Ushauri: Mchepuko umemkamata anataka kumuacha mkewe

Ushauri: Mchepuko umemkamata anataka kumuacha mkewe

msweken

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
441
Reaction score
1,717
Salaam kwenu waungwana,

Nina changamoto ambayo sijui ninaitatuaje mkasa upo kama ifuatavyo;

Ninae rafiki yangu wa dhati sana tangu kitambo kile tungali wadogo mpaka umri huu wa utu uzima, tumepitia mengi na kutenda mengi pamoja mpaka tumekua kama ndugu, changamoto yangu ni yake na yake ni yangu vivyo hivyo isipokua hii changamoto ni yangu peke yangu.

Mimi na huyu rafiki yangu tumeoa marafiki haswa ( wake zetu nao ni marafiki kama ndugu, imefika mahali wanangu wanamuona rafiki yangu kama baba yao mdogo na mke wa rafiki yangu kama mama yao mdogo.

Jamaa na mkewe wanaishi mikoa tofauti tofauti (anko Magu alitenda miujiza yake kwa kumpeleka mmoja Dodoma na kumuacha mwingine Dar)

Jamaa yupo Dar, sasa jamaa kaokota mwanamke mwingine Dar na amemkamata kuliko kawaida kiasi kwamba anataka aachane na mkewe (huyu mchepuko tishio namfahamu mimi tu, wake zetu hawajui).

Mkewe ni mtu mmoja mstaarabu sana, yaani ni wale wife material by birth na by registration. Mke wa jamaa ni dizaini ya wale wanawake ambao hata Yakobo na Yohaya wangegeuka leo hii na wao wangetamani kuwaoa, hanaga mauza uza, wanajitegemea kikipato, hana madrama ya kina Mwajuma.

Changamoto inakuja kuwa jamaa kakengeuka na mchepuko anataka piga chini mke wake, na wife wake nae anataka kudai talaka (jamaa hajui).

1. Namuonea huruma dada wa watu kwa namna anayotendewa na mshaji maana mshkaji ni mambo mengi sana alafu hana staha kwa mkewe ( hata mimi nina chepuka ila kwa staha). Nashindwa kumsaidia abaki ilihali anateseka kwa mshkaji.

2. Namuonea huruma mshkaji maana kwa namna navoyajua makunguru hatopata kirahisi mwanamke kama mkewe anaetaka kumuacha.

Sasa waungwana tusaidiane hapa:
Nimsaidiaje rafiki yangu asivunje ndoa yake? Au nimuache yamfike ya mwana kumtaka mwana kumpata?
Nimsiadiaje mkewe nae awe na furaha maana amekua ni kama ndugu kwa mke? Nimuache aachane na mshkaji?

Note: Mwanamke akipata changamoto yoyote katika ndoa yao huwa anakuja kuomba ushauri kwetu kwanza kwa maana anatuamini mimi na mke wangu.
 
Unajua wanaume tuko na akili za ajabu sana linapokuja suala la kutumia kichwa cha chini badala ya cha juu ktk kufikiri/kutafakari na kuamua mambo. Hapo ukimbana rafiki yako aachane na huyo mwanamke mchepuko mnaweza mkaishia kuvunja hata huo urafiki wenu

Namuonea huruma tu huyo mke halali wa ndoa yake.

Binafsi ningeacha tu kama lilivyo. Wapendanao wakihitilafiana................
 
Namna pekee ya kumsaidia jamaa wewe mgegede tu huyo wife wake maana kwa sifa ulizomwaga hapa naamini wewe mwenyewe unamtamani shemeji yako
 
Sometimes, shika jembe ukalime ni ushauri mzuri!

Mara nyingi kwenye counselling tunashauriwa sana kutotoa majibu (solutions) watu wanapokuja na matatizo yao kwa sababu deep within them KILA MTU ANALO JIBU la tatizo lake.

Kwa maelezo yako, unaendeshwa na hisia na hufai kabisa kuwa mtoa solution kwenye situation yao. Haimaanishi unakuwa rafiki mbaya, la hasha.

- Kama mke akija msikilizeni tu. Msimkatishe, msimfukuze. Msikilizeni tu. Katika maneno yake mwenyewe atapata solution.

- Huyo rafiki yako wa kiume naye anapokuja kukushirikisha mipango yake ya kumuacha mkewe. Msikilize tu. Usimkatishe, usimfukuze.

- Ushauri pekee mnaoweza kuwapa ni, "Hebu nenda ukafikirie tena mwenyewe. Kaa tulia ufikirie tena nini hasa unachotaka kufanya." Watieni moyo kutokuogopa kuwaza peke yao.

- Mwisho, ingependeza nawe ukaacha michepuko au mkeo si wife material!??
 
it sometimes happen...thou long distance relationship nayo ni changamoto sana
-you sometimes miss the dude its not there
-you sometimes miss his presence he's not there and so many so many..

penye miti mingi hakuna wajenzi

cc Smart911
 
it sometimes happen...thou long distance relationship nayo ni changamoto sana
-you sometimes miss the dude its not there
-you sometimes miss his presence he's not there and so many so many..

penye miti mingi hakuna wajenzi

cc Smart911
Na penye wajenzi napo hapana miti kabisa
 
Nilichojifunza ni kwamba unamtamani shemeji yako.. Weka ndani kama dini ilaruhusu
 
Back
Top Bottom