Ushauri: Mchumba wake ana mapenzi ya msimu

maimatha

Senior Member
Mar 2, 2013
129
161
Kuna mdogo wangu mi nashindwa jinsi ya kumshauri,

Anamchumba wake/mpenzi hawana mda mrefu tangu wamefahamiana walikutana kwenye mtandao wa kijamii wakapendana wakakutana wakafahamiana na kuanza safari ya mapenzi/uchumba anadai tabia ya jamaa inampa shida kudogo.

Jamaa anamapenzi ya msimu anaweza akaibuka na mapenzi motomoto bby, make wangu, my love za kufa mtu baada ya mda inakua kimya hata wiki 1, au 2 badae anakuja kwa kasi tena anashindwa kumuelewa anapomuuliza jamaa anadai kazi nyingi.

Wakati mwingi inaweza pita wiki jamani hampigii simu ni msg tu whatsup wanachart siku inaisha jamaa anaishi Dar jamaa akiwa Dar mawasiliano yanapungua hata kasi ya mapenzi inapungua ila akusafiri tu mapenzi yanapamba moto kajaribu kuongea na jamaa anamwambia wasiwasi wako tu mi nakupenda sana due!

Mi naombeni tusaidizane kumshauri huyu dada.
 
Kwanza weka bayana ni wapenzi au wachumba? Pili wamekutana kweny mtandao afu anataka kupigiwa cm badala ya kukutania pale walipokutania ili penzi lao liwe na hisia zile za mwanzo...but all in all mpenzi anayepatkana ktk mtandao uwa ni wa pili na c wa kwanza MPE pole rafk.
 
Ngoja leo nipite kimya....
Maana bado nina figisu fully majanga humu jf aiseeee
 
Ngoja leo nipite kimya....
Maana bado nina figisu fully majanga humu jf aiseeee
Ushaongea tayari! Kimya gani hyo?! Jamaa mjanja sana huyu anacheza na saikolojia ya huyo dada inahitaji mtu mwerevu sana kuelewa anachofanyiwa hapo
 
Aiseee....! Huenda anamke\au mchumba mwingine maaana sio hali ya kawaida.

Ila pia kuna watu Wa mapenzi ya msimu. Hususani akishapata game.

Cha msingi akomae kumbadilisha taratibu Huyo jamaa!! Au kumchunguza Huyo jamaa.
 
hapo ahesabu kaliwa jamaa anaish na mtu mke ,mpenz au mchumba.. yoyote.. so akiwa dar inakua shidah mawasiliano..
ajikubali ye ni spare.
 
Aiseee....! Huenda anamke\au mchumba mwingine maaana sio hali ya kawaida.

Ila pia kuna watu Wa mapenzi ya msimu. Hususani akishapata game.

Cha msingi akomae kumbadilisha taratibu Huyo jamaa!! Au kumchunguza Huyo jamaa.
Kumbadilisha binadamu mwenye meno yake 32? She is not an agent of change, labda mkaka atake kubadilika mwenyewe. Na sioni kama kuna cha kubadilika, labda dada afanye uchunguzi kuridhisha nafsi yake then achape lapa
 
Back
Top Bottom