Ushauri: Nahisi natumika na ndugu zangu

Ushauri: Nahisi natumika na ndugu zangu

Mm ni kijana wa miaka 25 nmemalza chuo fulani mwaka juzi tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni hii swala la kutumika bila manufaa yoyote ninayoyapata
1 . nlivyomaliza chuo baba alinipeleka manyara nikasimamie mashamba yake ya vitunguu mangola bila mshahara wowote(ananihudumia nauli na hela ya kula tu) kwa kweli nilifanya ile kazi kwa juhudi zote ila misimu yote miwili aliyovuna hajanipa hata 100.
2.baada ya project ya baba kuisha kaka yangu alianza ujenzi wa nyumba TEGETA nkaenda kusimamia ujenzi na huyu pia hakuna Lipa.
3.dada yangu ana vi biashara vyake huwa ananituma kufatilia pesa zake pamoja na kupeleka bank karibia kila siku pasipo na malipo pia....kuna kazi nyinyingi ambazo sijazitaja..hii Hali kwa kweli imenishinda kutumika japo ni ndugu zangu na mimi nahitaji kujenga maisha yangu tatizo ajira hamna na wote hao nimejaribu kuwaomba mtaji hakuna aliyenipa kila siku napigwa Dana Dana tu....juzi baba kaniita anataka nirudi manyara kusimamia mashamba yake na kimila kila kitu anachosema baba lazma ufate lasivyo atakuvulia nguo akulaani(apa nafuta machozi ) 😢😢......naomba ushauri ndugu zangu nifanyeje? ?au ni kawaida mm tu ndo nmepanic ?

Hii inakupa good experience ya kaxi na ujuzi acha kulalamika fanya kazi jenga uchumi wako kwisha habari.
 
Kina watu mnapata mwanzo mzuri sana wa maisha baada ya kutoka vyuoni halafu hamjui namna ya kujiongeza...

Unasubiri siku baba aanze kukulipa mshahara? Bila shaka utakuwa unasubiri Meli airport..
 
We na wee unakubalije? huyo baba yako angekuwa na mtoto kauzu fc kama mimi yaani angeshika kichwa maana angegomewa vibaya mno... we sahiv unatakiwa kusimamia mwenendo wa maisha yako na sio unatumwa tumwa tu hata kama ni ndugu zako gomaa acha uzembe kijana
 
Chemsha bongo kijana, huo ni uzembe wako acha kusingizia baba na nduguzo. Hakuna aliekufunga kamba, unaelimu ila inaelekea hujaelimika, kusimamia mashamba la mzazi wako si dhambi, wakati unasimamia hilo shamba unatakiwa uangalie fursa zilizopo eneo hilo na hata kujikodia shamba lako. Wakati unamaliza kusimamia shamba la mzazi wako na wewe unakuwa na chako. Kusimamia biashara za nduguzo, sasa dogo huna kazi, unataka ule na kulala tu? Hiyo kusimamia biashara ni mtaji wako wa siku zijazo. Wengi tulio katika ajira tunatamani tuwe na kipato kendo ya kazi kwa kufanya biashara, tunashindwa kwakuwa hatuna uzowefu, wewe kwa kusimamia biashara hizo utapata uzowefu utakao kunufaisha baadae.vijana wengi umri huo huwa na matarajio ya ajira mara tu mmalizapo Masomo bahati mbaya mnakutana na msoto kwa muda na mnakosa uvumilivu. Lakini usichoke kusaka ajira, ipo siku utapata hata kama baada ya miaka 3/4. Punguza kulalama..woga wako ndio umasikini wako!
 
Kufuta Meza na degree yangu ya uhasibu ntakua sijaitendea haki. ..by da way thnk you for ur comment

Kuwa foreman site au errand boy kwa sister ndo umeitendea haki?.
Sasa nakushauri:
Ukiwa na ndugu wasio na moyo wa kukunyanyua, pigana mtaani. Waonyeshe upo busy, na usiwe mtu wa kukaa kaa hovyo nyumbani. Pili, wakati hujapata kazi kumsaidia baba yako ni sehemu ya wajibu wako kama mtoto. Ukipata kazi yeye mwenyewe utaona hawezi kukuomba msaada wako.
 
Wanakufunza mambo muhimu ya kimaisha baba yako na ndugu zako wameshaona umuhimu wako na ufanisi wako wee simamia tu miradi ya ndugu zako ipo siku utaiona faida yake
 
Kumtumikia mzee wako na ndugu zako ni kitu kizuri sana. Jitume kwao kwa roho safi na nyeupe.

Kama hawajadeka kwako wakadeke kwa nani?

Kama unakula na kulala nyumbani kwa baba, ulitaka wasikutume?
 
sioni kama kuna shida wao kukutuma, naona wewe ndo unadhida! kijana uliyemaliza chuo huna kazi huna plan so kubali kusaidia ndugu
what to do! endelea kusaidia ndugu kwa malengo, kwa mfano unaenda kusimamia mashamba ila mwambie mzee wako akupe ekari 2 uzifanyie kazi akikubali meambie sister na broo umepata ekari 2 unataka mtaji wa kwenda kulima ukilima utawarudishia pesa zao
so utaenda kulima with zero mtaji na kwa sbb unasimamia mwenyewe you are guranteed kupata faida while unamsaidia mzee wako
next time unakodi mashamba mwenyewe na kufanya kazi ukipungukiwa unaomba msaada kwa mzee au ndugu zako kwa kuwa umeonyesha juhudi watakupa bila shida
chngamkia fursa kijna, acha kuwaza ajira while waweza kuwa milionea with zero mtaji
 
Dogo, siku zote mzazi hukuona wewe kama mtoto mdogo hata kama una taaluma yako na umekuwa. Sasa ukimuendekeza au ukaishia kulialia bila kujikakamua, utaishia kuw mtoto hivyo hivyo. Omba kazi, usibague eti mpaka iwe ya Taaluma uliyosomea au ya ofisini, omba hata uwaiter. Ile hali ya wewe kuondoka asubuhi na kurudi jioni itawajenga kisaikolojia kuwa uko occupied na kitu fulani. Mshahara wako wa kwanza kapange hata chumba cha elfu kumi ili uanze kujipanga kufanya mengine. Usitegemee mambo yatakuwa sawa automatically, tumia akili na nguvu zako yatakuwa super tu. Wengine Tukisimulia Tulikotoka Hutaamini, basi tu Tunawaangalia vijana mnavyolialia.
 
Dogo, siku zote mzazi hukuona wewe kama mtoto mdogo hata kama una taaluma yako na umekuwa. Sasa ukimuendekeza au ukaishia kulialia bila kujikakamua, utaishia kuw mtoto hivyo hivyo. Omba kazi, usibague eti mpaka iwe ya Taaluma uliyosomea au ya ofisini, omba hata uwaiter. Ile hali ya wewe kuondoka asubuhi na kurudi jioni itawajenga kisaikolojia kuwa uko occupied na kitu fulani. Mshahara wako wa kwanza kapange hata chumba cha elfu kumi ili uanze kujipanga kufanya mengine. Usitegemee mambo yatakuwa sawa automatically, tumia akili na nguvu zako yatakuwa super tu. Wengine Tukisimulia Tulikotoka Hutaamini, basi tu Tunawaangalia vijana mnavyolialia.
Asanteh sana kk...nitafanyia kazi ushauri wako
 
Back
Top Bottom