Ushauri: Naelekea kusitisha kuoa

taboa

JF-Expert Member
Feb 9, 2021
399
711
Habari zenu waungwana!

Mwaka 2019 nilibahatika kupata mwanamke mmoja ambaye ni muajiriwa katika ofisi za umma.Kwa wakati huo alikuwa na miaka 28.

Tulianza rasmi Safari ya mapenzi ambapo kufikia mwaka 2020 mwezi December nilifanikiwa kupeleka barua ya uchumba na baadaye kidogo nikatoa mahari,ndoa ilipangwa kufanyika mwezi wa pili mwaka huu,kwa bahati mbaya nilisafiri ghafla kikazi kwa miezi minne hivyo zoezi likasogezwa mbele mpaka nitakaporudi(katika hili mwanamke alichukia sana kwani alitaka tufunge tu ndoa then nitamkuta nikirudi Ila Mimi sikuona ulazima wa uharaka huo.)

Mwezi wa tano nilirudi salama nikafufua lile Jambo kuwa tufunge ndoa,tukaekea katika mjadala wa tarehe ya harusi ambayo ilikuwa mwezi huo huo wa sita,ajabu siku moja asubuh nilimpigia simu asubuhi akaniambia yupo kwa daktari hosp.nilishangaa kwani sikujua ugonjwa wake kabla akasema akimaliza atanipigia.Baada ya muda kidogo akanipigia kuwa anajisikia vibaya kuwa alikuwa anasumbuliwa na kiuno hivyo ilimlazimu kufika hospital kutibiwa lakini kwa mujibu wake Kuna maswali aliulizwa na daktari.

Daktari alimuuliza kwamba je ana umri gani daktari akamjibu 30, ameolewa?binti akajibu ndio,una mtoto binti akajibu hapana ndipo daktari akamuuliza kwanini hana mtoto binti akajibu hajui shida,kwa mujibu wa yeye daktari akamshauri apimwe hormone levels na afanye ultrasound,kweli binti akafanya hivyo vipimo na kesho yake akapewa majibu kuwa anashindwa kupata mimba kwa kuwa mayai hayapevuki katika ovary zake hivyo Kuna aina ya Kama operesheni afanyiwe ili kutibu tatizo hilo.

Ikumbukwe kwamba haya yalitokea siku chache kabla ya tarehe ya ndoa na wazazi wa mwanamke wakawa wanawasiliana sana na wazazi wangu kuhusu ndoa(binti alifanya haya yote bila kumshirikisha mzazi wake yoyote kwa kigezo kwamba watapata presha sana hivyo akawa anashirikiana na dada yake ambaye amepanga nje ya kwao.

Binafsi nilipinga sana operesheni hiyo kwani Mimi Kama mume mtarajiwa sijawah kuwa na mjadala nayeye kuhusu kupata mtoto nilikuwa nasubir tuzae baada ya ndoa Sasa nikawa namuuliza nini kimekulazimisha kuwa tayari kuingia kufanya operesheni wakati Mimi sijawahi kudai mtoto?majibu hayakuridhisha .

Ukweli tarehe ya harusi ilikaribia zaidi baba mkwe alinipigia simu kutaka kupata mipangilio yetu ya ndoa,kwa upande wangu nilikuwa nimeadhimia kusogeza harusi mbele mpaka amalize hiyo operesheni lakini mwanamke nilipomwambia kuwa akimaliza operesheni ndo tufunge ndoa alikataa sana akaomba Kama vipi akaongee na daktari ili operesheni ifanyike baada ya ndoa,binafsi nilimkatatia Hilo,aliishia kuchukia sana.

Nilipoona hatuelewani ilibidi niwaambie wazaz wangu A to Z ambao nao waliwaambia wakwe Zangu kila kitu,mkwe wangu alichukia sana na akanipigia nifuatilie kuhusu hiyo operesheni Kama kweli atafanya,na ukweli operesheni ilipangwa tarehe 3.6 na ambapo binti aliaga kwao kwamba atasafiri kikaz kwenda Moro goro kumbe ndo ilikuwa aende hosp.bahati mbaya ni kwamba binti akujua Kama mzazi wake tulishamjuza kuhusu Hilo,Ingawa baba mkwe hamkumbishia mwanae akamruhusu tu aende uko Moro then akanipigia simu Mimi nifuatilie Kama kweli ataenda Moro au hospitali,Mimi nikafanya utafiti nikabaini yupo hosp.nikaenda na kumkuta yupo hatua za mwisho za operesheni hiyo Ila bahati mbaya dakika chache wakati anasuburi kuingia kifaa kikaharibika ikabidi iahirishwe mpaka tarehe nyingine,yote haya nilimjuza mkwe wangu ndipo badae akaamuru kuitisha kikao Cha familia yao(mama mkwe,binti,mchumba na ndugu wengine) ili kumwambia anajua kila kitu na Wala hajaenda Morogoro kwa mujibu wa mkwe walimsema sana yule binti na binti akasema basi hatofanta tena hiyo operesheni,mkwe akampigia baba yangu kwamba wamemsema sana binti yao hivyo hatofanya operesheni badala yake tufunge tu ndoa,kiukweli nafsi yangu aikukubali kabisa ilo Jambo.

Nililazimika kumuita binti tujadili kwa kina haswa kuhusu sababu za msingi za yeye kutaka kufanya hiyo operesheni wakati Mimi sijawahi kudai mtoto,yeye aliniambia kuwa kabla yangu alikuwa na mtu Ingawa hajawahi kutafuta mtoto but hajawahi kujizuia kupata mimba na hajawahi kupata mimba,na Mimi nikiri katik miaka miwili niliyekuwa naye tulipima na hatujawahi kutumia kabisa kutumia kondom na hajawahi pata mimba mimba.Kiukweli nilipata msongo mkubwa wa mawazo ya kuamua,kitabia Yuko vizuri sana.

Wakati natafakari hatua za kuchukua nikapata Safari ya miez minne ambapo tunarudi mwezi wa kumi Ila kila nikiwaza ndoa na huyo binti napata kigugumizi sana.

Huyu binti bado anaishi kwa wazazi wake kipindi chote hicho.
IKUMBUKWE MIMI NINA 32YRS NA YEYE 30 YRS.
MAONI YENU TAFADHALI
 
Ukimchunguza sana bata utashindwa kumla.... Wanawake wanamatatizo mengi sana ya mambo ya uzazi kama fibroids, hormones n.k pengine anajua presha za wakwe na mawifi akiolewa ndoa isijibu itakuwa tatizo ameamua kutibu tatizo mapema....sijajua wewe unawasiwasi kwa upande upi, unahisi ametoa mimba au kuna kitu ana kuficha? Kibongobongo kwa sasa wanawake wachache sana wenye umri zaidi ya 28 hawajazaa wakuhesabu na ukifuatilia kuna sababu kwahiyo na yeye amefika 30 hajazaa na game amepiga miaka kibao ukute kuanzia akiwa na miaka 18 basi ameona ana tatizo.

Mtafute daktari wake private funguka muombe akuweke wazi tatizo ni lipi haswa.
Mi naona mchumba amejongeza kujiweka sawa kuingia kwenye ndoa na tabia umesema yuko poa, ujue watoto ni majaliwa yake mola.

Wewe oa tu mengine ya watoto mtajua mbele ya safari kama operesheni itamsaidia wacha atibiwe awe na amani.
 
Habari zenu waungwana!

Mwaka 2019 nilibahatika kupata mwanamke mmoja ambaye ni muajiriwa katika ofisi za umma.Kwa wakati huo alikuwa na miaka 28.
Funga ndoa ,afu huku unasafiri afanye operesheni. Ukifka 30 hujapata mtoto unakuwa na kimuyemuye cha mtoto hata kama hajaolewa cha muhimu
 
Binafsi naona kama ipo sababu ingine tofauti na hio labda tu Mungu anaepusha... kuhusu uzazi sikuhizi katika wanawake 10 basi 8 wana tatizo la hormone, imenitokeaga nimekaa na mwanaume miaka mi4 sijawahi kuzuia mimba na sikupata baadae homoni zimekuja kukaa sawa kwa jambo dogo,sasa kama ni ndoa si unasema tasa, kama tatizo ni homoni naamini zinakaa sawa.
 
Binafsi naona kama ipo sababu ingine tofauti na hio labda tu Mungu anaepusha...
kuhusu uzazi sikuhizi katika wanawake 10 basi 8 wana tatizo la hormone, imenitokeaga nimekaa na mwanaume miaka mi4 sijawahi kuzuia mimba na sikupata baadae homoni zimekuja kukaa sawa kwa jambo dogo,sasa kama ni ndoa si unasema tasa, kama tatizo ni homoni naamini zinakaa sawa..

Dada ulifanya nn kuweka homoni sawa. hebu nisaidie
 
Binafsi naona kama ipo sababu ingine tofauti na hio labda tu Mungu anaepusha...
kuhusu uzazi sikuhizi katika wanawake 10 basi 8 wana tatizo la hormone, imenitokeaga nimekaa na mwanaume miaka mi4 sijawahi kuzuia mimba na sikupata baadae homoni zimekuja kukaa sawa kwa jambo dogo,sasa kama ni ndoa si unasema tasa, kama tatizo ni homoni naamini zinakaa sawa..
Hormone zilionekana sawa shida mayai hayapevuki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom