa namna ya utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao, ili usije ukapoteza muda wako bure. Sheria inahitaji wahitimu wote wa vyuo vya elimu ya juu vilivyo nje ya nchi wapeleke vyeti vyao vikapewe certificate of recognition. Hii inatolewa na TCU kuthibitishia umma kwamba ulisoma chuo au programme isiyo na hatihati. Sasa kama umeshasoma ukamaliza halafu uje kuambiwa degree yako haitambuliki, utakuwa umekula hasara, ndio maana nikakuambia kabla hujafanya registration, nenda TCU wakakuthibitishie mapema. Usiangalie ukubwa wa jina la chuo
 
Nashukuru sana kamanda, nitafaNya hivyo
 
Kama unasoma ili utambulike kua umesoma chuo fulani then unapoteza muda, maana edx ni sehemu unajisomea mwenyewe tu kama tuition vile, na cheti ukilipia wanakupa ila huwezi kitumia kama cheti cha chuo.

Ila bado nakushauri usome, hiyo ni course moja tu kati ya nyingi, hapo ukiimaliza hujagusa hata 2% ya computer science, CS50 hata mimi niliisoma hiyo course online nilipokua mwaka wa kwanza chuoni na ilinisaidia sana kupass courses nilizokua nasoma chuoni kwa kua nilikua sina knowledge ya programming kabla sijaingia chuoni. Ni course nzuri sana na inajaribu kukuonyesha what's possible kwenye Computer science, japo haiingii deep sana, wanagusia juu juu lakini wanachofundisha ni fundamentals ambazo kila mtu inatakiwa ajue. Na mtu asikudanganye kua haya mambo huwezi jisomea mwenyewe, kwani anayekaa darasani anafundishwa na mwalimu, na anayekaa kwenye internet anaangalia mwalimu akifundisha wana tofauti gani? Kama una swali hata comment section, stackoverflow zipo unauliza watu wanakujibu haraka tu tena mara nyingine vizuri zaidi kuliko mwalimu wako wa darasani. Kitu kigumu kujisomea mwenyewe mi naona ni hardware tu.

Ukisoma CS50 ukaimaliza na ukaelewa vizuri, unaweza ukajisomea na courses nyingine pia, hawa jamaa wanatema madini ambayo hutokutana nayo kwenye vyuo vya Tanzania, course za lazima kuchukua Algorithms and Data Structures, ningeshauri pia uangalie na Introduction to Data mining, hadi kufika hapo utakua unajua mwenyewe direction ipi unataka kwenda, kama ni kwenye games, robotics, web, mobile, au general application software kusolve matatizo mbalimbali kama kilimo kwa kutumia drones e.t.c Unaweza jifunza online yote haya na ukayaelewa, sema usitegemee cheti, kama unasomea cheti then unapoteza muda na utaishia katikati haya mambo yanazidi kua magumu na mengi mno unavyoenda juu.
 
Mimi natumia sana online courses kuongeza maarifa , natumia sana coursera na udacity , pia kuongeza uzito wa cv kwa kusoma course zilizo nje ya field yangu. Kiukweli nafurahia sana online courses kwani wanatema madini ya ukweli sana. Mkuu nakushauri soma kwa kujiongezea maarifa zaidi , itakusaidia sana.
 
nashukuru sana kamanda Graph ,ninachofanya mimi ni just kuongeza ujuzi na kupanua ufahamu tu na sio kwaajili ya kupata cheti. Ahsante kwa mawazo yako mazuri na experience.
 
Back
Top Bottom