Ushauri: Nahitaji kuwa public speaker

Asovene

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
213
216
Miongoni mwa mambo ninayopenda kufanya ni pamoja na kuwa mzungumzaji mbele za watu yaani masuala ya TAALUMA, mijadala ya kitaaluma. Lakini nakutana na vikwanzo mbali mbali kama vile:
  • Kuonekana mjuaji yaani unajifanya unajua kila kitu.
  • Kujipendekeza.
  • Kuingilia mambo ya watu.
  • Kutafuta sifa za kijinga, siyo kila kitu lazima uongee kama unajua kausha.
  • Kuchekwa.
Nimejaribu kujizuia lakini siwezi kutulia nikiona mijadara hasa nikiwa darasani siwezi kujizuia kuongea au kuuliza swali.

Kwa wataalamu na watu wa saikolojia nawezaje kufikia malengo yangu?
 
Huwezi kuzuia watu kusema ila una uwezo wa kupuuza kile wanachosema.

Ukiona siku hayo uliyoorodhesha hawayazungumzii tena fahamu kuwa umeacha kuwa wewe badala yake umekuwa wao.

Endelea kuwa wewe.
 
Jaribu kupima kina cha maji kabla hujavua nguo kuogelea,huenda unajadili maada fulani kwa audience wasioijua utakumbana tu na hali hiyo.No challenges no support of motion.
Anza na kundi dogo la watu unaowafahamu ,usiwe tu speaker mzuri but also be a listener utafanikiwa tu.
 
Kama hivyo vikwazo vimekuwa vikikukuta mara kwa mara kutoka kwa watu tofauti tofauti mahali tofauti tofauti. Basi kuna uwezekano una matatizo yafuatayo;

Kuonekana mjuaji na kujifanya unajua kila kitu
  • Katika mazungumzo yako huwa una-negative attitude muda mwingi. Yaani huwa sio mwepesi wa kukubaliana na hoja ya mwenzako hata kama ni fact (utatafuta tu mahali pa kukosoa), au hata kama umekubaliana nayo huwa haukili kwa kwa maneno kuwa umekubaliana nae.

Kujipendekeza
  • (Ingawa muda mwingine sio jambo baya), kujipendekeza mara nyingi sio jambo baya sana, maana hukuweka karibu na watu ambao hujazoeana na mara nyingi huleta matunda mazuri baadae. Ila huenda namna yako ya kujipendekeza sio nzuri sana,huenda hauangalii nyakati wala muktadha, (yaani naweza kusema unakurupuka).

Kuingilia mambo ya watu.
  • Hapa inategemeana tena na wakati na muktadha, hata lengo lako ni lipi. Huenda watu walishakugundua kuwa wewe ni mchonganishi ndio maana huwa hawataki uhusike kwenye mambo ambayo hujashirikishwa.

Kutafuta sifa za kijinga
  • Mkuu...! ukiona mtu anakwambia hivyo basi ujue,ni kweli unapenda sifa. Tena watu kama nyie huwa mnapenda sana kujitafutia sifa kwa kumdharirisha mtu. Ipo siku utapigwa, sifa zinaua.

Kuchekwa.
  • Ukichekwa, utajisikia vibaya kama uliongea pumba, ila kama unajiamini na ulichoongea huenda wanaokucheka ndio wajinga.
 
Back
Top Bottom