Unajua maana ya "Shikamoo" lakini?! shikamoo maana yake "nakushika miguu" shika-moo! moo ni miguu!
Turudi kwenye mada! Me nadhani tatizo hilo lipo hasa kwa wanawake (wamama watu wazima) hawa huwa na tabia ya kujifanya bado wamo hata kama umri umesonga! wengi wao hawataki shikamoo kabisa!
hata huku pande za kwetu wapo wengi sana ukiwaamki hawakujibu au hujifanya hawajasikia.
Na wakishajua wewe unatabia ya kuwapa shikamoo, basi wao wakikuona wanakuwahi haraka na "mambo" au "habari yako" ukiona hivyo ujue hawataki "shikamoo! hata kama wamekuzidi miak1 10 au zaid! Na ukiwasalimia kwa kuwapa "mambo" au "habari yako" wanafurahi sana na kukuchangamkia sana kuliko ukiwapa shikamoo wanakujibu kama hawataki!
Nakushauri wala usikwazike kwani kama ushavuka teenager wewe sio mtoto tena! karibu kwenye adult hood! sio lazima kutoa shkamoo! ziko salaam nyingi nzuri kama "habari zenu, umeshindaje, hali yako, mambo vipi, wajionaje na hali n.k.