Ushauri: Nashindwa kujizuia hisia zangu

Dec 22, 2016
7
20
Nashindwa kabisa kuzi-control hisia zangu kila mwanamke nitakayemuona mimi natamani niwe naye, hii hali inanitesa sana, nikitaka kujaribu kujizuia nashindwa kabisa na muda mwingi nikikaa nawaza kuhusu wanawake sina hata muda wa kufikiri vitu vya msingi.

Sasa kama kunamtu anaweza akanisaidia jinsi ya ku-control hisia zangu au kama anafahamu chochote kuhusiana na tatizo langu.

Please msaada!
 

Plan Paris

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,916
2,000
Fanya mazoezi kila siku , tafuta marafiki wenye tabia nzuri na wanaofanya vizuri darasani, hudhuria vipindi vya dini, muombe mungu pia jisomee biblia, jikite kwenye masomo tumia muda mwingi kusolve maswali hasa hasa hesabu , fizikia n.k
Fanya kitu unachokipenda kama kufuatilia mpira n.k
SEX huondoa MAARIFA
Mwisho
PAMBANA UWEZAVYO KUTIMIZA NDOTO ZAKO
 

pistmshai

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,315
2,000
Nashindwa kabsa kuzkotroo hisia zangu kila mwanamke ntakaye muona me nataman nwe naye

kila mwanamke?!!!:D:D:D
mkuu wewe ni umeme wa radi..! hiyo hali ikiendelea, baadae utatamani hata ndugu zako. (kama bado hujaifikia hiyo hatua)

  • Huenda una pepo mkuu...! tafuta msaada wa kiimani.
  • Huenda watu wako wa karibu (mfano. marafiki) wanakuchochea uwe hivyo, badilisha kampani yako, kuwa karibu na watu wenye mtazamo chanya.
  • Huenda tatizo ni wewe mwenyewe, jichunguze mienendo yako, kisha badilika.
TERRIBLE:(
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,576
2,000
Nashindwa kabsa kuzkotroo hisia zangu kila mwanamke ntakaye muon me nataman nwe naye ii hali inantesa sana nkjalibu kujizuia nashindwa kabisa na mda mwingi nkikaa nawaza tuu kuhusu wanawake sina ata mda wa kufkil vtu vya msingi

Asa kama kunamtu anaweza akansaidia jinsi ya kukotroo hisia zangu au kama anafahamu chochote kuhusiana na tatzo langu pls msaada

Kwa hivi unavyoandika kazana na shule kwanza.

Kwa ufupi hilo siyo tatizo ni hatua ya kubalehe.

Kwa urefu;

kwa umri wako hivyo unavyojisikia siyo kitu cha ajabu ni kawaida, katika kipindi hiki unakua na gusa hiki acha, jaribu kile acha, au nifanye anachofanya fulani nyingi.

Unachohitaji ni kupata mtu wa kuongea naye, itapendeza kama atakua mzazi wako. Lakini kama maisha yako ni kama ya waTanzania wengi, jitengenezee ratiba ya kuifuata kila siku.
Tafuta kitu ambacho unaweza kuwa mzuri katika hicho mfano unaweza kuamua uwe unajifunza gita, au unaweza kuwa na ratiba na chochote ambacho una passion nacho.

Kuna mdau kasema fanya mazoezi, fanya na ule inavyotakiwa naamini itasaidia.

Mengine yatasemwa na wadau wengine.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
195,362
2,000
Kumbe tupo wengi tofauti yangu mie kila msuko wa rasta nautamani hata kama nimesuka jana yake, nataman kufumua hizo, nisuke msuko niliouona muda huo.

DAWA NI ACHA TAMAA.
 

mwamba c

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
690
1,000
Kuna mawili ya kufanya moja kuwa nao hao unaotaman kuwa nao ili utimize haja za kimwili au amua mwenyewe kubadili mtazamo wako juu ya wanawake...
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,576
2,000
Kumbe tupo wengi tofauti yangu mie kila msuko wa rasta nautamani hata kama nimesuka jana yake, nataman kufumua hizo, nisuke msuko niliouona muda huo.

DAWA NI ACHA TAMAA.
Si unajilipia mwenyewe au kuna mtu anapasuka?
 

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
8,846
2,000
Nashindwa kabsa kuzkotroo hisia zangu kila mwanamke ntakaye muona me nataman nwe naye ii hali inantesa sana nkjalibu kujizuia nashindwa kabisa na mda mwingi nkikaa nawaza tuu kuhusu wanawake sina ata mda wa kufkil vtu vya msingi

Asa kama kunamtu anaweza akansaidia jinsi ya kukotroo hisia zangu au kama anafahamu chochote kuhusiana na tatzo langu pls msaada

Ndio umeingia balehe nini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom