Ushauri: Nataka kuoa mwanamke ambaye simpendi

Jr. Gong Mira

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
1,279
1,295
Wakuu habari za Weekend.

Mimi ni kijana na nimefikia umri wa kuoa sasa, ila changamoto ni kutaka kumuoa msichana ambae hayumo katika hisia zangu, ila sababu ya yeye ana tabia zote nzuri, lakini mimi tu sijavutiwa sana kwa upande wa sura tu basi.

Na kwa upande wake ananipenda zaidi ya sana na hana tatizo lolote na mimi. Samtime hua najipa moyo labda tukiwa katika ndoa nitampenda. Ushauri naomba, je nimuoe kulingana na sifa na tabia zake nzuri!?

Ahsanteni.

1625726233115.png
 
Wakuu habari za Weekend.
Mimi ni kijana na nimefikia umri wa kuoa sasa, ila changamoto ni kutaka kumuoa msichana ambae hayumo katika hisia zangu ila sabubu ya yeye ana tabia
Bwana mdogo linapofika swala la kuoa tunaoa character na si umbo. Hujawahi ona ya kuwa wanawake wenye sura nzuri wanakosa kuolewa? Na vile wenye sura za kawaida tu ndo wengi wao wameolewa?
 
Naomba nikuulize,

1. Hakuna wasichana wazuri wenye character nzuri?
2. Je kila msichana mmbaya ana character nzuri?

Asante kama nitajibiwa
Bwana mdogo linapofika swala la kuoa tunaoa character na si umbo. Hujawahi ona ya kuwa wanawake wenye sura nzuri wanakosa kuolewa? Na vile wenye sura za kawaida tu ndo wengi wao wameolewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi utu ndio mapenzi? Muonekano, tabia vyote si kitu kama hamna hisia.
Huyo hampendi huyo dada Bali anapenda jinsi alivyo na utu. Akatafute anaempenda huyo aache watakaompenda wamuoe
Utu wa mtu ni muhimu sana kuliko muonekano wa nje.
Oa huyo mkuu. Huyo ndo mke wako sasa.
Na usipomuoa utakutana na kurumbembe moja litakalokufanyia utajua maisha yako yote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Usimuoe kama hayuko kwenye hisia zako kwa sababu ukipata alie kwenye hisia zako utamtesa mwanamke wa watu.
Kama unaona hakufai muache apate atakaempenda bila kuangalia mengine Bali upendo alio nao juu yake.

Sent using Jamii Forums mobile app

We mdada nimekumiss mnooo .... huonekani mara kwa mara humu jukwaani aisee .... naamini upo salama
 
Cha kushangaza watu wengi wanaweka muonekano mzuri wa sura/umbo na tabia zisizofaa. Kwao mwanamke mwenye sura ya kawaida ndie ana character nzuri.
Ndio maana hata hapa wanashauri amuoe kwa sababu tu ameandika sura yake sio ya kuvutia basi wameshaamini anafaa hata kama mwenzie hana hisia nae
1. Wapo wasichana wazuri na wenye character nzur tu.
2. Sio kwel km kila mbya ana character mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom