Ushauri na Mwongozo: Biashara ya nyama ya kuku wa kienyeji

uzeebusara

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
657
514
Habari wajasiriamali
Naomba kupata ushauri na mwongozo ikibidi katika biashara ya kuuza nyama za kuku wa kienyeji kwa kilo na kwa oda.
Hii ina maana kwamba natafuta supermarkets na hoteli kubwa kwa hapa Dar Es Salaam nawauzia. Sasa je kwa wenye ufahamu naomba nijazwe katika haya
1. Malipo yao huwa kwa cash papo kwa hapo au kwa credit?
2. Kama kwa credit inachukua muda gani kulipwa?
3. Uhitaji wa kuku inawezekana ikafikia kilo ngapi labda kwa wiki au mwezi nk
4. Uwezo wangu unatakiwa niwe napata kama kilo ngapi hivi kwa mwezi mzima?
5. Biashara hii inalipa kwa aliyewahi kuifanya?
6. Je inachangamoto zipi

Asanteni
 
Mkuu haya makuku ya kisasa unadhani wengi wetu tunayapenda.......Mimi huwa sili kabisa......tatizo Kuku wa kienyeji mpaka umnyonyoe umfanye hivi......so nadhani ukiweka sokoni itakulipa sana......
 
Back
Top Bottom