Ushauri na msaada wa biashara nzuri ya kufanya

senzoside

Senior Member
Mar 13, 2012
183
31
Habari za muda huu wandugu
Mm ni kijana mwnaume nina umri wa miaka 25 nafanya kazi kwenye shirika fulani la kitalii hapa mjini Moshi Kilimanjaro kazi yangu namshukuru Mungu inanilipa kwasasa nina hela taslimu shilingi milioni 20 kama mtaji niifanyie biashara gani itakayoweza kunilipa vizuri ambayo naweza kuifanya huku nikiwa naendelea na kazi yangu kazini kwenyewe ni kuanzia saa 2 asubuhi mpaka sasa 10 jioni.
Asanteni karibuni kwa michango yenu
 
nafanya kazi kwenye shirika fulani la kitalii hapa mjini Moshi Kilimanjaro kazi yangu namshukuru Mungu inanilipa kwasasa nina hela taslimu shilingi milioni 20 kama mtaji niifanyie biashara gani
..biashara inayoendana na kazi yako..., itakubidi umwajiri mtu wa kusimamia wakati wewe haupo.
 
Nakushauri fanya biashara ya kununua mazao kipindi cha mavuno uyauze yakipanda bei. Mfano babati wakivuna mwanzoni kabisa gunia la mahindi ni sh 30000-35000. Baada ya miezi 3 unauza kwa 60000 na kuendelea 80000 Mtaji wako unaruhusu. Ukifungua biashara ya kuajiri mtu hiyo 20000000 wataigegeda yote
 
aisee mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako kwani hii itanipa faida na hamna mtu atakaye niibia
 
hahaha bora hata umemjibu umeoa,maana nlikua cjaelewa huko kuoa kuna relate vp na hyo biashara+mtaji??

labda alikuwa anataka ashauri kama cjaoa nioe ili mke asimamie hizo biashara
ila mkuu kama na ww una ushauri mwingine karibu sana kwasababu biashara unatakiwa kuwa makini sana
 
Back
Top Bottom