Volatility
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 3,920
- 7,469
Najua kwa sasa machafuko ya huko Msumbiji yanakukosesha usingizi, ukizingatia ukaribu wa Taifa letu na maeneo ambayo Majeshi ya Serikali ya Msumbiji yameshindwa kudhibiti hao tunaombiwa ni magaidi.
Mimi naomba nikutie moyo, hofu yako ni sahihi, na ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe busara za kukabaliana na changamoto hizo.
Ni Mategemeo yangu kwamba washauri wako wa masuala ya ulinzi na usalama, na Majeshi yetu yako tayari kukabiliana na changamoto hizo, na mpaka sasa ninaunga mkono maamuzi ya Serikali yetu kuzuia wakimbizi wa machafuko huko Msumbiji kuweka kambi nchini mwetu, endelea na msimamo huu mpaka dakika ya mwisho.
Lakini, ukirudi, ukirudi kutoka Kampala tuondolee Sirro. Vilio, majonzi, machungu, na hasira za wananchi wa Taifa hili dhidi ya Serikali yako na Magufuli ni namna Jeshi la Polisi chini ya Sirro lilivyoshindwa kujiweka mbali na matukio ya utekaji nyara na mauaji ya Raia katika mazingira yaliyoonekana kuwa ya kisiasa.