nimechafukwa
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 290
- 237
Mm ni kijana wa miaka 25 nmemalza chuo fulani mwaka juzi tatizo lililonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni hii swala la kutumika bila manufaa yoyote ninayoyapata
1 . nlivyomaliza chuo baba alinipeleka manyara nikasimamie mashamba yake ya vitunguu mangola bila mshahara wowote(ananihudumia nauli na hela ya kula tu) kwa kweli nilifanya ile kazi kwa juhudi zote ila misimu yote miwili aliyovuna hajanipa hata 100.
2.baada ya project ya baba kuisha kaka yangu alianza ujenzi wa nyumba TEGETA nkaenda kusimamia ujenzi na huyu pia hakuna Lipa.
3.dada yangu ana vi biashara vyake huwa ananituma kufatilia pesa zake pamoja na kupeleka bank karibia kila siku pasipo na malipo pia....kuna kazi nyinyingi ambazo sijazitaja..hii Hali kwa kweli imenishinda kutumika japo ni ndugu zangu na mimi nahitaji kujenga maisha yangu tatizo ajira hamna na wote hao nimejaribu kuwaomba mtaji hakuna aliyenipa kila siku napigwa Dana Dana tu....juzi baba kaniita anataka nirudi manyara kusimamia mashamba yake na kimila kila kitu anachosema baba lazma ufate lasivyo atakuvulia nguo akulaani(apa nafuta machozi ) 😢😢......naomba ushauri ndugu zangu nifanyeje? ?au ni kawaida mm tu ndo nmepanic ?