Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda. Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko. Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.Mkuu inategemea unataka kwenda inchi gani kujilipua. Zipo inchi zipo ulaya lakini utatamani ubaki Africa..sasa wewe nidokeze unataka uende inchi gani?
Wewe ndio useme ni nchi gani, wewe si ndio unazifahamu au?Mkuu inategemea unataka kwenda inchi gani kujilipua...zipo inchi zipo ulaya lakini utatamani ubaki Africa..sasa wewe nidokeze unataka uende inchi gani?
Mkuu ni kweli. Uhamiaji hawatoi passport bila reason. Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.Binafsi uzi huu nauunga mkono 100% Lakin pamoja na hayo bado kuna changamoto nyingi kufikia hatua ya kuondoka nchini, kuna mambo mengi ambayo niya msingi hasa upande wa Serikali yetu tukufu hasa upande wa Idara ya uhamiaji. Tz yetu mtu kupata the tu cheti cha kuzaliwa ambacho ni haki ya Mzawa mpaka jasho likutoke, na ikiwezekana na rushwa juu utoe. Ukienda Migiration ili kuanza mchakato wa passport utahenya vibaya,
Kupata card ya chanjo ya homa ya manjano mpaka utahenya.
Lakini pia changamoto nyingine ni mtu kupata Nauli kamili ya kukufikisha mahari unako taka kwenda.
Binafsi ninacho elewa wakirahisisha hayo mambo ya juu, naona Tanzania inaweza kubaki na wazee tu,
Sasa nchi gani hii isiyo toa ajira, Mali asili ni nyingi lakini hatujui wala hatuoni uthamani wake, Vyeo vya juu wanapeana wao kwa wao
HAKI YA MUNGU MIMI SIKU NIKIONDOKA NDO BASI TENA. BORA NIKAFIE KWA FARAO KULIKO KANANI AMBAKO SIJAWAHI FIKA.
Wangefanya hivyo. Siku nyingi ningekuwa sauzi. Walinipa form zao zile. Zina maswali hatari zikazichoma moto.Mkuu ni kweli. Uhamiaji hawatoi passport bila reason. Nafikiri tungebadili huu utaratibu tuwe kama wenzetu ambao passport kwao ni haki ya msingi na unaweza miliki tu.
Ufanikiwe ndugu, maisha ya bongo unanyonga tai kali mwisho wa mwezi unaondoka na hela ambayo haitoshi hata robo ya mahitaji.Mkuu, mwaka huu nimeomba scholarship kwenda kusoma Australia, China na UK
Niombeeni nifanikiwe ,nijilipue huko, nafanya kaxi ila haina maslahi na wategemezi lukuki, bora nitokomee huko kwanza
Mimi nataka kwenda Denmark. Naomba jinsi ya kuingia na fursa zilizopo huko zisizohitaji elimu.yaani nguvu kazi.Mkuu hii ni thread maalumu kwa kupeana uzoefu wa majuu na namna ya kwenda. Ni maalumu kwa wenzetu wanaohitaji kwenda huko. Sio mimi ninayehitaji nimeweka kwa niaba ya wengine. Nimeshaishi USA for 8 years na Denmark.
So ili kupunguza wimbi la thread za ushauri ni vizuri tutiririke hapa ili wengine wajifunze.
Denmark ni nchi ya scandinavia. Ni nchi yenye maisha ya raha na amani sana japo ni nchi ndogo. Njia rahisi kwenda huko unaweza kwenda as tourist then ukifika huko unapambana upate wa kumwoa hata kwa makaratasi tu ili upate kibali cha ukaazi.Mimi nataka kwenda Denmark. Naomba jinsi ya kuingia na fursa zilizopo huko zisizohitaji elimu.yaani nguvu kazi.