DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,986
- 3,151
Mkuu elezea tu kwa ujumla wake maana tunaopatamani ni wengi.
Kwa kuishi kupitia kilimo, ufugaji na biashara za kununua na kuuza haswa vyakula.
Mkuu elezea tu kwa ujumla wake maana tunaopatamani ni wengi.
Kwa kuishi kupitia kilimo, ufugaji na biashara za kununua na kuuza haswa vyakula.
Nina miaka minne sasa naishi mbinga, sijui nitatoka lini lakini lazima nitimize nilichokipanga.
Sababu;
1. Mbinga kuna fursa nyingi za kiuchumi hahasa kilimo, biashara, ufugaji na madini.
a) Kilimo, hapa ndo mahala pake unaweza amua kulima au kununua mazao na badaye kuyauza ama vyote, mazao yanayolimwa kwa wingi ni mahindi, ufuta, maharage, alizeti, kahawa na miti. Maeneo kama matiri na kindimba juu huko maharage usiseme japo matiri na mahindi sana tu, maeneo ya mkako, kiwombi, amani makolo nk. huko mahindi, ufuta, alizeti ushindwe wewe.
b). Misitu, hali ya hewa inayoruhusu ukuaji wa miti hasa maeneo ya milimani.
C). Madini, kuna biashara ya madini inaendelea japo wengi hawajui kuna vijana wengi hasa wa kutoka nje ya Ruvuma wamefanikiwa kwa biashara hii hapa mbinga, maeneo ya mkako, Masuguru, Amani makolo, mkeso nk. Huko kuna rubi.
C) ufugaji, aridhi ya kutosha
2. Upatikanaji wa aridhi, huku aridhi ni bei rahisi kuanzia 30000 na kuendelea kwa ekari kutegemea eneo na hali ya shamba, je ni jipya au limetumika na pia miundombinu.
3. Jambo la mwisho kubwa, hapa naomba nisieleweke vibaya. Uelewa wa raia. Lazima tukubaliane kwamba ubepari huambatana na dhuruma na hilo linafanikiwa kirahisi ikiwa uelewa wa wananchi uko chini, sasa basi kwa mbinga hali iko hivyo, kwa mfano, mfanyabiashara anamkopesha mkulima mfumo mmoja wa mbolea wa thamani ya 40,000 tshs. halafu anakuja kulipwa gunia 3 au 2.5 wakati wa mavuno halafu mkulima anaona sawa tu au anakopeshwa shilingi 20000 na anakuja kulipa gunia moja la mahindi na hata serikali iingilie kati mkulima haelewi.
Nb. Huo ni mtazamo wangu, na asiwepo mtu wa kufikiri akifika mbinga basi ndo kamaliza kazi, kunachangamoto kwenye kila kitu kimsingi hatupaswi kuogopa wala kukata tamaa yawezekana ukalima mwaka huu na usifikie matarajio huo si mwisho lazima tupambane.