Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

Ushauri: Najuta kuingia kwenye mahusiano

BILGERT

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2015
Posts
6,532
Reaction score
11,027
Habarin za jioni wana MMU.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,nina kazi ambayo inaniingizia kipato changu kinachonikimu ktk maisha nipo kwenye mahusiano na binti mmoja kwa takribani mwaka mmoja sasa, ambaye pia ana kipato chake kizuri tu,tumekuwa tukisaidiana katika shida na raha, wiki moja iliyopita huyu binti, aliniambia kuwa amepatwa na shida ambayo inagharimu kiasi cha shiling laki nne na akaniahidi atanirudishia mwezi wa kwanza, hivo akaomba nimuazime.

Huyu binti namshirikisha kwenye mambo mengi sana, ikumbukwe nilishawahi kumshirikisha malengo yangu,na pia nikamjulisha kiaisi ambacho kinahitajika ili hayo malengo yaweze kutimia na pia isitoshe nikawa nmemjulisha kiasi ambacho nimefanikiwa kukikusanya na kukihifadhi katika account yangu ya akiba.Maana nlipanga kufikia 2016 mwezi wa 7 niweze kuanza kutekeleza hayo malengo yangu,vyote hvo nilimshirikisha.

Hivo alivyonifuata kuomba nimuazime hyo hela alijua kabisa siwezi kumnyima kiukweli kutoka moyoni sikupanga kabisa kuigusa hyo hela maana nafahamu madhara yake,nlikuwa nathubutu hata kujinyima mwenyewe kipindi nmekosa hela, niko tayari nitafute hela sehemu nyingine ili mrad tu saving account yang ibaki salama.

Baada ya yeye kuniahidi kuwa hyo hela itarudi mwezi wa kwanza kama ilivyo nkawa nmeamua kumkabidhi hyo laki nne.Juzi kati tar 20 siku ya ijumaa ya mwezi huu tukiwa tunachat akaniambia kuwa anashukuru kwa kumkabidhi hiyo pesa, mimi nkamuambia asijali ila nkamuomba anirudishie hyo pesa mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.Hapo ndo ugomvi ulipoanzia, akaniambia kuwa mimi sina utu wala ubinadamu na nina roho ya kinyama,maana haiwezekani nimuazimishe pesa hata wiki mbili hazijapita naanza kumdai hivi wadau iko sawa kweli hii? Akawa amekasirika sana, siku ya jana usiku akanipigia tena akaongea tena maneno yaleyale kwa hasira sana, akasema kuwa amemuomba mtu amuazime hela ili anirudishie na hatothubutu tena kuniomba ama kuazma chochote kutoka kwangu.

Nimejaribu kumuomba sana na kumsihi kuwa mimi sikumaanisha anipe saivi ila nichosema ni kwamba anipe mwanzoni mwa huo mwezi wa kwanza.anasema kuwa lazima anirudishie ndani ya wiki hii maana mtu aliye muomba hawezi kumzuia asitume kwa madai ya kuwa anaogopa siku atakapo muomba tena ataonekana anamtania nipo njia kuu wadau yaani sijui nifanyaje,je nmemkosea nini? Maana tangu hiyo jana usiku hatujaongea wala hajanitafuta mpaka saivi simu hapokei, najiuliza je,ana mpango gani na mimi? Mbona ananifanyia vitimbwi vya ajabu hvi? Pia nafikia mahali najuta kumshirikisha huyu mtu mambo yangu,wenda asingefahamu nina kias gani cha pesa pia najiuliza kwa hayo yanayotokea nini hatima yake?

Samahani kwa thread ndefu wadau ila nna huzuni sana, maana sijui hatima ya huu uhusiano na pia sijui hatima ya pesa yangu maana simu hapokei, naomba mnishauri ndugu zangu, maana naiona dunia chungu.

Natanguliza shukurani kwenu nyote
 
ndio matatizo ya mapenzi, yanahitaji uvumulivu na kuweza kuyatatua, kama anakupenda basi atakua mweledi, punguza stress endelea na kazi zako
 
ndio matatizo ya mapenzi, yanahitaji uvumulivu na kuweza kuyatatua, kama anakupenda basi atakua mweledi, punguza stress endelea na kazi zako

nmekusoma mkuu,ahsante
 
Acha ujinga wewe chukua chako mapema kwa umeoa!ndugu zako wapo kijijini wana hali mbaya alafu unajipendekeza,sisi wachaga huwa hatumwambii mtu yoyote una kiasi gani kwenye account.
 
Something you're not telling us...
cwezi nkaficha kitu mkuu,maana mficha maradhi kifo humuumbua..nmeeleza kila kitu kutokana na situation ilivo na jinsi mambo yalivotokea
 
Malengo yenu yanatofautiana
Afu wewe kwenu ni mzaliwa wa pili yeye kwao wa mwisho!
Ha ha ha m kidding!!
 
Anapima upendo kwa pesa... Anazira.. Anapenda kubembelezwa.. Chukua pesa zako akizileta, kaa kimya. Akienda hakuwa wako, akirudi alikuwa wako
^^
 
Maskini pole, na ukicheza utazidiwa kete atajifanya kasusa mazima na kukuacha juu na hela usilipwe....
daah,nmeumia sana dada evelyn salt..yaan hapa nacho wazia ni nn hatma ya huu uhusiano.angalau hata pesa,siiwazii sana
 
Huyo msichana still looks very immature. Kama alikuomba na kukubali atakurudishia, hapo hakuna shida, una haki ya kumkumbusha. Kingine at 24, you're still very young, there is no need to rush into relationship, just take your time, build up your life, do something productive and useful for your future. Msichana wala asikupe presha. At the right time when you're ready to start a family, ask GOD to give you a very good girl.

There is no point engaging in relationships which leads nowhere. I dont understand the level of seriousness that you had in the relationship and whether you had long term plans together. Hata kama ni hivyo, let he go, wala asikupe presha, wewe unathamani kubwa sana. Tengeneza maisha yako ya baadaye, yaani wala usihofu. Pia msisitize akupe hela zako, kwasababu alikubali kufanya hivyo, kama hataki, wewe utaona what to do next. Whether kwenda kwenye vyombo vya sheria au kumsamehe deni.
 
Polee Sanaa!! Next Time Usirudie Tabia Ya Kumwambua Mtu Yyte Kias Cha Pesa Kwenye Akaunt Yako Na Inaonekana Huyo Bunti Ulimuamin Sanaaa....Naweza Otea Hata Mama Yako Mzaz Au Baba Aujawah Mwambia Hicho Kiasi Ulichonacho Kwenye Akaunt Ila Binti Ukamwambia..Huu Ni Mojawapo Ya Udhaifu Mkubwaa Sanaaa...Na Kwa Hii Case, Unachotakiwa Sasa Ni Kuchagua 1, Pesa Au Huyo Binti!!! Kma Ni Pesa Uwe Tayar Kumpoteza Binti Na Kma Ni Binti Huwe Tayr Kuzipoteza Pesa!! Kwa Maelezo Yako Binti Muhuni So Chagua 1. Na Kingne Ukichagua Binti, Fahamu Uwezekano Ni Mkubwa Wa Binti Kuja Kukuzngua Kivingine, Kwa Hiyo Stor Kishaonyesha Yeye Ni Kimeo!!! Ulipokua Unashare Nae Mambo Ya Akaunti Yy Alikua Anazitaman Hizo Pesa.
 
Mkazie tu akupe pesa yako, madem hawanaga dhamana ndugu yangu' utajikakamua kutoa vipene vyako kwa lengo la kumfanya akuone una care kumbe mwenzio hana hata mpango na ww! pia hakuna ulazima wa mwanamke kujua mipango yako hao hawana maana kaka! mkazie kwa njia ya sms arudishe pesa yako
 
Huyo msichana still looks very immature. Kama alikuomba na kukubali atakurudishia, hapo hakuna shida, una haki ya kumkumbusha. Kingine at 24, you're still very young, there is no need to rush into relationship, just take your time, build up your life, do something productive and useful for your future. Msichana wala asikupe presha. At the right time when you're ready to start a family, ask GOD to give you a very good girl.

There is no point engaging in relationships which leads nowhere. I dont understand the level of seriousness that you had in the relationship and whether you had long term plans together. Hata kama ni hivyo, let he go, wala asikupe presha, wewe unathamani kubwa sana. Tengeneza maisha yako ya baadaye, yaani wala usihofu. Pia msisitize akupe hela zako, kwasababu alikubali kufanya hivyo, kama hataki, wewe utaona what to do next. Whether kwenda kwenye vyombo vya sheria au kumsamehe deni.

Nashkuru sana kwa maneno yako yenye ushaur mzur,,ahsante sana.Mungu akubariki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom