Waziri Shamata Shaame Khamis: Uzalishaji wa nyama ya kuku Nchini ni tani 1,161 na Mahitaji ni takriban tani 24,567 kwa mwaka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,919
13,669
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, na wawekezaji ili kuleta mageuzi ya haraka katika tasnia hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha programu za pamoja za utafiki kati ya nchi za SADC ili kushughulikia changamoto zinazofanana zikiwemo udhibiti wa magonjwa na teknolojia za kuboresha ufugaji.

Waziri Khamis ameyasema hayo wakati akifunga jukwa la Tasnia ya kuku na ndege wafugwao kwa nchi za kusini mwa Afrika 17 Oktoba 2024

Aidha amesisitiza Kufungamanisha kanuni na viwango vya ufugaji kuku katika nchi za SADC ili kuwezesha biashara za kikanda na kuhakikisha usalama wa mazao ya kuku na bidhaa zake

Pia amesisitiza Kuendeleza programu za mafunzo za kikanda kwa wafugaji, madaktari wa mifugo, na wafanyakazi wa ugani ili kuongeza ujuzi katika usimamizi wa kisasa wa kuku na ustawi wa wanyama.

Kadhalika amesihi Uwekezaji katika Miundombinu ya uzalishaji wa kuku na ndege wafugwao: kama vile vyumba baridi (cold room facilities), machinjio, vifaa vya usindikaji

Mbali na hayo ameelekeza kuwepo kwa ushirikiano katika teknolojia bunifu ili kuongeza tija ya uzalishaji na biashara ya kuku.

Waziri Khamis amefafanua kuwa mahitaji ya nyama nyeupe duniani kote yanaendelea kuongezeka ambapo Takwimu zinaonesha kuwa Zanzibar ina jumla ya idadi ya kuku 2,485,606 ambapo kuku 762,333 ni wamayai, kuku 986,039 wa nyama na kuku 737,234 wa asili.

Aidha, uzalishaji wa nyama ya kuku ni takriban tani 1,161 kwa mwaka ambapo tani 3,881 kwa mwaka huagizwa kutoka nchi mbalimbali, na mahitaji ya nyama ya kuku ni 9 mji takriban tani 24,567 kwa mwaka.

“Ni wazi kuwa tukidhamiria kuwekeza soko la uhakika wa nyama ya kuku na ndege wafugwao lipo. Hali hii ya uhitaji wa nyama nyeupe ipo pia kwa upande wa Tanzania visiwani (Zanzibar), kama ilivyo kwa Tanzania bara.

Kutokana na Zanzibar kuwa kitovu cha utalii na uwepo wa hoteli za Kimataifa, mahitaji ya nyama nyeupe ikiwemo ya kuku ni makubwa. Hivyo hii ni fursa ya kujenga uwezo wa ndani na kuimarisha uwekezaji katika uzalishaji wa nyama ya kuku ili kukidhi mahitaji hayo” Alisema

Kutokana na hivyo, Waziri Khamis alitoa rai kwa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha tasnia ya kuku na ndege wafugwao, ili kupunguza/kuondoa changamoto/vikwazo vilivyopo katika tasnia hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa AGRA Tanzania, Vianey Rweyendela amesema wanakuja na mpango wa kupunguza uagizaji wa kuku na bidhaa zake kutoka nje ya eneo la SADC kwani asilimia 50 ya bidhaa za kuku na kuku wenyewe wanaotumika katika nchi za SADC inatoka nje

“Hii maana yake tunakwenda kwenye upotevu wa fedha za kigeni ambazo zingetumika
Kwenye vitu vingine hivyo tumekubaliana kuwa na mipango mmoja ambayo itakua chini ya SADC ikiwa inaangazia haya masuala yote yanayohusiana na kuku na ndege wafugwao”

“Umuhimu wake ni kwamba tutaongeza ustawi wa wakulima kwa kuwaongezea tija na faida lakini pia ustawi wa jamii kwa kuongeza kipato”
 
Back
Top Bottom