Ushauri: Msio na ajira, ombeni ualimu shule binafsi

Ushauri: Msio na ajira, ombeni ualimu shule binafsi

KILLANEKELI

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
295
Reaction score
123
Napenda kuwashauri wale ndugu zangu waliosoma course tofauti na uwalimu na wako mtaani wakizunguka na bahasha za kaki,

Kutokana na tatizo la ajira kugeuka kuwa janga la kitaifa na serikali imetangaza mwaka huu kuajiri zaidi ya walimu elfu 30 napenda kuwashauri ndugu zangu muombe kujishikiza ata private schools huku mkiendelea kufanya application ya field zenu.

Kwanini nasema hivyo, kwa sasa kuna waalimu wengi sana wamejishikiza private schools wakisubiri ajira serikalini hii inamaanisha kwamba shule za Private zitaenda kuwa na upungufu waalimu sasa hapo ndio muda wa nyie kuchukua nafasi,

Nina rafiki yangu alisoma PSPA akaomba shule moja ya private uku akikomaa kutafuta kazi ya taaluma aliyosomea mambo yalikuja kukaa sawa leo ni afisa utumishi wa wilaya moja ivi, kile kitendo cha kuwepo private school kilichangia kupata ajira ya taaluma aliyosomea ingawa alikuwa akipata mshahara wa kawaida lakini ilimsaidia kwa kiasi kikubwa wakati Wa kusafiri kwenda kufanya usahili.
 
Mleta uzi big up, nakumbuka niliwahi kushauri kama hilo miaka miwili mitatu iliyopita.

Mimi mwenyewe nilipitia kwenye kujichanganya mitaani sana sikubagua kazi. Nakumbuka baada ya kidato cha Sita wakati nasubiria majibu niliomba kibarua Tanga Cement kwa kutumia sifa ya Form 4, lakini kutokana na uelewa mkubwa wa kazi na kujieleza kutumia lugha ya Wazungu nilipandishwa cheo kuwa Shift Supervisor nikawa nakula hela nzuri.

Nilipopata nafasi Chuo kikuu nikasepa na baada ya Chuo sikujipandisha mabega nikatafuta shule moja ya Kimataifa nikawa nafundisha Somo la ICT. Somo lenyewe miaka ya 90 hata Sylabus ya kitaifa haikuwepo basi wanafunzi walikuwa wanafundishwa basic operation na kucheza game tu, mwisho wa mwezi mshahara kibindoni.

Wakati huo unakutana na watu mbalimbali sehemu za kutumia na kufahamiana nao. Mungu si mwanadamu connections zikapatikana humo humo na baada ya muda mfupi nikaingia rasmi kwenye fani niliyosomea ya Computer Science.

Vijana wa leo muache kuwa na maono ya kampuni kubwakubwa tu vichwani mwenu pindi mtokapo vyuoni au shuleni.
 
hivi kwan ualimu private kama umesomea taaluma hyo upatikanaji wake ukoje? niwakuzunguka sana na bahasha au kawaida tu
 
hivi kwan ualimu private kama umesomea taaluma hyo upatikanaji wake ukoje? niwakuzunguka sana na bahasha au kawaida tu
Inategemea na masomo uliochukua wakati unasoma kama ni science+ geography au language ni rahic sana kupata
 
Mimi ni shahidi wa uyasemayo.

Tena mimi nilikuwa nafundisha Tuisheni Centre tu ambayo ilikuwa inanipatia 20,000/- kwa siku na mwisho wa wiki 40,000/- kwakweli kazi ya kufundisha ilinibeba sana, kununua magazeti, kuchapa barua na cv, kuhudhuria interviews, kulipa kodi ya chumba, matumizi yangu ya kila siku.

Nashukuru ulikuwa ni msingi wa kazi niifanyayo sasa.

Niseme ukweli sikuwahi kutafuta kazi under presha na nilipokuwa naona mshahara ni kidogo kwenye sehemu nimefanya interview siendi kwakuwa nilikuwa najua niko kwenye Centre yangu.
 
Mimi ni shahidi wa uyasemayo. Tena mimi nilikuwa nafundisha Tuisheni Centre tu ambayo ilikuwa inanipatia 20,000/- kwa siku na mwisho wa wiki 40,000/- kwakweli kazi ya kufundisha ilinibeba sana, kununua magazeti, kuchapa barua na cv, kuhudhuria interviews, kulipa kodi ya chumba, matumizi yangu ya kila siku. Nashukuru ulikuwa ni msingi wa kazi niifanyayo sasa. Niseme ukweli sikuwahi kutafuta kazi under presha na nilipokuwa naona mshahara ni kidogo kwenye sehemu nimefanya interview siendi kwakuwa nilikuwa najua niko kwenye Centre yangu.


Safi Sana kijana utafika mbali kimaisha.
 
Hata mimi naunga mkono hoja ya ndugu yetu.....nami baada ya kumaliza BA yangu ya Uchumi nikajashikiza high school fulani...imenisaidia sana tu...
 
Hata huo ualimu wa shule binafsi kuupata ni ishu....sio lahisi kama kunywa maji baridi katika jua kali la Dar es salaam...
 
Back
Top Bottom